Wednesday, February 27, 2013

RIHANNA NA CHRIS BROWN WARIDHIA KUFUNGA NDOA JULY MWAKA HUU

Jarida maarufu (Star Magazine) limeripoti kwamba mastaa wa muziki Chris Brown na Rihanna wanampango wa kufunga ndoa mwishoni mwa July 2013 nyumbani kwa kina Rihanna huko Barbados.

Jarida hili limeendelea kutiririka kwamba kwenye ndoa hiyo wamepanga kusherehekea na watu mbalimbali wakiwemo wanaoamini kwamba Chris Brown amebadilika kitabia.

Ni harusi ambayo watu wote walioalikwa watakua wamesimama na wahudumu watakuepo kumfata kila mtu alipo, pia wale wachoraji wa tattoo watakuepo pia.

MAAJABU: KITANDA KIMOJA CHA HOSPITALI YA BUTIAMA HULAZA WATOTO WANNE....

HALI ya hospitali ya Butiama iliyopo wilayani Musoma mkoani hapa, iliyofunguliwa rasmi mwaka 1972 na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere imezidiwa na wagonjwa kutokana na kuachwa kama ilivyoziduliwa enzi za Mwalimu Nyerere. Tanzania Daima limebaini.

Hali hiyo imebainika jana baada ya jopo la waandishi wa habari za afya ya Mama, Baba na mtoto nchini kutembelea hospitali hiyo.

Waandishi hao walitembelea na kujionea hali halisi ya hospitali hiyo yakiwemo mawodi ya wagonjwa na vifaa vilivyopo ndai ya hospitali hiyo huku wakijionea mlundikano mkubwa wa wagonjwa.

MSANII OMOTOLA ANG'AA HOLLYWOOD

Muigizaji wa Nollywood, Omotola, Jalade- Ekeinde, ameanza kuonekan kwenye televisheni za Marekani, kwenye kipindi kiitwacho Bounce

Nyota huyo ambaye amekuwa Marekani kwa muda sasa ameanza kuonyesha uwezo wake mbele ya wakali wa Hollwood nchini Marekani

Baadhi ya wasanii mbalimbali kutoka Nigeria walishindwa kung'aa lakini msanii huyo amefanikiwa kushiriki kwenye tamthilia nchini Marekani

Katika tamthilia hiyo Omotola amecheza na Kimberly Elise

CHOCOLATE ZAMPONZA WEMA SEPETU NA KUMFANYA APOTEZE "MENO"

 CEO wa Endless Fame Films Wema Sepetu amelazimika kujisamilisha kwa daktari wa meno baada ya ulaji wa chocolate kumponza na hivyo kuozesha baadhi ya meno yake.

Tuesday, February 26, 2013

Redio mbili zafungiwa kwa uchochezi

KAMATI ya Maadili ya Utangazaji nchini imevifungia vituo viwili vya radio pamoja na kukipiga faini kituo cha Clouds FM kutokana na kukiuka maadili ya utangazaji.

Vituo hivyo vya redio ambavyo vyote kwa pamoja vimefungiwa kutorusha matangazo yake kuanzia leo kwa miezi sita ni pamoja na Imani FM cha Dar es Salaam na  Kwa-Neema FM kilichopo mkoani Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Walter Bgoya alisema Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kufuta kipindi
chake cha Jicho la Ng'ombe mara moja pamoja na kulipa faini ya sh. milioni 5.

Akifafanua zaidi Makamu Mwenyekiti huyo alisema vituo vya Imani FM na Kwa-Neema vimefungiwa kwa kosa la kufanya kazi zao kwa uchochezi jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya tasnia ya utangazaji. Kituo cha Clouds FM kimetakiwa kutoanzisha kipindi kingine kinacho fanana na Jicho la Ng'ombe.

Kituo cha Imani FM kinadaiwa kufanya uchochezi kwa wananchi juu ya suala la sensa ya watu na makazi huku kile cha Kwa-Neema kufanya uchochezi juu ya mgogoro wa
uchinjaji wanyama kwa Waislamu na Wakristu mkoani Geita.

