Thursday, December 6, 2012

Mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite akutwa amekufa hotelini

MFANYABIASHARA wa madini aina ya Tanzanite mkoani Arusha,Ngerii Olerumwa anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 40 amekutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha ndani ya hoteli ya Premier Palace ambayo timu ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano imeweka kambi hotelini hapo jijini Arusha.

Maiti ya mfanyabiashara huyo iligundulika majira ya saa 3 ;30 asubuhi leo mara baada ya mhudumu wa hoteli hiyo kugonga kwa muda mrefu mlango wa chumba alichokuwa amefikia marehemu huyo bila mafanikio na kisha kubaini alikuwa amefariki dunia.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo meneja wa hoteli hiyo ambaye alikataa kutaja jina lake hadharani alisema kwamba marehemu huyo aliwasili hotelini hapo mnamo desemba 3 mwaka huu majira ya saa 1 ;00 jioni na kukodi chumba kimojawapo hotelini hapo.

Meneja huyo akisimulia tukio hilo alisema kwamba marehemu aliwasili akiwa peke yake hotelini hapo na kubainisha kwamba yeye ndiye alikuwa mtu wa mwisho kukodi chumba hotelini hapo.

Hatahivyo,alidai kwamba ilipotimu leo majira ya saa 3 ;30 asubuhi wakati mhudumu wa hoteli hiyo akigonga mlango wa chumba alichofikia marehemu kwa lengo la kufanya usafi mlango huo haukuweza kufunguliwa kwa wakati hali iliyowapelekea kufanya juhudi za kuufungua mlango huo kwa lazima.

Alisema kwamba baada ya kufanikiwa kuufungua mlango huo walijaribu kumwamsha marehemu lakini hakuweza kuamka hali iliyowapelekea kuliarifu jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo.

Mwandishi wetu ilipofika maeneo ya hoteli hiyo iliwashuhudia askari wa upepelezi kutoka jeshi la polisi mkoani hapa wakichukua maelezo kwa baadhi ya watumishi wa hoteli hiyo wakiwemo walinzi wa hoteli hiyo huku baadhi ya wabunge wanaounda timu ya wabunge wa bunge la jamhuri wakitaharuki kutokana na tukio hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti ndugu wa marehemu ambao walikusanyanya nje ya hoteli hiyo walisema kwamba wameshtushwa na kifo cha ndugu yao na wanahisi kwamba aliuwawa katika mazingira ya kutatanisha huku wakilitaka jeshi la polisi kubaini chanzo cha kifo cha marehemu.

Akihojiwa na waandishi wa habari kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoani Arusha Liberatus Sabas,alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza kwamba jeshi lake linachunguza kwa kina kifo hicho.

Sabas,alisema kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti ndani ya hospitali ya mkoa ya Mt,Meru na atatoa taarifa kamili ya tukio hilo kuanzia leo mbele ya waandishi wa habari.

PRECISION AIR YAZINDUA NDEGE YAKE MPYA AINA YA ATR 42-600

 Waziri wa Uchukuzi (wa tatu pichani) kutoka kulia, Mh.Dkt Harisson Mwakyembe akikata keki kuashiria uzinduzi wa  ndege yao mpya aina ya ATR 42-600, kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar, kulia kwake ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo, Michael Shirima na shoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Alfonse Kioko kwa pamoja wakishuhudia tukio hilo adhimu.
 Waziri wa Uchukuzi (wa tatu pichani) kutoka kulia, Mh.Dkt Harisson Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Watendaji wakuu wa Shirika la Ndege la Precision, wakati wa uzinduzi wa  ndege yao mpya aina ya ATR 42-600.
 Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki uzinduzi wa ndege hiyo mpya aina ya ATR 42-600 wakiipanda.
Precision Air yazindua ndege yake mpya aina ya ATR 42-600.

.Yaanza kufanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Kilimanjaro
.Hatua hiyo ni miongoni mwa mwendelezo wa uboreshaji wa huduma zake

Shirika la Ndege la Precision limezindua ndege yake mpya aina ya  ATR 42-600, ikiwa ni hatua ya mwendelezo wa maboresho ya miundombinu ya shirika hilo kwa maslahi ya wateja wake. Hata hivyo uzinduzi huu ni sehemu tu ya mkakati wa miaka mitatu, ambapo katika kipindi hicho, shirika limepanga kuongeza aina kama hii ya ndege za (ATR) hadi kufikia idadi ya ndege 5, mradi utakaogharimu kiasi cha Dola milioni 95.

Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo, Michael Shirima, alipongeza hatua ya uzinduzi huo, ambapo alisema itasaidia kwa kiasi kikubwa kuleta mapinduzi katika sekta ya usafirishaji wa anga. “Ndege hii  mpya na ya kisasa ya ATR 42 - 600 ina zaidi ya viwango vinavyohitajika katika huduma ya usafiri wa anga, ina muundo wa kipekee uliotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu,  na inaweza kufanya huduma zake hata kwenye maeneo ya miundombinu duni,” alisema Shirima.

Katika mwendelezo wa uboreshaji wa huduma zake, Precision imeendelea kupeleka ndege zake ndogo mikoani na kuahidi kuendeleza azma yake ya kuwa kitovu cha utoaji wa huduma bora za anga nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Alfonse Kioko, alisema upanuzi wa wigo wa huduma za anga katika shirika hilo, ni miongoni mwa mikakati ya kuhakikisha wateja wake wanafurahia ufanisi na huduma za usafiri huo, sanjari na kupunguza adha na usumbufu kwa wateja .  “Ni fahari kubwa kwa Tanzania kupitia shirika la ndege la Precision kuwa taifa la kwanza katika bara
la Afrika kuingiza ndege hii ya kisasa na iliyotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu,”alisema Kioko.

“ATR 42-600 inakidhi matakwa na mazingira ya ukuaji wa miundombinu katika maeneo mengi barani Africa jambo ambalo linatupa hamasa ya kuongeza masafa na uboreshaji wa huduma zetu katika hali ya ufanisi zaidi.” Precision Air ina wigo mpana na imejiimarisha zaidi katika kuhakikisha inafikisha huduma zake katika mikoa yote. Shirika hilo ni la kwanza kati ya mengi yaliyopo nchini, kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam, DSE.

Aina hiyo ya ndege itasaidia kupanua wigo wa usafiri wa anga unaofanywa ndani ya shirika hilo kwa safari za ndani na nje ya Tanzania. Hata hivyo shirika liko mbioni kuanzisha safari zake katika mikoa inayokua kwa kasi kama Mtwara.

“Maeneo mengine tunayoyatazama ni mkoa wa Mbeya punde tu uwanja wake mpya utakapozinduliwa mwakani, Bukoba na Kigoma ambapo viwanja vyake bado vipo kwenye matengenezo.”

DAKTARI WA ‘MOI’ MUHIMBILI, NESI WAKE MBARONI KWA RUSHWA

 Daktari Matiko (katikati) akiongozwa na Afisa wa Takukuru (nyuma yake).  Aliyetangulia ni wakili anayemtetea, Paschal Kamala.
                                                                 …Akielekea kizimbani kwa upole.
                      Nesi KImwomwe (kulia) naye akielekea kizimbani kusomewa mashitaka yake.
                                           Uchungu wa safari ya kuelekea kizimbani.
                    Ndugu na jamaa wakifuata nyuma kwa ajili ya kusikiliza kesi za wapendwa wao.

DAKTARI wa hospitali ya Muhimbili Kitengo cha Mifupa (MOI), Deodata Kisasi Matiko (30) na nesi wake, Erick Petro Kimwomwe (28), leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakishitakiwa kwa kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni moja waliyomwomba Stanford Aaron Mhina ili wamfanyie upasuaji wa mgongo ndugu yake aitwae Fanuel Daniel Gideon aliyelazwa Wodi ya Sewa Haji namba (18) Kitengo cha Mifupa (MOI). Imedaiwa kuwa mgonjwa huyo alipelekwa MOI baada ya kupewa rufaa na Hospitali ya Tumbi iliyopo Kibaha mkoani Pwani ambapo alifikishwa hospitalini hapo baada ya kupata ajali ya gari maeneo ya Kibaha na kuvunjika mgongo.
                                              

PICHA : RICHARD BUKOS / GPL  

HAPPY BIRTHDAY JACQUELINE WOLPER

MSANII Jacqueline Wolper ambaye pia ni Ijumaa Sexiest Girl 2012, leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa. Wolper alizaliwa mkoani Moshi Desemba 6, mwaka 1988 na leo ametimiza umri wa miaka 24. Mtandao huu unamtakia kila la heri katika siku hii muhimu katika maisha yake. Happy Birthday Jaque!

