Monday, October 1, 2012

CHADEMA Yazidi Kuitafuna Familia Ya Wasira

Baada ya kamanda Makongoro Wasira kujiunga na M4C siku chache zilizopita, leo tena watoto wengine wa Wasira wamejiunga na M4C na kukitupia virago Chama cha Baba yao CCM. Waliojiunga leo katika Makao makuu ya Chadema na kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Slaa ni kamanda Ester Wasira na Lilian Wasira.

 Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa kadi walikuwa na haya ya kusema:Ester wasira: (Ni mwanasheria, graduate wa UDSM) (i) Chadema ni Chama cha kizalendo na mkombozi wa dhati wa Mtanzania. (ii) Chadema kinaleta matumaini mapya kwa Watanzania hasa vijana wasio na kazi na matumaini, Watanzania wenye maisha magumu hata kushindwa kumudu milo miwili kwa siku, akina mama

wanaohangaika vijijini bila matibabu ya uhakika, maji, umeme, nyumba bora nk (iii) CCM imedumaza nchi, nchi imekuwa kama mtu aliyedumaa kwa kukosa protein, haikui tena, Chadema ni damu mpya yenye kuweza kuingiza protein kwenye mishipa ya nchi iweze kufufuka na kukua tena. (iv) Chadema kina viongozi imara na kwa maneno na matendo yake wanawadhihirishia watanzania kuwa ni waadilifu na wana nia njema ya kuipeleka Tanzania mbele.

Alimalizia kwa kuwaasa vijana, akina mama na wazee wajiunge na M4C ili kuijenga Tanzania mpya. Alimalizia kwa kusema, “Kwa msaada wa Mungu, Tanzania Mpya inakuja. Lilian Wasira (Mwanasheria, graduate wa TUDARCO): (i) Alielezea furaha yake kwa kujiunga na Chama makini na chenye kuleta matumaini mapya kwa mtanzania (ii) Aliwaasa vijana, akina mama na wazee wajiandikishe kwa wingi nafasi itakapotokea na 2015 wakamalizie kazi ya ukombozi kwa kuipigia Chadema kura (iii) Amewaasa Watanzania kuacha kulalamikia maovu ya CCM na kuchukua hatua ya kuiweka CCM pembeni na kuleta Chadema kama chama mbadala.

Alisema hakuna sababu ya kuwa na mfumo wa vyama vingi kama watanzania hawathubutu kuchagua chama mbadala na badala yake kuendelea kuichagua CCM na kulalamika kila siku kuwa CCM imeshindwa kuongoza nchi (iv) Kwamba CCM imekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 50 hivyo ni wakati sasa wa kuiweka pembeni na kuingiza chama kipya, mawazo mapya na kujenga mfumo mpya wa uongozi. Hakuna kitu CCM imeshindwa kufanya kwa miaka 50 inaweza kufanya kwa miaka 5 au 10 ijayo. (v) Anasema ana imani na sera za chadema kuwa ndizo zitatukomboa.

Amewapa moyo viongozi wa Chadema wasitishwe na vitisho na mauaji yanayofanywa na dola na kusema yupo tayari kwa M4C na yupo tayari kulipuliwa kama walivyolipuliwa wanachadema wengine na kuuawa kama itambidi afanye hivyo. (vi) Kwamba Chadema ni Chama kinachosubiri kuingia Ikulu isipokuwa tu watu wajiandikishe, wapige kura na walinde kura. (vii) Nae alimalizia kwa kusema “Kwa msaada wa Mungu Tanzania mpya inakuja.”Dr Slaa alitiwa moyo sana na ujasiri ulioonyeshwa na vijana hawa pamoja na maneno ya kizalendo waliyoongea na akawakarisha kwenye uwanja wa mapambano ya M4C.

Yaliyojiri Magazetini leo Jumatatu 1st October 2012