Hata hivyo Kamati ya Maadili imeweka mlango wazi kwa vituo hivyo kukata rufaa endapo havikuridhika na adhabu vilivyo pewa kutokana na makosa vinao daiwa
kufanya.

Kamati Imevitaka vyombo vyote vya habari kufanya kazi kwa kuzingatia Kanuni Sheria na maadili ya tasnia hiyo ili kuepuka kuzua migogoro kwa wananchi ambao wamekuwa
wakiviamini vituo hivyo.

Hata hivyo mara baada ya ujumbe wa kamati hiyo kumaliza kusoma adhabu hizo kwa waandishi wa habari haukuruhusu maswali kwa waandishi wa habari, hivyo waandishi kubaki wameduwaa.

Na Thehabari.com

LOWASSA: CCM ITASHINDA 2015

 Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Moh Edward Lowassa amesema kuwa iwaposerikali zote mbili ile Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na ya visiwani, zitatekeleza  kwa usahihi maelekezo ya mkutano mkuu wa CCM juu ya suala la ajira basi chama hicho kitashinda kiurahisi katika uchaguzi mkuu wa 2015.

Utafiti: Dk Slaa aongoza vinara tisa urais 2015

 WAKATI baadhi ya wanasiasa wakiwa wameanza kujiwinda kwa ajili ya kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, Shirika la Utafiti la Synovate limetoa matokeo ya utafiti wake ambao unaonyesha vigogo tisa kuwamo katika mchuano huo.

Utafiti huo umeonyesha kuwa endapo uchaguzi huo ungefanyika sasa, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa angeibuka mshindi baada ya kuongoza orodha hiyo akipata asilimia 17.

Breaking News


Magazeti ya leo Jumanne ya 26th February 2013





LULU MICHAEL AJIPANGA KUJIENDELEZA KIMASOMO

BAADA ya kupata dhamana msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ajipanga kujiendeleza na masomo ili aweza kupambana na changamoto za maisha.

Akizungumza na Maisha msanii wa filamu ambaye pia amekuwa ni mtu wa karibu  familia ya Lulu Mahfudh Hussein 'Dkt. Cheni' amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo yake

TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI: KAMA UMEGUSWA MCHANGIE MTOTO HUYU AWEZE KUTIBIWA

 Mtoto Ombeni Mbeula akiwa na mama yake Kilaudia Kigaila wakiwa hospitali kama umeguswa na hali ya mtoto huyu tafadhari tuma choche kwa njia ya M-Pesa 0757 498336 ili apata matibabu.

PENZI LA DIAMOND NA PENNY LAZIDI KUOTA MIZIZI



MCHUNGAJI ALIYEKUBALI KUWATAHIRI WATOTO WAKE ARUSHA AVULIWA NGUO ZOTE NA KUCHAPWA VIBOKO

Mchungaji wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo katika kata ya Ngusero mkoani Arusha aliyedhalilishwa na vijana wa jamii ya kifugaji kwa kuvuliwa nguo zote na kuachwa uchi wa mnyama na kisha kutandikwa viboko amesema atanunua bunduki na kuitumia kuua endapo Serikali haitachukua hatua.

Mchungaji huyo alifanyiwa udhalilishaji huo hivi karibuni baada ya kuwatahiri wanawe katika hospitali ya Kiteto, jambo ambalo vijana wa jamii hiyo walisema ni kosa kwa kwenda kinyume na mila na destruri ya kuwatahiri kimila, na hivyo kumvua nguo, kumchapa, kumpiga na kumjeruhi.

Mchungaji huyo anasema aliripoti shambulio hilo katika kituo cha polisi na amekuwa akifuatilia lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa dhidi ya vijana hao wala kuulinda usalama wake ikiwa ni pamoja na kuenedelea kupewa vitisho.

WEMA SEPETU ATANGAZA AJIRA KWENYE KAMPUNI YAKE

Kampuni ya Wema Sepetu, Endless Fame Films, inatangaza nafasi za kazi mbalimbali ikiwemo ya usekretari, graphic designer, cameraman na editor.

Monday, February 25, 2013

WAKUU WA SHULE WADAI KUWA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE ILITUNGWA KWA MFUMO TOFAUTI....

