Friday, October 5, 2012

Sekeseke za Mgambo wa jiji la Arusha leo na Wafanyabiashara










Katika hekaheka za safisha jiji leo arusha bado Manispal ya mjini hapa wakiendelea kuwaondoa wale wote wanaofanya biashara maeneo ya barabarani, leo nilikutana nao wakiwa wanaviondoa vibanda hivyo kwa wale waliokaidi agizo hilo.

Ni kweli jiji linakuwa safi lakini je hawa watu wanakwenda wapi? je kuondoa uwanja wa NMC waliouteuwa kuwa soko kuna eneo lingine lililoteuliwa kwa ajili yao? NMC hauna huwezo wa kuwaweka wafanyabiasha hawa je serikali wanaliona hii kama tatizo la Taifa?au hadi pochi zetu ziishe kwa kuchukuliwa na vibaka ndio wajue chazo?

Pamoja na yote tunahitaji jiji liwe safi.Basi tunawataka manispal wawe wabunifu wawatafutie mahali ambapo wataweza kujibatia riziki angalae waweze kuendesha familia zao.Je serikali inajua kuwa watoto hawaindi shule, hawapati milo mitatu kwa siku hata matibabu ndio kabisa bado kodi ya nyumba, Je Maisha bora kwa kila Mtanzania Itawezakana??????

Siku Ya Pili Ziara Ya JK Canada

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni mara baada ya kupokelewa katika Bunge la Seneti la Canada. Kulia ni Spika wa Bunge hilo Mhe Noel Kinsella, anayefuatiwa na Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper na Spika wa Bunge la wawakilishi la Canada (House of Commons), Mhe Andrew Scheer pamoja na viongozi wengine wa bunge hilo Alhamisi Oktoba 4, 2012






Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea jezi toka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper katika jengo la Bunge la Seneti la nchi hiyo, Alhamisi Oktoba 4, 2012                                     

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Spika wa Bunge la Seneti la Canada  ramani ya dunia na njia za meli, pamoja na kuoneshwa chemba ya mikutano ya Maseneta wa Bunge la Canada  Alhamisi Oktoba 4, 2012                                        Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Canada Mhe Stephen Harper wakitembea kuelekea kwenye chumba cha mkutano kuongea na wanahabari. Zuria jekundu na bendera za Canada za kiongozi wa  nchi husika huwekwa sehemu hiyo kwa heshima na wakati wa ziara ya kiongozi wa nchi ya nje aliye katika ziara rasmi nchini humo.

Picha na IKULU

Ukiamua, hata kwa kubeba zege unaweza kufanikiwa!

WAKATI nasoma sekondari nilitamani sana kufanya kazi ya uandishi licha ya kwamba pia niliamini biashara ingeweza kunifanya nikafika pale ambapo nilitamani kuwepo katika maisha yangu. Kutokana na utashi wangu huo nilijikuta nikiamua kuchagua  kuwa mwandishi na wakati huo huo mfanyabiashara huku nikiamini kwamba kazi hizi zitanipatia mafanikio makubwa.

Mafanikio ni mafanikio licha ya kwamba viwango vya kufanikiwa vinatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Kwa mantiki hiyo basi naweza kusema nimefanikiwa kwa kiasi fulani licha ya kwamba nahitaji mafanikio makubwa zaidi.
Labda nikuulize wewe msomaji, ukiulizwa umeamua kuwa nani na kufanya nini katika maisha yako utajibu nini? Naamini kwa swali hilo kila mtu atakuwa na jibu lake. Usishangae ukamsikia mtu akisema ameamua kuwa kahaba na mwingine akakueleza kwamba ameamua kuwa mwizi katika maisha yake.

Lakini pia unaweza kumsikia mtu akisema, ameamua kuwa daktari ama mfanyabiashara katika maisha yake. Kimsingi kila mtu ana chaguo lake. Unachotakiwa kujiuliza ni kwamba je kwa kuwa mwizi au kahaba unaweza kuwa na mafanikio ya kudumu katika maisha yako? Hilo ndilo swali la msingi.

Wakati mwingine inakuwa ni rahisi sana kwa mtu aliyeamua kufanya kazi ya kubeba zege ama kuzibua mtaro kufanikiwa katika maisha yake kuliko yule ambaye hajaamua afanye nini, yaani yupoyupo tu. Hawa ni wale wanaoishi kibubusa ilimradi tu siku zinakwenda.

Ninavyoona ni kwamba, karne hii si ya kuishi kibubusa na kushukuru Mungu kwa kuiona siku nyingine bali unatakiwa kujiuliza baada ya Mungu kukujalia kuiona siku hiyo nyingine utaitumia vipi? Kitu cha msingi ni kujiwekea mikakati madhubuti ya vipi utaendesha maisha yako katika kila siku ya Mungu.

Umefika wakati sasa wa kuamua ufanye nini na uwe nani katika maisha yako la sivyo utabaki kuwa si chochote wala si lolote na mwishowe Mungu ataona hana sababu ya kukubakiza ulimwenguni wakati huna chochote unachokifanya.

