Monday, November 12, 2012

Mkutano Mkuu Wa Ccm, Dodoma Leo

                         Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwasili ukumbi wa Kizota akifuatana. Kulia ni Karume, Dk. Bilal na kushoto ni Mukama na Msekwa.                              
                                                                 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiongoza Mkutano Mkuu wa CCM leo Novemba 12. Kushoto ni Karume na kulia ni Msekwa
                    Waasisi wa Tanu na baadaye CCM, Mwadawa Ali (85) na Mohammed Makber (72)
                        wakisoma gazeti ya UHURU la Chama Cha Mapinduzi, kabla ya mkutano kuanza

              Khadija Kopa (kushoto) akiimba wakati TOT ilipotumbuiza kwenye mkutano huo

Picha na Bashir Nkoromo

Chadema Yasambaza Pikipiki Nchi Nzima

 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza mkakati wa Uchaguzi Mkuu 2015 kikiahidi kumwaga pikipiki katika tarafa zote nchini kwa ajili ya kuwafikia wananchi kuelekea uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema hayo jana katika kikao cha viongozi wa chama hicho na wadau wake kilichofanyika hapa.

Mbowe alisema pikipiki hizo zitakuwa na vipaza sauti maalumu zitawasaidia viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

“Tumeanza mkakati wa kuhakikisha tunawafikia wananchi kila mahali. Tunataka kusikiliza matatizo yao, na hata pale ambako kuna shida ya usafiri, kwa pikipiki tutafika,” alisema.

Tayari chama hicho kimezindua kampeni yake ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ambayo lengo lake ni kuwaandaa wananchi kwa uchaguzi ujao.

Mbowe alisema upatikanaji wa pikipiki hizo unatokana na fedha za ruzuku ambazo zinatolewa na Serikali kwa chama hicho  pia marafiki na wanachama wake walioko nje ya nchi.

ngozi wa chama hicho katika ngazi zote kufanya kazi kwa kujituma ili kuhakikisha kinashika dola mwaka 2015.

“Tanzania inahitaji mabadiliko na sisi tukiwa viongozi tunapaswa kujipanga kwanza, kuhakikisha tunaongeza wanachama pia kuzitatua kero za wananchi,” alisema Mbowe.

Katika mkutano huo, Mbowe aliwapongeza viongozi wa Chadema, Wilaya ya Hanang’ kwa kazi kubwa waliyoifanya kiasi cha kupata na madiwani 17 katika halmashauri hiyo.

Awali, Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Manyara, Rose Kamili alisema chama hicho kimejipanga kutwaa Jimbo la Hanang’ katika uchaguzi ujao na Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’.

“Katika miaka hii mitano Chadema, Hanang’ tumekuwa na mafanikio makubwa na hili linatokana na mshikamano mkubwa wa viongozi katika ngazi mbalimbali,” alisema.

Na:  Mussa Juma Hanang’

BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AIPA CHANGAMOTO BODI YA UTALII TANZANIA (TTB)

 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe, wakati alipowasili katika hafla ya chakula cha jioni katika yake, Balozi na maaofisa wa Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na maofisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza ili kuagana na kutathimini mapungufu na mafanikio ya ushiriki wa Tanzania katika maonyesho ya dunia ya utalii World Treavel Market (WTM) yaliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini Uingereza, ambapo zaidi ya makampuni 55 yanayouza na kutangaza utalii wa Tanzania yalishiriki katika maonyesho hayo, maonyesho hayo hufanyika kila mwaka eneo la Excel jijini London.

Balozi Khamis Kagasheki aliitaka Bodi ya Utalii Tanzania kuongeza juhudi zaidi ili kuleta mafanikio zaidi katika maonyesho hayo na menine na kuongeza idadi ya watalii kufiki milioni moja kwa mwaka, Tanzania ikijipanga vizuri na kutangza vivutio vyake zaidi duniani inaweza kupata mafanikio zaidi katika utalii na kuongeza zaidimapato yake ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi kupitia sekta ya utalii.
                                   Maofisa mbalimbali wakiingia katika hafla hiyo ya chakula cha jioni.
 Baadhi ya maofisa waliohudhuria katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Dkt. Wegoro kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha , Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Balozi mdogo wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Kilumanga na Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania ubalozini Bw. Kashangwa.
                       Maofisa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza wakiwa katika hafla hiyo.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki kulia akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maliasili, Utalii na Ardhi wakati alipokuwa kichangia mazungumzo katika hafla ya chakula cha jioni baada ya kumalizika kwa maonyesho ya WTM nchini Uingereza mwishoni mwa wiki iliyopita, katikati ni Balozi wa Tanzania nchini humo Balozi Peter Kallaghe.
 Ofisa Habari wa TANAPA Bw. Shelutete kulia akiwa na Maofisa wa Kituo cha biashari cha Tanzania nchini Uingereza katikati ni Dilunga na kushoto ni Mohamed
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Balozi Peter Kallaghe akizungumza katika hafla hiyo kulia ni Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili na Utalii.
 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki akizungumza katika hafla hiyo ambapo aliwashukuru maofisa kutoka Bodi ya Utalii na Taasisi zake pamoja na makampuni yaliyoshiriki katika maonyesho hayo kwa maandalizi mazuri katika ushiriki huo, lakini pia akaagiza kuangalia changamoto na kuzifanyia kazi ili kuboresha zaidi ushiriki wa Tanzania katika maonyesho yajayo na mengine yanayoweza kufanyika katika nchi zingine, kulia katika picha ni Balozi Peter Kallaghe na kulia ni Mama Balozi

