Saturday, November 10, 2012

MAMBO YALIVYOKUWA EBSS 2012 WALTER CHILAMBO AIBUKA KIDEDEA HAAAAA JAMAA MKALI

    Msanii Barnaba akiimba na mmoja wa washiriki wa shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),
                   Mshiriki wa EBSS NshomaNg'hangasamala akiimba moja ya wimbo wake jukwaani.
Mwanadada Salma Albushiri akiimba kwa hisia huku akipiga gitaa mbele ya mashabiki wake waliofika kumshuhudia ndani ya ukumbi wa Diamond usiku huu.
                                         Mapouda.! majaji hawaishi vituko
                                                                 Mashabiki
 Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Linah na Amin wakiimbwa kwa pamoja wimbo mpya uitwa Mtima Wangu





                               Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited,
 Mkurugenzi wa kampuni ya Benchmark Productions Limited, na jaji mkuu wa Shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS), akiwa amemkumbatia mshindi wa shindano hilo Walter Chilambo ndani ya ukumbi wa Diamond,Chilamba ameibuka na kitita cha shilingi Milioni 50
  Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akiwashukuru wapenzi na msahabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi wa shindano hilo,lililofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,

 Mshindi wa shindano la  Epiq Bongo Star Search 2012 (EBSS),Walter Chilambo (Dar) akikabidhiwa sanduku lake lenye kitita cha shilingi milioni 50 jana usiku ndani ya ukumbi wa Diamond jubilee,katika shindano hilo lililovuta hisia za wengi,mshindi wa pili ameibuka mwanadada Salma Abushiri  (Zanzibar) na watu ni Wababa Mtuka (Dar)
 Baadhi ya mashabiki wa mshindi wa shindano hilo la EBSS,Walter Chilambo wakishangilia kwa shangwe na vifijo mara baada kutamkwa yeye ndiye kinara katika kilele cha shindano hilo lililovuta hisia za watu wengi

                Huyu ni Salama Jabir  na hapa ni katiak yale ya Look ndani ya fainali za EBSS 2012
 Washiriki wa Washindano la EBSS 2012 ambao wamefanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa kuanza kwa fainali hizo. Ni ndani ya Ukumbi wa Diamond Jijini Dar es Salaam. Mshindi kuondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania.
  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya simu za Mikononi ya Zantel, Awaichi Mawalla akiwa katika mahojiano na mmoja wa ma MC wa sho ya leo Caesar Daniel,wakati akingia katika zulia jekundu la Fainali za EBSS nadani ya  Diamond Jubilee.




                                                      Mwasisi akitumbuiza jukwaani

                                                                          Majaji
                                                          Salma Yusufu
Shindano la EBSS usiku huu limefikia patamu baada ya washiriki 3 walio ingia katika fainali hizo kutoka na sasa kubakia washiriki wawili ambao ni Walter Chilambo na Salama Yusufu mwakilishi pekee kutoka kisiwani Zanzibar.

Washiriki waliotoka usiku huu na kuachia kitita chaa Shilingi Milioni 50, kikiwaniwa na Walter na Salama ni pamoja na Nsami Nkwabi, Nshoma Ng’hangasamala Wababa Mtuka.

Shindano la EBSS linafikia tamati yake usku huu katika ukumbi wa Diamond Jublee linapoendea kufanyika.
WALTER CHILAMBO ndiye mshindi wa Shindano la Epic Bongo Star Search (EBSS)  2012. Kufuatia matokeo hayo Kalambo amejinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania kutoka kwa wadhamini wakuu wa shindano hilo kampuni ya Simu za Mkononi ya Zantel.

Chilambo ametwaa ubingwa huo baada ya kumwangusha mwana dada kutoka Zanzibar ambaye alikuwa ni mshindani wake wa karibu katika kinyang’anyoro hicho Salma Yusufu.

Wanajeshi Wa Marekani Waadhibiwa

Wanajeshi saba wamarekani wa kitengo cha Elite akiwemo mmoja wa maafisa wa jeshi aliyehusika na kumkamata na kumuua Osama bin Laden wameadhibiwa kwa madai ya kutoa taarifa za siri za marekani kinyume na sheria.

Kuvunjwa kwa usalama huo kunadaiwa kujiri wakati wanajeshi hao walikuwa wakifanya kazi ya kutoa huduma za ushauri katika kutengeneza mchezo wa video inayoonyesha makabiliano ya kijeshi.

Saba hao walipata barua za nidhamu na kupokea nusu ya mishahara yao kwa kipindi cha miezi miwili .

Idara ya usalama ya marekani bado inachunguza iwapo maafisa zaidi wa kitengo cha Seal walihusika

Chanzo:  http://www.bbc.co.uk/swahili/news

Dk. Shein Afanya Mazungumzo Na Balozi Mdogo Wa India Zanzibar


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi Mdogo wa India wa Zanzibar, Pawan Kumar alipofika Ikulu Mjini Zanzibar Kujitambulisha kwa Rais.

  [Picha na Ramadhan Othman Ikulu]

Magazeti ya leo Jumamosi ya 10th November 2012