Wananchi Watembelea Banda La Tume Ya Katiba

Mkazi wa Jijini la Dar es Salaam, Bw. Joseph Msindai akizungumza na Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bw. Amour Kagya (kulia) katika banda la Tume hiyo leo (alhamisi Disemba 6, 2012) wakati wa maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu Duniani yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
 (PICHA NA TUME YA KATIBA)

Mwandishi Aliyepigwa Risasi Anaendelea Na Matibabu MOI


Ndugu wapendwa, DSM City Press Club imepata taarifa za kushtusha kufuatia ya kupigwa risasi na kujeruhiwa begani kwa mwandishi wa Tanzania Daima Bwana Shabani Matutu (30) ambaye pia ni mwanachama wa Dar City Press Club (DCPC). Sambamba na taarifa hizo imeelezwa kuwa mwandishi huyo amelazwa katika Taasisi ya mifupa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MOI). Chanzo hasa cha kupigwa risasi kwa mwandishi huyo bado hakijaeleweka kwa DCPC, uongozi wa DCPC unafuatilia. Tutakapojiridhisha na taarifa zilizotolewa pamoja na zile tutakazozipata tutawataarifu rasmi. Kwa sababu hizo tunaomba waandishi wote, ndugu, jamaa, marafiki, wapenda haki na amani, wanaharakati washirika na wadau wote wa vyombo vya habari kuwa watulivu tukimjulia hali kwa misaada ya hali na mali mwandishi mwenzetu Shabban Matutu ili apone majeraha

Walimu Wakimbia Shule Kwa Kubakwa Na Wanafunzi

 WALIMU wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Ruaruke wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, wameitelekeza shule hiyo kutokana na kukithiri kwa vitendo vya baadhi ya wanafunzi kuwadhalilisha kimapenzi, ikiwamo kuwabaka baadhi yao.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa mbali na udhalilishaji huo, wanafunzi hao wamekuwa wakiwatishia maisha walimu wao kwa namna mbalimbali. Katika moja ya vitisho hivyo, wamechoma moto nyumba zao tatu.

Habari hizo zimeeleza kwamba walimu hao wamelazimika kuikimbia shule hiyo baada ya baadhi ya walimu wa kike kutongozwa na wanafunzi, kupigwa mabusu kwa nguvu hadharani, kutishiwa kuchomwa visu na kuchorwa vikatuni vya kudhalilisha.

Mmoja wa walimu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini akihofia kushughulikiwa na wanafunzi hao alisema amelazimika kuikimbia pamoja na walimu wenzake wote, kwa kuwa wameshindwa kudhibiti tabia hiyo kutokana na vijana hao kuungwa mkono na wazazi wao.

Akizungumza kwa simu akiwa Dar es Salaam, mwalimu huyo alisema shule hiyo yenye wanafunzi 485, imepoteza mwelekeo, haitawaliki na mazingira yake hayavutii walimu, hasa wa kike, kuishi na kufanya kazi.

“Tumevumilia vya kutosha, lakini kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya. Walimu wanafikia mahala wanabakwa! Kibaya zaidi wazazi na mamlaka nyingine hazionyeshi ushirikiano kwetu, wazazi wanawa-support (wanawaunga mkono) watoto wao,” alieleza.

Hata hivyo, mwalimu huyo hakuwa tayari kueleza kwa undani kuhusu vitendo hivyo vya ubakaji lakini alieleza kwamba vimekuwa vikitokea walimu hao wanapokuwa katika matembezi usiku.
Vitendo hivyo vimekuwa vikitokea baada ya wanafunzi hao kuwatongoza walimu wao na kukataa kufanya nao mapenzi.

Mwalimu huyo alidai kuwa walimu: http://www.mwananchi.co.tz/

Yatima Wa Kituo cha Amani 'Wanapofuzu'!!

 Bi Erica Mwakalebela, Meneja wa Kituo cha Amani kinacholea watoto yatima wilayani Kilolo, akitoa nasaha zake leo mchana wakati akiwaaga baadhi ya vijana waliolelewa kituoni hapo, kusomeshwa na kuwakabidhi vifaa mbalimbali kulingana na taaluma zao.
 'Bonge la Mtu' Maregesi Gerson, ambaye leo hii amepewa 'ujiko' wa kuwa mgeni rasmi na kukabidhi zawadi mbalimbali kwa yatima wa Kituo cha Amani, wilayani Kilolo. Hapa alikuwa akitoa nasaha zake.
                   Zawadi mbalimbali ambazo vijana hao walikabidhiwa jana ili kwenda kuanzia ujasiriamali.
Walikwenda wadogo, sasa wamekuwa vijana. Kutoka Kushoto ni Claudia Mbugi (17), Waziri Kivamba (19) na Yusta Msangi (16) wakiwa na bahasha zao zenye vitita vya Shs 100,000 kila mmoja ili ziwasaidie wakaanze maisha.