  MATOKEO mabaya ya mtihani wa kidato cha nne yamezidi kuibua mapya, baada ya wamiliki wa shule na vyuo binafsi nchini kusema mitihani ilitungwa kwa mfumo tofauti na uliozoeleka miaka yote, huku tume iliyounndwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ikipondwa na baadhi ya watu.

Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi nchini (TAMONGSCO), Mahmoud Mringo alisema kwamba maswali waliyoulizwa watahiniwa yalikuwa ya kujieleza tofauti na miaka ya nyuma, ambapo mfumo uliotumika uliwataka watahiniwa kutaja vitu tu bila ya kulazimika kuvielezea kwa undani.

Kauli yake iliungwa mkono na Mkuu wa Taaluma katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian, Florence Mapunda ambaye alisema kuwa mtihani wa mwaka jana ulitaka zaidi watoto kujieleza tofauti na miaka ya nyuma wakati wanafunzi walipokuwa wanakariri.

STIVE NYERERE "ATIWA RUMANDE" BAADA YA KUVAANA KWA MANENO NA POLISI






 Mashuhuda wakishuhudia ajali hiyo, gari likiwa mtaroni.

WATUHUMIWA WALIOUKATA MKONO WA ALBINO WASOMEWA MASHITAKA KWA MARA YA KWANZA.....

Wanaoonekana pichani ni watuhumiwa watano wakiwa katika Mahakama ya Hakimu wa Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa wanaotuhumiwa kuukata na kuunyofoa mkono wa mwanamke albino, Maria Chambanenge (39) (hayupo pichani) na kutokomea nao wakimwacha na majeruhi makubwa kichwani. Mkono huo waliufukia porini kijijini Miangalua ambapo ulipatikana katika msako uliofanywa na Polisi.

Watuhumiwa hao ni pamoja na mfanyabiashara aliyekuwa mteja wa mkono huo (shati la bluu), mumewe Maria (koti jeupe, fulana rangi ya machungwa), mganga wa jadi, “mchora ramani” na aliyeunyofua mkono huo.

PICHA ZA MSIBA WA GOLDIE, MUME WAKE NA WENGINE WALIOHUDHURIA..

 
                                               Mwili wa Goldie Ukiwa umebebwa kwenye jeneza

                                                                 Andrew Harvey  Mume wa Goldie

Magazeti ya Jumatatu ya 25th February 2013



Kama mchezo vile ila ni ajali mbaya sana



Sunday, February 24, 2013

MDEE AONGELEA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE


Mheshimiwa Halima Mdee akinukuu ilani ya uchaguzi ya CCM wakati akijibu swali
Mbunge wa Kawe Mheshimiwa Halima Mdee amesema watoto wa viongozi kusoma shule za binafsi maarufu kama “Academia”  inachangia matokeo mabovu ya kidato cha nne kwa shule za kawaida. Mdee aliyasema hayo wakati akijibu swali la chanzo cha kushuka kwa kiwango cha ufaulu mwaka hadi mwaka wakati akiongea na Fina Mango katika Kipindi cha Makutano. “Kwa Mtazamo wangu mimi, zamani watoto wa viongozi tulikuwa tunasoma shule hizi za umma, kwa siku hizi tunawasomesha hizi shule za academia, kwa ubinafsi wetu hawa huku kwa kuwa watoto wetu hawapo hata ule moyo wa kutoa maelekezo unakuwa haupo”

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI



                                       TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete  leo Februari 24, 2013 ameungana na Wakuu wenzake wa Nchi za  Ukanda wa Maziwa Makuu  kutia  saini Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Amani, Usalama na Ushirikiano katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Mhe. Rais Kikwete alisema mara baada ya utiwaji saini wa Mpango huo kwamba: “Hii ni siku kubwa na ya kihistoria kwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jirani zake na Ukanda wote wa Maziwa Makuu. Ni siku ya kukumbukwa kwa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), Afrika, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa na Jumuiya yote ya Kimataifa. “Watu wa Kongo wameteseka kwa muda mrefu sana. Wanastahili kupumua sasa. Wanastahili kuishi maisha

