Friday, July 20, 2012

UZINDUZI WA KAMPENI YA UJENZI WA MABWENI YA WANAFUNZI WA KIKE KWA SHULE ZA SEKONDARI.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia  na Watoto Mh.Ummy Mwalimu (MB) akicheza ‘kwaito” na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kibaigwa katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wa kike kwa shule za sekondari.
Mbunge wa viti maalumu kupitia CHADEMA Mh. Susan Lyimo(MB) akiongea katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya uchangiaji  ujenzi wa wa mabweni- Kibaigwa  Katika hafla hiyo jumla ya shilingi 37,214,000/= zilipatikana ikiwa ni ahadi na fedha taslim.
Dk. Naomi Katunzi  Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) akimkabidhi, Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto  Mh. Ummy Mwalimu (MB) mkasi kwa ajili ya kuzindua rasmi harambee ya ujenzi wa mabweni  wanafunzi wasichana  wa shule za sekondari nchini.
Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Kibaigwa Mh Job Ndugai  (MB) Akivuta utepe uliokatwa na mgeni rasmi Mh. Ummy Mwalimu huku tukio hilo likishangiliwa na wananchi wa  Kibaigwa.
Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Sylvia Lupembe Gunze (kushoto) akijadiliana na Diwani wa Kibaigwa  Mh.Richard Kapinye na Afisa Elimu Taaluma  Wilaya ya Kongwa BiBI Emilia Litunguru.
Mjumbe wa Bodi ya soko la Kibaigwa, Bibi Asha Rajab akitoa ahadi ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya shule ya Sekondari Kibaigwa. Bodi iliahidi kuchangia shilingi milioni 6 katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuchangia ujenzi wa Mabweni inayoendeshwa na TEA.
 Mgeni Rasmi Mh. Ummy Mwalimu (MB) akitoa mchango wake na akihimiza watu wengine wachangie katika Kampeni ya ujenzi wa Mambweni.
Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa Mh.Job Ndugai (MB) akiongea na wananchi wa jimbo lake pamoja na wageni mbalimbali waliohudhulia uzinduzi wa kampeni ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi wasichana. Shule ya Sekondari Kibaigwa itafaidika na mpango huo.

Hongera Teresea Na Glory kwa kupata Sakramenti ya Pili (Kumonyo)

Hakika ni atua nyingine katika maisha hasa ya kiroho mungu awape hekima na maarifa kiakili, kimwili na kiroho nitawalea ipasanyo kama mama mlezi.nawapenda sana.
                                                 Wakaka na Dada zao wakipozi
Mama mzazi akiwa na wazimamizi wa wanae big up sana my sister umekuza madinti.
                                                 Mabrother
Wageni wakiwa nyumbani wakiwasubiri mabibi harusi wetu. namuona mama yangu mzazi na dada yangu mkubwa, wifi langu mama mwalimu na marafiki zangu wakibadilishana mawili matatu watu raha bwana kukutana.
Sherehe imekwisha jamani asanteni mashostito mmenitia joto mungu awabariki sana

UAMUZI KUHUSU SUALA LA MCHEZAJI KEVIN YONDANI

mchezaji Kevin Yondani ni la kiutendaji, hivyo uamuzi wa Sekretarieti ya TFF kuwasiliana na Klabu ya Simba kwa suala hilo la kiutendaji  kama Sekretarieti  ilivyofanya katika barua yake ya Julai 14 mwaka huu ulikuwa sahihi.

2.   Kamati ilibaini kuwa Mkataba wa mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya Simba ulimalizika Mei 31 mwaka huu. Hivyo kwa taratibu za usajili mchezaji Kevin Yondani kuanzia Juni 1 mwaka huu alikuwa ni mchezaji huru.

3.   Aidha Kamati ilibaini kuwa Mkataba uliowasilishwa na Klabu ya Simba TFF ukiwa na maana ya kuongeza mkataba uliokuwepo TFF baina ya mchezaji Kevin Yondani na Klabu ya Simba uliwasilishwa TFF, Juni 7 mwaka huu ambapo ni kinyume cha utaratibu wa kuongeza mikataba ya wachezaji unaozitaka klabu kuwasilisha mikataba ya kuongeza muda wa mikataba ya wachezaji wao wakati mkataba halisi haujaisha muda wake. Hivyo mkataba huo kwa jicho la kisheria haupo.