PICHA NA WWW.FULLSHANGWEBLOG.COM

Matokeo Wajumbe 10 Kapu La Kifo

Matokeo ya chaguzi za nafasi 10 za wajumbe wa NEC Tanzania Bara wa Chama cha Mapinduzi zinazoendela Dodoma yametoka ni kama ifuatavyo:

1. Stephen Wassira - 2,135
2. January Makamba – 2,093
3. Mwigulu Nchemba – 1,967
4. Martine Shigela – 1,824
5. William Lukuvi – 1,805
6. Bernard Membe – 1,455
7. Mathayo David Mathayo – 1,414
8. Jackson Msome - 1,207
9. Wilson Mukama - 1,174
10. Fenela Mukangara - 984

Shukurani za taarifa hii: Makongoro Nyerere (via blogu yake ya Muhunda)

Wakati huo huo, blogu ya CCM inaripoti kuwa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kwamba uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara na Makamu Mwenyekiti Zanzibar utafanyika kesho tarehe 13 Novemba 2012.

Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,uliofanyika leo asubuhi Kizota mjini Dodoma, Nape alizungumzia kufanikiwa kwa siku ya jana, baada kila kitu kwenda vizuri kwa mujibu wa ratiba.
Pia alizungumzia ratiba ya leo, ambapo kutakuwa na Taarifa mbali mbali za kazi za chama, Taarifa za utekelezaji za ilani ya uchaguzi (Bara na Zanzibar) itasomwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa upande wa Tanzania Bara na kwa upande wa Zanzibar itasomwa na na Makamu wa Pili Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.

Taarifa kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pia zitasomwa leo.
Akizungumzia mabadiliko ya Katiba, alisema kumekuwa na mafanikio sana baada ya mapendekezo yote kupitwa bila kupingwa, moja ya mapendekezo ni kuwepo kwa Baraza la Ushauri la Wazee, pamoja kubariki mapendekezo wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa watoke wilayani. Baada ya uchaguzi kutakuwa na mrejesho wa mijadala na kutoa maazimio ya Mkutano Mkuu.

Chama Cha Makahaba Chasajiliwa Malawi

                                                                    Rais Banda wa Malawi
ZAIDI ya makahaba 2000 nchini Malawi wameungana kwa ajili ya kupinga manyanyaso wanayoyapata na kuboresha mazingira ya afya, baada ya kuzindua rasmi chama cha kuwatetea juzi.

Kundi hilo linaundwa na vyama visivyo vya kiserikali vya ndani na nje ya nchi hiyo, ikiwa ni la kwanza kutambuliwa rasmi na kupewa usajili katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ambapo biashara ya ukahaba inaharamishwa.

“Muda wa kujadili kwa pamoja matatizo yanayowakabili ndio huu. Mnajua namna Polisi na Mahakama vinavyowabana na kwamba mnahitaji kupata huduma nzuri za kulinda afya zenu na afya ya uzazi bila kipingamizi,” alisema mwanasheria wa haki za binadamu, Chrispin Sibande alipokuwa akizungumza na kundi la wateja wake wapatao 50 ambao ni makahaba.

Makahaba nchini humo mara nyingi wamekuwa wakikamatwa na Polisi hata kwa makosa madogo ikiwemo kukutwa wakiwa wamekaa bila kazi, ambayo pia huambatana na kutozwa faini.