Tufahamu kabisa kwamba kama tutashindwa kuamua kuwa nani na kufanya nini hakika tutakuwa hatuna uhakika wa nini tunatafuta katika maisha yetu.

Kimsingi tutakuwa ni watu wa kubahatisha na kufanya kila tutakachoona kinaweza kutuingizia pesa na wakati mwingine kufanya mambo mengine ambayo hayawezi kutupa mafanikio ya kudumu na furaha ya kweli katika maisha.

Hebu anza kujiuliza leo hii bila kujali elimu uliyonayo, jinsi wala umri wako kwamba ni kitu gani ambacho ukikifanya utafurahi na kuona kwamba umetimiza lengo lako la kuletwa hapa ulimwenguni na hatimaye kupata mafanikio?

Katika maisha ukijaribu kuchunguza kwa makini utakuta wengi waliofanikiwa ni wale waliochagua mafanikio. Waliamua kufa na kupona kuhakikisha kwamba wanafika pale ambapo walitaka kufika kwa kufanya kazi mbalimbali.

Hii inadhibitisha kwamba katika maisha kila kitu ni uamuzi na ndiyo maana nadiriki kusema wale ambao wana nguvu za kutosha na afya njema lakini ni maskini, naamini wameamua kuwa maskini katika maisha yao. Watu hao wakiamua kuwa matajiri pia wanaweza.
Kwa kumalizia niseme tu kwamba hakuna hata mmoja wetu ambaye ameletwa hapa ulimwenguni ili awe si lolote wala si chochote. kila mtu ana nafasi yake ambayo akiitumia vizuri ana uwezo wa kuwa na maisha bora na yenye furaha.

Unachotakiwa kufanya ni kuamua ufanye nini katika maisha yako ili uweze kupata mafanikio.

WALIMU WAGOMEA SIKU YAO

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) kimegoma kushiriki maadhimisho ya Siku ya Walimu Duniani inayoadhimishwa leo kwa madai kina huzuni na hakina mafanikio yoyote ya kuwaambia walimu.

Aidha, chama hicho kimetoa mwito kwa Serikali kukubali ushauri wa Bunge na uamuzi wa Mahakama, ili warudi katika meza ya majadiliano kwa ajili ya kuendeleza walipoachia.

Katibu wa CWT, Ezekiel Oluoch alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho hayo ambayo kaulimbiu yake ni ‘Kuwatetea walimu’.

“Kesho (leo) ni Siku ya Walimu Duniani, kwa bahati mbaya hatutakuwa na sherehe ama maadhimisho kwani hakuna chochote cha kuelezea … hatuwezi kusherehekea tukiwa na matatizo mengi ambayo hayajafikia suluhu,” alisema Oluoch na kuongeza kuwa wataadhimisha siku yao wakiwa kazini na wamekata tamaa.

Alisema mwajiri wao ambaye ni Serikali hajalipa madai ya wakufunzi wa vyuo vya ualimu, hajashughulikia madai ya walimu ambayo hayajalipwa na kutoajiri walimu waliohitimu ingawa fedha zimetengwa na Bunge.

Alisema katika siku hiyo, CWT inatoa mwito kwa Watanzania na jumuiya za kimataifa kujitokeza kutetea walimu dhidi ya manyanyaso wanayopata kutokana na mishahara duni isiyokidhi mahitaji muhimu ya kila siku.

Pia alitaka walimu kushikamana katika kudai maslahi bora zaidi kama watumishi wengine wa umma na Serikali ilipe madeni yote wanayodai walimu, wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini pamoja na wakaguzi wa shule.

Kuhusu kurudi katika meza ya majadiliano, Rais wa CWT, Gratian Mukoba alidai Serikali imegoma kukutana na chama hicho kama ilivyoagizwa na Mahakama na Bunge.
Alisema pamoja na leo kuwa Siku ya Walimu, Serikali imekataa mapendekezo ya CWT ya kuteua timu ya majadiliano nje ya chombo cha majadiliano ya pamoja kwenye utumishi wa ualimu ili madai ya walimu yashughulikiwe ndani ya mwaka huu wa fedha.

“Hadi sasa Serikali imekiuka amri ya Mahakama ya Kazi ambayo iliagiza pande zote, yaani CWT na Serikali zirudi kwenye meza ya majadiliano… kwa uelewa wetu, meza iliyokuwa inatumika kwa majadiliano kabla ya mgomo ndiyo inayostahili kutumika kuendeleza mazungumzo kati ya pande hizi,” alisema Mukoba.

Alisema CWT inalaani kwa nguvu zote ukaidi huo wa Serikali ambao hauna tija kwa nchi, bali unazidi kuwasababishia walimu kuishi maisha magumu yasiyo na mfano na kudhulumu wanafunzi haki yao ya kupata elimu.

Akijibu hoja ya Serikali kukaidi uamuzi wa Mahakama na Bunge, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani alisema Serikali inapanga tarehe mwafaka ya kukutana na kwamba haijakaidi agizo hilo.
Alisema baada ya CWT kuwaandikia wako katika majadiliano na kwamba wameahidi kukutana ili kuzungumza.

CHANZO: HABARILEO

Magazeti ya leo Ijumaa ya 5th October 2013