Tiririka na habari kamili...www.kwanzajamii.com/?p=4574

Taarifa Kwa Umma: Usafiri Wa Tren Jijini Dar es Salaam

 Baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuandika tarehe 3 Desemba 2012 kauli yangu kuwa usafiri wa treni katika jiji la Dar es salaam kwamba kwa sasa unaingiza hasara ya wastani wa shilingi milioni 10 kwa siku tano, wanahabari mbalimbali kupitia simu na baadhi ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii wametaka nitoe ufafanuzi kuhusu madai hayo.

Ieleweke kwamba nilitoa kauli hiyo wakati nikijibu swali la mwananchi kwenye mkutano wa hadhara tarehe 1 Desemba 2012 katika mtaa wa Saranga Jimboni Ubungo ambaye alihoji kuhusu ufanisi wa usafiri wa treni jijini Dar es salaam na hatua nyingine ambazo Serikali inapaswa kuchukua kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es salaam; hivyo katika hotuba yangu nilizungumza masuala mengi na kueleza mapendekezo niliyotoa kwa nyakati mbalimbali ya kuboresha mfumo mzima wa usafiri.

Nilieleza kwamba naunga mkono usafiri wa treni kuwepo jijini Dar es salaam na kwamba katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ilikuwa ni moja ya masuala niliyoahidi wananchi kwamba nitayafuatilia, na wakati huo wa kampeni wapo walionipinga ikiwemo kwa kuzungumza katika mikutano yao ya kampeni na hata katika radio.
Kazi ya mbunge ni kuwawakilisha wananchi katika kuishauri, kuisimamia serikali na kutunga sheria hivyo kwa msingi huo mara baada ya kuchaguliwa nilihoji bungeni kutaka hatua za haraka za kuanzishwa kwa usafiri huo na hatimaye Wizara ya Uchukuzi (wakati huo ikiwa chini ya Waziri Omar Nundu) mwaka 2011 ikajibu kuwa itatumia sehemu ya fedha kwenye bajeti kuanza matengenezo kwa ajili ya usafiri huo kuanza.

Kwa hiyo nilisisitiza kwenye mkutano wa hadhara usafiri huu kuanza mwaka huu 2012 ni matokeo ya kazi ambayo ilishaanza mwaka 2011, na nikawaeleza wananchi kwamba natambua mchango wa Waziri wa sasa Dk. Harrison Mwakyembe katika kuongeza msukumo; hata hivyo niliwaeleza wananchi kwamba kama mbunge bado siridhiki na maandalizi yaliyofanyika na kwamba iwapo mapendekezo yangezingatiwa kwa wakati usafiri huo ungekuwa na mfumo na utaratibu bora kuliko ilivyo sasa.

DNA Yabaini Watoto Wengi Wa Kusingiziwa


ASILIMIA 44 ya wapenzi wanaokwenda Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali kupima vinasaba (DNA), kwa ajili ya kujua uhalali wa watoto kwa baba, wamethibitishiwa kuwa watoto hao si wa kwao.

Takwimu za mwaka 2012 kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, zimeainisha kuwa kati ya watu 90 waliokwenda kupima DNA, 40 ambao ni sawa na asilimia 44, wameonekana kubambikiziwa watoto.
Takwimu hizo za kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, zilionyesha kuwa katika kesi 50 za waliokwenda kupima, matokeo yalionyesha kuwa ni wazazi halisi wa watoto wao.

Hata hivyo, idadi hiyo inayoonyesha kuwa kinababa siyo wazazi halisi wa watoto, imeshuka ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2008/2009 ambazo zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya watu waliochukua vipimo hivyo wamebainika kuwa si wazazi halisi wa watoto hao.

Soma....  www.kwanzajamii.com/?p=4547

Magazeti ya leo Alhamisi ya 6th December 2012

Cheki Matokeo ya Mechi za UEFA Dec 5th 2012