4.   Hata kama kamati ingeuona mkataba huo katika jicho la sheria, bado mkataba huo una tatizo la kisheria hasa katika tarehe ambazo pande mbili husika ziliingia makubaliano hayo. Ukiuangalia mkataba huo unabainisha kuwa, wakati mchezaji Kevin Yondani aliingia makubaliano Desemba 23 mwaka jana, upande wa pili wa kimkataba ambao ni Klabu ya Simba inaonekana iliingia makubaliano hayo kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wake Geofrey Nyange Kaburu, Desemba 23 mwaka huu.

5.   Kisheria utata huu unaweza kuondolewa na pande husika tu kwa kurekebisha dosari hiyo kwa maridhiano kuweka saini katika mabadiliko hayo ili kuthibitisha mabadiliko hayo. Hivyo katika jicho la kisheria mkataba huo hauwezi kutumika kumzuia mchezaji huyo kwenda katika klabu anayoipenda wakati akiwa huru.

Kutokana na maelezo yote hapo juu, Kamati imeridhia hatua iliyochukuliwa na Sekretarieti ya TFF ya kumruhusu mchezaji Kevin Yondani kuichezea timu ya Yanga katika mashindano ya Kombe la Kagame 2012.

Alex Mgongolwa
Mwenyekiti
Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Rais Kikwete Na Mama Salma Kikwete Watua Zanzibar Kutoa Rambirambi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza Bw.  Kitwana Makame Haji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali ya meli waliolazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja mjini Unguja Jana Jioni.
Rais Jakaya Kikwete akimpa pole Bi Salome Abeli, mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission jijini Arusha, aliyekuwa njiani kuelekea Pemba kikazi kabla ya kupatwa na ajali hiyo ya meli. Amesema hali yake inaendelea vyema hapo katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita mbele ya miili ya waliokufa katika ajali hiyo ya meli jana karibu na kisiwa cha Chumbe. Hapa ni uwanja wa Maisara ambako miili huletwa kwa kutambuliwa.

Magazeti ya Leo Ijumaa 20th July 2012


Mnyika Kuwa Shahidi Kesi Ya Mauaji

MBUNGE wa jimbo la Ubungo, John Mnyika atakuwa ni mmoja wa mashahidi wa Serikali watakaoithibitishia mahakama namna walivyohusika washtakiwa wanaotuhumiwa kumuua Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Ndago, Yohana Mpinga (30).

Jeshi la Polisi mkoani Singida, limemefikia azimio hilo baada ya kumhoji Mnyika kwa saa tatu juzi usiku, kuhusiana na tukio hilo la mauaji lililotokea baada ya mkutano wake wa hadhara uliofanyika Julai 14 mwaka huu, majira ya jioni.

Mahojiano hayo yaliyoanza saa 11.53 jioni na kumalizika saa 3:15 usiku, yaliendeshwa chini ya kikosi maalum cha askari wa upelelezi kutoka jijini Dar es Salaam kwenye ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani hapa.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zilithibitisha kwamba Jeshi la Polisi lilimtaka Mnyika awe tayari kuitwa wakati wowote ili kusaidia kwenye kesi hiyo ya mauaji.

Tayari watu 18 wametiwa mbaroni, miongoni wakiwemo wanachama wa Chadema, kwa tuhuma za kuhusika kwenye mauaji ya kijana huyo wa CCM.


Mnyika alihojiwa huku akiwa na wakili wa Chadema na mbunge wa jimbo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mauaji hayo ya mwenyekiti wa UVCCM yalifanyika Julai 14 mwaka huu saa 10 jioni huko katika kijiji cha Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi.

Mauaji hayo yanadaiwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na vurugu zilizotokea kwenye mkutano wa hadhara ambao Mnyika alikuwa mgeni rasmi.

Katika hatua nyingine, mshauri na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitila Mkumbo, ambaye alikuwa ameambatana na Mnyika, alitarajiwa pia kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo jana.
Chanzo: www.mwananchi.co.tz

HAYA SASA, WALE WALIOTAMANI KUMUONA MTOTO WA BEYONCE TOKA AKUE… NDIO HUYU.