POLISI YATANGAZA DAU ALIYEMUUA PADRI MUSHI



MWANANCHI
WAKATI kukiwa na taarifa kwamba maofisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) wametua nchini kwa ajili ya kufanya upelelezi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi, Jeshi la Polisi limetangaza dau la Sh10 milioni kwa atakayefichua aliyemuua padri huyo.Padri Mushi aliuawa kwa
kupigwa risasi Jumapili iliyopita wakati akienda kuongoza ibada katika Kanisa la Mtakatifu Teresia lililopo Beit el Ras nje kidogo ya mji wa Zanzibar, ambapo inadaiwa kuwa waliomuua walikuwa wamepanda pikipiki aina ya Vespa na walimfyatulia padri huyo risasi tatu akiwa ndani la gari yake.

Tuesday, February 19, 2013

KANISA LACHOMWA MOTO ZANZIBAR

Wakati Watanzania wakiendelea kutafakari tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Padre Evaristus Mushi, wa Kanisa Katoriki Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadaye kulichoma moto Kanisa la Walokole la Shaloom lililoko eneo la Kiyanga kwa Sheha mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar, ACP Augostine Olomi, alisema jana kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 9.30 usiku.

JOHN MNYIKA (MBUNGE) AWAJIBU NAPE NA RIDHIWANI KIKWETE JUU YA ELIMU YAKE

 UTANGULIZI

- Amesoma S/Msingi Mbuyuni (Dar) | Alichaguliwa kwenda Ilboru lakini hakwenda, akaenda Maua Seminary na alipata A tisa | Alisoma A-Level Tambaza | Ana BBA toka UDSM

- Amtaka Ridhiwan aongee na 'mshua' juu ya tatizo la maji Dar!

SASA  ENDELEA>>>>>>>

Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.

Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

HUU NDO WARAKA WA UAMSHO UNAOCHOCHEA MACHAFUKO NA MAUAJI YA WAKRISTU HUKO ZANZIBAR

Huu   ndo waraka uliosambazwa Zanzibar ukichochea  mauaji  ya  wakristu  ambao  wao  wanawaita  "MAKAFIRI"....

Swali  la  kujiuliza  ni JE, SERIKALI  ILILITAMBUA  HILI?..Maana  hizi  ni  dalili  za wazi kwamba  mauaji haya  YALIPANGWA.

NB: Hatutegemei lawama  toka  upande  wowote.Palipo  na  lolote sisi  hufichua  kwa uwazi  ili  kuifahamisha  jamii...

Kuna  haja  gani  ya  kuuficha  ukweli?...Ni bora kuuanika  ili watanzania  wenzetu walioko  zanzibar wachukue  tahadhari  wakisubiri   msimamo  wa serikali.

Chanzo  cha  waraka  huu ni blog ya zanzibar.

"RAIS KIKWETE ANA HASIRA, WANAOSEMA MPOLE HAWAMJUI"...MAMA SALMA

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCN, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete ametoboa siri kwamba mumewe, Rais Jakaya Kikwete pamoja sura yake kujawa haiba ya ucheshi wa mara kwa mara lakini kwa tabia ana hasira.

Amesema, Rais Kikwete hukasirika sana anapoona au kusikia mtu au mtendaji katika Chama au serikali anafanya mambo ya hovyo au ya kizembe hasa katika masuala ya kazi.

Mama Salma Kikwete ametoboa siri hiyo, leo Februari 18, 2013, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Kikwetu Kata ya Mbanja akiwa katika ziara ya kukagua, kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kuwashukuru wana-CCM wa Lindi mjini kwa kumchagua kuwa mjumbe wao wa NEC.

"SINA KINYONGO JUU YA PENZI LA DIAMOND NA PENNY"...JOKATE

BAADA ya Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kupata demu mpya, Penniel Mungilwa ‘Penny’, Jokate Mwegelo ametoa baraka zake kwa jamaa huyo aliyewahi kudaiwa kuwa mpenzi wake akisema haoni tatizo wawili hao kuwa pamoja kama kweli wamependana na kuridhiana.

