Monday, May 6, 2013

Rais Jakaya Kikwete Atuma Rambirambi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha.  Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa.  Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake. 

Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikalina vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili.  Tutawasaka popote walipo na kupambana nao bila huruma.  Aidha, tutakabiliana na aina yoyote ya uhalifu nchini iwe ni ugaidi au aina yoyote ya uhalifu wa namna hiyo au wa namna nyingine, uwe na chimbuko lake ndani ya nchi ama nje ya nchi yetu. Kamwe hatutakubali kuwaacha wavuruge amani na usalama wa Tanzania na watu wake. Rais anaamini kuwa Serikali, kwa msaada na ushirikiano wa wananchi, watu hao watapatikana na kuadabishwa ipasavyo.

Aidha, Rais Kikwete anatoa rambirambi za dhati ya moyo wake kwa wafiwa na wale wote ambao wamejeruhiwa katika tukio hilo. Anaungana nao katika machungu na msiba. Rais pia anawaombea wote walioumia katika tukio hili wapate nafuu ya haraka na waendelee na shughuli zao za ujenzi wa taifa.

Rais Kikwete vilevile anatoa pole nyingi kwa viongozi na waumini wa Kanisa Katoliki kwa tukio hili la kusikitisha na kuvurugika kwa ibada na shughuliyao muhimu ya uzinduzi wa Kanisa lao.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

IKULU,

DAR ES SALAAM

 5 Mei, 2013

DKt. BILAL AWAFARIJI MAJERUHI WA BOMU, ARUSHA

                 Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akiwafariji majeruhi wa mlipuko huo.
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal akiwafariji majeruhiwa milipuko ya bomu jijini Arusha, kulia ni Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania, Dkt. Alex Malasusa na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Assah Mwambene
 Makamu wa Rais Dkt. Bilal akimsikiliza Askofu mkuu wa Kanisa la KKKT Tanzania Askofu Dkt. Alex Malasusa
                                                        Majeruhi wa mlipuko huo wakihangaika
Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilal Pamoja na Mh.Stephen Masele pichani chini na chini wakiwapa pole majeruhi wa mlipuko wa bomu uliotokea majira ya saa 4;35 asubuhi kwenye uzinduzi wa kanisa la St.Joseph Mfanyakazi maeneo ya Olasiti jijini Arusha

Magazeti ya leo Jumatatu ya 6th May 2013



JANUARY MAKAMBA NAYE AWAPONDA CLOUDS FM KWA VITISHO VYAO VYA KUGOMA KUPIGA "BONGO FLEVA " LEO

Huenda mjadala kuhusu uamuzi wa kituo cha radio cha Clouds FM, leo kutopiga Bongo Flava siku nzima haujalikuna sikio la naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba.

Kupitia Twitter, Makamba ameandika kuwa Tanzania ina matatizo matatizo mengi ya kujadili kuliko nyimbo za kuchagua kucheza redioni. “We’ve got much bigger problems than radio playlists, ” ametweet.

Katika mahojiano maalum leo kwenye kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM, mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba alidai kuwa ametoa amri leo kituo chake kisicheze Bongo Flava.

Uamuzi huo leo umekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

RAIS KIKWETE AKATIZA ZIARA YAKE NCHINI KUWAIT.....ANARUDI NCHINI KUJUMUIKA NA WAHANGA WA BOMU LA JANA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatatu, Mei 6, 2013, ameamua kukatiza ziara yake ya Kiserikali nchini Kuwait ili kurejea nyumbani kutokana na tukio la shambulio la kigaidi la mlipuko mjini Arusha ambako watu wawili wamefariki na 60 wamejeruhiwa.

Rais Kikwete alikuwa aondoke kesho kurejea nyumbani, amekatiza ziara hiyo na anaondoka Kuwait City kurejea nyumbani mara moja ili kuwa karibu na wafiwa pamoja na wale waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.

Miongoni mwa shughuli ambazo hazitafanyika sasa kutokana na uamuzi huo wa Rais ni ziara ya kutembelea Kampuni ya Mafuta ya Kuwait katika eneo la Ahmadi mjini Kuwait.

Aidha, Rais hatahudhuria dhifa ya chakula cha jioni ambacho alikuwa anaandaliwa na Waziri Mkuu wa Kuwait, Mheshimiwa Sheikh Jaber Al Mubarak Al Hamad Al Sabah.

