Monday, January 21, 2013

RAIS KIKWETE AWASILI UFARANSA

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwa na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.
Mama Salma Kikwete akiongea na mke wa Rais wa Mali Mama Touré Lobbo Traoré waliyekutana naye uwanja wa ndege wa Kimataifa Charles de Gaulle jijini Paris, Ufaransa, baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kiserikali ya siku tatu.

Maafa stendi ya ubungo








SEHEMU ya ukuta wa kituo cha mabasi ya kwenda mikoani cha Ubungo, jijini Dar es Salaam, leo alfajiri umeanguka na kuyaharibu vibaya magari zaidi ya ishirini yaliyokuwa yameegeshwa nje ya eneo hilo. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Charles Kenyela alisema kuwa idadi ya magari yaliyopatwa na ajali hiyo yanakadiriwa kufikia 24 ambapo watu watatu wanasemekana wamejeruhiwa.

Magazeti ya leo Jumatatu ya 21st January 2013

Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kumtimuwa uwanachamaMwamalala ajiunga nccr mageuzi

Edo Mwamalala, hatimaye mwanachama huyo ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mageuzi ya Taifa (NCCR- Mageuzi).

Mwamalala, alisema harakati za kisiasa alizianza tangu akiwa kijana, kuwa muumini wa siasa za upinzani na rasmi alijiunga na Chadema.

Alisema ameamua kujiunga na Chama hicho kutokana na ukweli kwamba ndicho chama kinachoonekana kuwa chama chenye utu, misingi bora ya usawa, uheshimu wa haki za wanachama na Watanzania pamoja na mshikamano.

“Kwa furaha kubwa kabisa na penda kuchukua fursa hii kuwatangazia Wanambeya na umma wa Watanzania kwa kuvunja ukimya na sasa natangaza kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi na nisema kuwa huu ni mwanzo tu mimi nimetangulia na wengine watakuja au kufuata hatua kwa hatua”alisema Mwamalala.

Hata hivyo, Mwamalala alipinga kuwa alifukuzwa chama bali kilichotokea ni kwamba mwanzoni mwa Januari 3 mwaka huu alitangaza kujiuzulu nafasi zote za uongozi ndani ya Chadema ikiwa ni pamoja na kujivua uanachama wa chama hicho.

Pamoja na kudai kuwa hajafukuzwa, taarifa za Chama hicho zinaeleza kuwa Mwamalala alifukuzwa uwanachama tangu mwaka jana.

MTWARA : SERIKALI INAVUNJA NCHI KWA KUTOSIKILIZA WANANCHI

Mbunge wa Kigoma Kaskazini(CHADEMA)na Mwenyekiti wa kamati ya Bunge Ya Mashirika ya Umma Mheshimiwa Zitto Kabwe

Kwa wiki ya tatu mfululizo kumekuwa na malumbano kuhusiana na suala la ujenzi wa Bomba la gesi kutoka Mtwara mpaka Dar es Salaam. Kumekuwa na madai yenye nguvu ya hoja kutoka kwa wananchi wa Mtwara dhidi ya porojo kutoka kwa viongozi wenye dhamana ya kujibu madai haya ya watu wa Mtwara. Watu wa Mtwara kwa umoja wao na kwa kuungwa mkono na viongozi wa dini zote wamekuwa wakitaka Serikali ifikirie upya suala la mradi wa ujenzi wa Bomba la gesi na badala yake kujenga mitambo ya kufua umeme mkoani Mtwara na kusafirisha umeme huo kwenda maeneo mengine ya nchi. Kwenye moja ya maandishi yangu (Serikali iwasikilize watu wa Mtwara) nimeshauri kuwa Taifa liwe na gridi nyingine ya Taifa ambayo itatokana na Gesi tu na ianzie Mtwara.

MABAO 3 DHIDI YA MABAO 2 NDIYO YALIIPA YANGA USHINDI

Wachezaji wa Young Africans wakisalimiana na wachezaji wa Black Leopard kabla ya kuanza kwa mchezo

Mabingwa wa kombe la Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati almaarufu kombe la Kagame, timu ya Young Africans Sports Club imeifunga timu ya Black Leopard ya Afrika Kusini mabao 3-2 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo jioni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaaam.

Young Africans iliyokuwa nje ya nchi kwa kambi ya mafunzo takribani wiki ilikuwa ikicheza mbele ya washabiki wake, iliweza kucheza soka safi na la kuvutia kipindi chote cha mchezo huku Black Leopard ikipata wakati mgumu kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Didider Kavumbagu alikosa bao la wazi dakika ya 21 ya mchezo akiwa yeye na mlinda mlango wa Black Leopard Ayanda Mtshali, lakini shuti alilopiga lilipaa juu ya lango la timu hiyo.