Akizungumza katika mahojiano maalum alipobanwa kuhusiana na uhusiano wa wapenzi hao huku ikifahamika kuwa Penny alikuwa shosti wake, Jokate ambaye ni Miss Tanzania namba 2, 2006/07 alisema kwamba yeye na mrembo huyo walikuwa washikaji tu na wala hawakuwa na urafiki wa karibu kama baadhi ya watu wanavyoamini.

Jokate ambaye pia ni mtangazaji wa Runinga ya Channel O alifunguka kuwa anawatakia kila la heri na baraka zote Diamond na Penny katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi endapo tu watakuwa wamependana na kuridhiana kwa dhati.

“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu,” alifunguka Jokate ambaye pia ni bonge la mwigizaji.

Kabla ya kutoka kimapenzi na Penny ambaye naye ni mtangazaji wa Runinga ya DTV, Diamond aliwahi kuviteka vyombo vya habari akiripotiwa kuwa na Jokate, kabla ya mambo kwenda mrama.
tagazo

"SIPO TAYARI KUKUTANA NA LULU MICHAEL KUTOKANA NA UNYAMA ALIOUFANYA KWA KANUMBA"...MAYA

STAA wa filamu za Kibongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa tangu Elizabeth Michael ‘Lulu’ atolewe gerezani kwa dhamana, moyo wake unakuwa mzito kukutana naye.

Akipiga stori na mwandishi wetu, Maya aliweka plain kuwa kila anapofikiria ukaribu aliokuwa nao na marehemu Steven Kanumba, moyo wake unakuwa mzito kumuona Lulu ambaye alikuwa mpenzi wa marehemu.

“Mh! Kukutana na Lulu ni ngumu sana, sijui hata najisikiaje? Moyo unakuwa mzito sana kukutana naye na sijui kwa nini,” alisema Maya.

Baba Mtakatifu aanza wiki ya kufunga na kutoonekana hadharani.

Baba Mtakatifu Benedict wa 16 ameanza wiki yake ya mafungo ya kiroho ambapo atakuwa haonekani hadharani kwa wiki nzima ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kuelekea kuachia rasmi uongozi wa kanisa Katoliki na kusema kuwa ana matumaini ibada zake zitakuwa na mafanikio.

 Baba mtakatatifu atabakia Vatican na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu kwa ajili ya ibada za awali za sikukuu ya Pasaka na atapata mapumziko mafupi kila siku kwa ajili ya kuonana na katibu wake Georg Gaenswein, ili kuyashughulikia masuala ya dharura ya kanisa.

 Baada ya wiki nzima ya ibada, Baba Mtakatifu atakutana na rais wa Italia, Giorgio Napolitano, tarehe 23 Februari kushiriki ibada ya Jumapili yake ya mwisho ifikapo tarehe 24 mwezi huu na kuzungumza hadharani kwa mara ya mwisho mbele ya waumini wapatao 10,000.

Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani ataachia uongozi rasmi tarehe 28 mwezi huu na inasemakana kuwa Waziri wa Utamaduni wa Vatican Kadinali Gianfranco Ravasi ndiye anayeonekana mtu mwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi yake kwa muda mfupi au mrefu.

KAULI ZA SERIKALI YA ZNZ NA MAASKOFU WAKUU KATOLIKI KUHUSU MAUAJI YA PADRE.

 Baada ya kifo cha Padre Evarist Mushi ambae alifariki kwa kupigwa risasi Zanzibar jumapili iliyopita, kanisa Katoliki limewataka waumini wa kanisa hilo na Watanzania wengine kuwa watulivu na kufanya maombi ya amani katika kipindi hiki.

Askofu mkuu wa kanisa hilo Tanzania Muadhama Polycarp Cardinal Pengo amesema kifo cha Padre Mushi ni pigo kwa kanisa na Taifa na ni ishara ya kutoweka kwa amani hivyo hilo swala linatakiwa kufanyiwa kazi kabla ya madhara kuzidi, kwa sababu ukikosekana usalama kwa imani moja, kesho na kesho kutwa haijulikani ni imani gani ikashambuliwa.

