Friday, May 10, 2013

LADY JAYDEE AFUNGULIWA KESI MAHAKAMANI.....JOTO LIMEPANDA NA ANAMUOMBA MUNGU ASIKAMATWE MAY 31

Bado joto ya show ya mika 13 ya Lady JayDee inazidi kupanda kutokana na mengi yanayohofiwa kutokea siku hiyo.

Kwanza kulikuwa na tetesi kuwa huenda Clouds Fm wakafanya show nyingine siku hiyo, kitu ambacho Ruge Mutahaba alikifafanua vizuri kwa kusema mtu ukiwa na shughuli haimaanishi kuwa wengine wasifanye shughuli nyingine kama hiyo.

Lakini sasa kuna jingine ambalo limejitokeza, na amelisema mwenyewe Lady JayDee....

Kupitia akaunti yake ya Twitter Jide ameandika:

“Nimepata taarifa zisizo rasmi kuwa nimefunguliwa kesi mahakamani natumaini sitaitwa kizimbani tar 31 May ambayo ndio siku ya show.”

WAHANGA WA MLIPUKO WA BOMU KANISANI WAZIKWA KWA HUZUNI KUBWA

Misa ya Mazishi ya wahanga wa mlipuko wa bomu la Jumapili iliyopita kwenye parokia teule ya Olasiti ilianza katika eneo lile lile mlipuko ulipotokea.

Misa  hiyo  iliongozwa na Muadhama Polycarp Kardinal Pengo, Askofu Mkuu wa Dar es Salaam.

Maandamano yalianzia toka chumba cha kuhifadhia maiti, miili ikapelekwa makao makuu ya Asofu Mkuu, Burka  na  baadaye  ikawasilishwa kanisani .....

Mahubiri ya Kardinali Pengo
Ndugu zangu,

Nafasi hii inaunganisha mawazo ya furaha na uchungu kutokana na kilichotukutanisha leo.

Mazingira haya yanaweka ugumu wa kupata cha kusema. Ila sisi ni watu wa imani. napenda kueleza imani yetu kama tunavyopaswa kuwa kwenye mazingira haya.

Magazeti ya leo Ijumaa Ya 10th May 2013




HAYA NDO MAJINA 9 YA WATUHUMIWA WALIOLIPUA BOMU KANISANI ARUSHA

Imeripotiwa kuwa jumla ya watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Arusha kwa kutuhumiwa kuhusika na mlipuko wa bomu lililorushwa katika eneo la Kanisa la Mt Joseph Mfanyakazi katika parokia teule ya Olasiti siku ya Jumapili, Mei 5, 2013 na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60.

Ripota wa WAPO FM radio alisema majina ya watuhumiwa hao yametajwa kuwa ni:-

    1- Victor Ambrose Calist (20, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
    2- Joseph Yusuph Lomayani (18, mkazi wa Kwa Mrombo, Arusha)
    3- George Bartholomeo Silayo (26, mkazi wa Olasiti, Arusha)
   4-  Mohammed Suleiman Said (38, mkazi wa Ilala, Dar es Salaam, aliyewafuata kwa gari binafsi washukiwa wa ugaidi kutoka kiwanja cha ndege na kuwepeleka hadi hoteli ya Aquiline iliyopo Arusha)
   5-  Said Abdallah Said (28, mkazi wa Abu Dhabi, Nchi za Falme za Kiarabu)
   6-  Abdelaziz Mubarak (30, Nchi za Falme za Kiarabu)
   7-  Jassini Mbaraka (29 mkazi wa Bondeni, Arusha)
   8-  Foud Ahmad (28, Nchi za Falme za Kiarabu)
   9-  Said Mohsen (Najran, Saudi Arabia)

Hata  hivyo, himaya ya Imarati, Nchi za Falme za Kiarabu (UAE - United Arab Emirates)  inasema maafisa wake wamekanusha kuhusu raia wake watatu kuhusika na mlipuko wa bomu la Olasiti, Arusha.

Abu Dhabi ni mji mkuu wa Imarati (UAE), ambazo zina imirati saba -- Abu Dhabi, Dubai, Sharjah, Fujairah, Ras al Kaimah, Ajman na Umm a Quwain. Nchi jirani na UAE ni Qatar, Saudi Arabia na Oman.

Mapya bomu la Arusha:Majeruhi aeleza bomu lilivyokuwa

Bomu lililorushwa na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi huko Arusha, inadaiwa lilitengenezwa kienyeji.

Wakati kukiwa na madai hayo, mazishi ya marehemu hao Regina Kurusei, (45), James Gabriel (16) na Patricia Joachim (9) yanatazamiwa kufanyika leo Olasiti, Arusha na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuhudhuria.

Ofisa mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alimdokeza mwandishi wetu jana kuwa kwa ujuzi na uzoefu wake wa masuala hayo, bomu hilo si la kiwandani akisema msingi wa imani yake ni jinsi vyuma vilivyotawanyika na kuumiza watu zaidi ya 20.

Watu saba wamefikishwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuondolewa vyuma na kupata matibabu zaidi.

R.I.P ALL

Hali tulivu,baridi kiasi, majonzi yakiwa yametawala kila kona jijini arusha Tukiwasindikiza wapendwe wetu waliotangulia mbele ya haki siku ya jumapili 5/5/2013 katika mlipuko wa bomu kanisa la mtakatifu joseph olasiti.Hii ni chachu kwa wakristo wote Tanzania na dunia, sali kila sekunde uliyonayo kuombea AMANI nchi yetu.Mungu uwaangazie mwanga wa milele wapumzike kwa Amani Amina.