Hizi picha zimepigwa na mtu tu ambae alishtukia Beyounce na mwanae wakifanya shopping mbele yake, akazipiga na kutweet… Blue Ivy kakua.
Hizi ni picha ambazo zilitolewa bure na Beyonce na Jay Z miezi kadhaa iliyopita zikimuonyesha mtoto wao ambae wengi tulidhani wangeuza kwa mamilioni ya dola picha za mtoto wao kama walivyofanya mastaa wengine ikiwemo J.Lo!

Ni miezi kadhaa toka mara ya mwisho dunia ilipomuona Blue Ivy kwa uwazi kiasi hiki.

HUU NDIO MKOPO CHINA ILIOTOA KWA AFRIKA.

Rais wa China Hu Jintao ametangaza mkopo wa dola Bilioni 20 kwa nchi za bara la Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya nchi hiyo na Afrika.

Mkopo huo ni mara mbili zaidi ya kiasi ambacho China iliahidi kwa kipindi cha miaka mitatu 2009.

DW wamesema ahadi hiyo inaonekana kuimarisha uhusiano mzuri wa China na bara la Afrika, ambalo ni muuzaji wa mafuta na mali ghafi kama vile shaba na uranium kwa nchi hiyo yenye idadi kubwa zaidi ya watu ulimwenguni na ya pili kwa ukubwa kiuchumi.

Lakini mikopo hiyo huenda isiwe habari njema kwa nchi za magharibi ambazo zinaishutumu China kwa kupuuza uiukwaji wa haki za binaadamu katika ushirikiano wake wa kibiashara na Afrika, hasa katika tamaa ya China ya kuulisha uchumi wenye njaa ya raslimali na unaozidi kukua.

President Hu alipuuzia hofu kama hiyo katika hotuba yake kwa wananchi Great Hall, mkutano uliohudhuriwa na viongozi akiwemo rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na mwenzake wa Guinea ya Ikweta Teodoro Obiang Nguema, mtu anayeshutumiwa vikali na makundi ya haki za binaadamu kama mmoja wa viongozi mafisadi zaidi ulimwenguni.

TAARIFA MPYA KUHUSU AJALI YA MV SKAGIT ZANZIBAR, IDADI YA VIFO IMEONGEZEKA.

Kwa mujibu wa TBC1 katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku leo July 19 2012, mpaka sasa idadi ya waliopoteza maisha kwenye ajali ya MV SKAGIT ni 68 ambapo baadhi ya maiti tayari zimetambuliwa na tayari majeruhi zaidi ya 100 walikua wamefikishwa hospitali huku watu ambao hawajaonekana wakiwa ni 91.

Mpaka jana usiku kwenye taarifa ya habari saa mbili usiku, ni watu saba pekee walioripotiwa kupoteza maisha kwenye ajali hiyo.
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano na Serikali ya Zanzibar zimetangaza siku tatu za maombolezo kuanzia July 19 2012 ambapo kituo cha mawasiliano kwa ndugu wanaohitaji kujua habari za ndugu zao waliopata ajali kwa upande wa bara ni ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es salaam.

Kutoka bungeni ni kwamba wabunge wamekubaliana posho za leo (July19) hawatazipokea na badala yake zitapelekwa kama rambirambi kwenye ajali.

Spika wa bunge Anne Makinda ambae aliahirisha kikao cha bunge leo mpaka kesho amesema “tulikua tunaamini kwamba kutakua na mazishi ya halaiki lakini Serikali ya Mapinduzi imesema hapana mpaka sasa”

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini SUMATRA imesema cheti cha ubora cha meli hiyo kilianza tarehe 24 August 2011 na muda wake unaisha tarehe 23 2012 ambapo imefahamika kwamba meli hiyo ilisajiliwa na Mamlaka ya usafiri wa baharini Zanzibar (ZMA) na ilikua imepitishwa kubeba abiria 300 na mizigo isiyozidi tani 26 ambapo Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi  amesema meli ilikua imebeba watu 290, watu wazima ni 250, watoto ni 31 na wafanyakazi 9 wa meli.