Namkariri akisema “vyombo vya usalama vinatakiwa viwe makini, mimi sio mtaalamu wa usalama lakini naona ni jambo ambalo lingeweza kuzuilika na lisitokee kama watu wangesoma ishara za nyakati, wale wanaohusika wazuie kisitokee chochote… kuendeleza moyo wa kisasi hakutasaidia chochote na badala yake kutaleta madhara zaidi”

Magazeti ya leo Jumanne ya 19th February 2013





Saturday, February 9, 2013

Tanzania yashiriki utalii hispania

 Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Youssou Ndour Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini Senegal  ambaye pia ni mwanamuziki maarufu duniani wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho hayo , Youssou Ndour amewahi kufanya ziara ya kimuziki mara tatu nchini Tanzania kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini mwake.

Miss Utalii Tanzania 2013 kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii





    Miss Utalii Tanzania 2012/13 wiki ijayo wataanza ziara ndefu ya kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii katika mikoa ya Dar es salaam,Morogoro,Mtwara,Lindi na Pwani. Vivutio hivyo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Mikumi, Udizungwa, Saadani, Selous, pia maeneo ya kihistoria ya Bagamoyo, Amboni, Kijiji cha makumbusho,Makumbusho ya Taifa, Pugu sekondari,maeneo mengine ni ufukwe wa kigamboni, soko la kimataifa la Magogoni, Uwanja wa Taifa, uwanja wa ndege wa  J.K.Nyerere Air Port, Soko la Kariakoo, Mashule ya sekondari na msingi, pia watatembelea manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni ambapo watakutana na viongozi wakuu wa wilaya, mikoa, na wabunge katika majimbo ya mikoa hiyo.

JK atua msumbiji Jana

 Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya nchi jumuiya ya Maendeleo ya Uchumi Kusini Mwa Afrika SADC Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Maputo.Rais Kikwete yupo nchini Msumbiji kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC

MAgazeti ya leo Jumamosi ya 9th February 2013




YALIYOJIRI BUNGENI

 Mh Kigwangalla alimalizia kwa kusema “naomba atumie uungwana yeye mwenyewe kusimama katika bunge hili.. aidha kuwaomba radhi Watanzania kwa kudanganya ama kutimiza wajibu aliousema hapa yeye mwenyewe wa kujiuzulu, uongo aliousema ni mkubwa sana.. naomba nitoe hoja kwamba Mh Mbatia aadhibiwe kwa mujibu wa kanuni ya 63, asihudhurie vikao visivyozidi 20 na aombe radhi kwa maandishi kwa Watanzania kwa kusema uongo bungeni”

Friday, February 8, 2013

MSIKUBALI KUDANGANYWA ANGALIENI MAFANIKIO YENU- PALANGYO

WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Meru,mkoani Arusha,wameshauriwa kutokukubali kudanganywa na Vyama vya kisiasa ambavyo vinaeneza Propaganda chafu  kuwa hakuna kilichofanyika tangia Uhuru,badala yake wachukie siasa zinazosababisha uvunjifu wa amani

KAMPUNI YA NDEGE YA fastjet YAKANUSHA UVUMI KUWA IMEFUTIWA LESENI YA BIASHARA

Jean Uku Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni ya ndege ya Fastjet akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Hyyat Regency Dar es salaam kukanusha uvumi wa habari zinazosema kampuni hiyo imenyang’anywa leseni ya kufanya biashari nchini Tanzania, Kushoto ni Givaldine Dawe Meneja Utawala.

Pamoja na habari zilizoandikwa na kusemwa kwenye vyombo vya habari leo, biashara ndani ya kampuni ya fastjet inaendelea kama kawaida. Madai yanayotukabili ya kunyang’anywa leseni hayana ukweli wowote. Tunaendelea kufanya kazi na ndege zetu nchini Tanzania kama kawaida na bado tunazidi kuzindua vituo vipya kama ilivyopangwa. Huu ni uzushi wa baadhi ya watu au kampuni zenye chuki dhidi ya kampuni ya fastjet, kusudi lao ni kudhoofisha uaminifu na kuharibu sifa ya jina la biashara na bidhaa zetu za fastjet.

Ofisi zetu na vituo vyetu vya kuuzia tiketi bado viko wazi kwa ajili ya bookings na Kwa tiketi zilizolipiwa pesa haitarudishwa.

TAMKO RASMI BAADA YA MASAA MACHACHE