Miaka mitatu iliyopita, makahaba 14 walikamatwa na Polisi na kulazimishw akupimwa Virusi vua Ukimwi (VVU) na wote kukutwa wakiwa wameathirika, ambapo walishtakiwa mahakamani kwa kufanya biashara ya ngono huku wakijua kuwa wana maradhi hayo ya kuambikiza, ambapo walichajiwa Dola7 kila mmoja na kuachiwa huru.

Baadaye waliishtaki Serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia mambo yao binafsi katika kesi ambayo hadi sasa bado inasubiri kusikilizwa katika mahakama kuu.

Wataalamu wa afya nchini humo wanasema maambukizi ya Ukimwi miongoni mwa makahaba hao yanafikia asilimia 70. Mawakili wao wanasema kuw awanatumiani umoja wao utawasaidia pia katika kuwaelimisha kuepuka maambukizi hayo.

Sherehe Za Uhuru Wa Tanzania Marekani

                                            SHEREHE ZA UHURU WASHINGTON STATE
Watanzania wote wa Washington State, mnaalikwa kwenye sherehe za uhuru zitakazofanyika Dec. 8, 2012 (Saturday) kuanzia saa 12 jioni (6:00PM) hadi saa sita usiku (12:00PM).

MAHALI: 411 156th AVE NE Bellevue WA 98007
BURUDANI: DJ Haroub atashusha Disco la kufa mtu. Pia kutakuwa na kikundi cha sanaa kutoka University of Washington kitakachoonyesha onyesho la ngoma za Tanzania.
KIINGILIO: Bureeeeeeeee
CHAKULA : Bureeeeeeee
VINYWAJI: Soda ($1), maji ($1), vinywaji vikali ($2 na kuendelea)

MUHIMU: 1) Tafadhali alika mtu yeyote. Hizi sherehe ni za Watanzania wote (wanachama na wasio wanachama), alika marafiki pia (2) Wahi ili usikose chakula (3) Kutakuwa na vitu vya Kitanzania vitakavyouzwa ukumbini. Tafadhali njoo ununue ili kuichangia jumuiya.

Hotuba Ya JK Kwenye Mkutano Mkuu Wa CCM Dodoma

HOTUBA YA MHE. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWENYEKITI WA CCM KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA NANE WA CHAMA CHA MAPINDUZI, UKUMBI WA KIZOTA – DODOMA, TAREHE 11 NOVEMBA, 2012

Utangulizi Mheshimiwa Dkt. Amani Abeid Karume, Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais Mstaafu wa Zanzibar; Ndugu Pius Msekwa, Makamu Mwenykiti wa CCM wa Bara; Mwenyekiti Mstaafu wa CCM,

Ndugu Benjamin William Mkapa; Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Waziri Mkuu; Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ;

 Viongozi Wakuu Wastaafu; Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Wilson Mukama; Ndugu Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM; Wageni wetu waalikwa kutoka vyama rafiki, Ndugu zetu wa Vyama vya Siasa Nchini; Waheshimiwa Mabalozi, Viongozi wa Dini, Wageni Waalikwa, Mabibi na Mabwana; Kama ilivyo ada, naomba tuanze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa Dodoma, siku ya leo, kwenye Mkutano Mkuu wa Nane wa Chama cha Mapinduzi.

 Ndugu Wajumbe;

 Karibuni Dodoma. Karibuni Mkutanoni. Nawapeni pole kwa safari. Tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kufika salama na tuombe turejee makwetu salama. Kwa niaba yenu, niruhusuni niwashukuru wenyeji wetu, yaani wana-CCM na wananchi wote wa Dodoma, wakiongozwa na Alhaji Adam Kimbisa, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dodoma na Mkuu wa Mkoa Dkt. Rehema Nchimbi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Tunawashukuru kwa kutupokea vizuri na kwa ukarimu wao unaotufanya tujisikie tuko nyumbani katika huu mji ambao ndiyo Makao Makuu ya nchi yetu na Chama chetu.

Ndugu Wajumbe;

Napenda kuchukua nafasi hii kutoa pongezi nyingi kwa Halmashauri Kuu ya Taifa kwa matayarisho mazuri ya Mkutano huu wa Nane wa Taifa wa CCM. Natoa pongezi maalum kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa chini ya uongozi mahiri wa Katibu Mkuu Ndugu Wilson Mukama na Kamati zote za Maandalizi ya Mkutano kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya ya kuwezesha Mkutano huu kufanyika. Kwenu nyote nasema hongereni na asanteni sana.

 Ndugu Wajumbe; Karibuni tena Kizota. Nasikitika kwamba .... Soma zaidi: http://www.kwanzajamii.com

Magazeti ya leo Jumatatu ya tarehe 12th November 2012