CLOUDS WAMJIBU LADY JAYDEE....WAMEDAI KUWA AACHE KUTAPATAPA NA BADALA YAKE AKAZE BUTI

Baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, hatimaye mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba ameamua kujibu shutuma za Lady Jaydee dhidi yake. Ruge amekitumia kipindi cha Power Break Fast cha Clouds FM, kujibu rasmi shutuma hizo.

Amesema anasikitishwa na jinsi Jaydee anavyoendesha harakati zake na kudai kuwa anapigana kwenye vita isiyo sahihi.

“Jaydee akaze buti, anapigana na wrong war, vita yake ameidirect tofauti na mizinga yake, bunduki zake amezielekeza kusiko. Skylight Band inamsumbua, akubaliane na ukweli kwamba Skylight ndio iliyoisababishia Nyumbani Lounge kushuka ilivyoshuka, sio Lady Jaydee kama msanii.

Vita yake na bunduki zake azielekezee Skylight Band. Hajazungumza hata mara moja kwamba ndio kitu kinachosumbua. Mimi naamini kabisa akifanya hiyo kazi, Jaydee bado ni msanii mzuri, ana nguvu, afanye kazi kubwa ya kuweza kurudisha mapambano yake kisanii, kufanya kazi na aangalie tatizo lililotokea Nyumbani Lounge labda anaweza akatatua matatizo lakini sio kushambulia watu kwenye mitandao,” amesema Ruge.

MWANAMKE AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MAJAMBAZI JIJINI DAR

Majambazi yamempora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi na kutokomea kusikojulikana....
Tukio hilo limetokea leo saa 5:16 jioni  na inavyosemekana  ni  kuwa mwanamke  huyo  alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia..
Alipotoka ,majambazi  hayo  yalimfuata na kuligonga gari lake makusudi   na ndipo dada huyo aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa. ..

MAAGIZO ALIYOYATOA RAIS KIKWETE KUHUSU SHAMBULIO LA KIGAIDI LILILOFANYIKA HUKO ARUSHA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya tukio la leo, Jumapili, Mei 5, 2013 la mlipuko kwenye Kanisa Katoliki la Mt. Joseph Mfanyakazi la Olasiti Jijini Arusha.  Tukio hilo la kigaidi limesababisha mtu mmoja kupoteza maisha na wengine 40 kujeruhiwa. 

Rais Kikwete analaani vikali shambulio hilo lililofanywa na mtu au watu katili, waovu na wenye dhamira mbaya na nia mbaya kwa Tanzania na watu wake.

Rais Kikwete ameagiza vyombo vya usalama nchini kumsaka mtu au watu waliohusika na kitendo hicho kiovu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.  Vile vile Rais Kikwete amewataka wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali na vyombo vyake inaendelea kufuatilia tukio hili. 

RPC- ARUSHA ATHIBITISHA KUWA KILICHOLIPUA KANISA NI BOMU....WATU 3 WANAHALI MBAYA, 50 WAMEJERUHIWA

Mkuu wa Mkoa Mulongo naye  amefika  eneo  la  tukio  na  kuwafariji  wahanga  wa  tukio  la  bomu....

RPC  wa  mkoa  wa  Arusha  naye  aliambatana  na  mkuu  wa  mkoa  na  muda  huu  alikuwa  anatoa  nasaha  zake  kwa  wananchi....

RPC  ameeleza  kuwa  tukio  hili  ni  la kigaidi. Katika  maelezo  yake, RPC amesema kuwa  aliyehusika alijitokeza nyuma ya jengo kwa kujificha na kurusha bomu. ...

Amesema Polisi wanawasaka waliohusika  na  unyama  huu  na  ameomba yeyote  mwenye taarifa yoyote aisaide polisi. ..

Waliojeruhiwa ni 50 .Hao wana majeraha ya kawaida  na 3 wako  mahututi

Mpaka sasa  mtu mmoja anashikiliwa  na  polisi kwa mahojiano  zaidi

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA MLIPUKO WA BOMU KATIKA KANISA KATOLIKI HUKO ARUSHA

 Hali ilivyo kanisani hapo baada ya tukio