Thursday, June 6, 2013

HATIMAYE NGWEA AZIKWA KWENYE MAKABURI YA KIBONDA MKOANI MOROGORO....HIZI NDIO PICHA ZA MAZIKO YAKE

 Baada ya siku kadhaa zilizokuwa na kila aina ya harakati, ugumu na majonzi makubwa, Albert Mangweha aka Ngwair leo amezikwa kwenye makaburi ya Kihonda mkoani Morogoro ambako ni nyumbani kwao.

PICHA ZA M 2 THE P AKILIA KWA UCHUNGU WAKATI WA KUMUAGA ALBERT NGWEA MOROGORO MCHANA HUU

M2  THE P amefanikiwa  kutoa  salamu zake  za  mwisho  kwa  rafiki yake  kipenzi  ambaye  alikuwa  naye  huko  Afrika  kusini  tena  walikuwa  ndani  ya  chumba  kimoja  kabla ya  mauti  kumkuta Ngwea....!!

Mwanzoni, M 2 THE P alikuwa  amefichwa  na  kudanganywa  kuwa  Ngwea  alikuwa  ametangulia  Tanzania. Baadaye  Maggie  alilazimika  kumweleza  ukweli......

M 2 THE P AREJEA TANZANIA KUMZIKA MANGWEA LEO

Rafiki wa wa karibu wa marehemu Albert Mangwea aliyekuwa amelazwa nchini Afrika Kusini amerejea Tanzania na yuko njiani akielekea mkoani Morogoro kwaajili ya kushiriki mazishi ya swahiba wake Mangwea jioni ya leo (June 6).

Akizungumza na Times Fm asubuhi hii Mgaza Pende a.k.a M 2 The P amewashukuru watanzania kwa kumuombea japo hali yake bado haijawa nzuri sana lakini ameamua kurudi Tanzania kuja kumzika ndugu yake Mangwea.

“Ndugu zangu watanzania mimi ni Mgaza Pende M 2 The P nawashukuru sana kwa kuniombea mpaka muda huu, nimeweza kuwasili Tanzania salama na tutakuwa pamoja kwenda kumzika ndugu yangu kipenzi changu Albert Mangwea, nawashukuru sana watanzania kwa kuniombea asanteni na endeleeni kuniombea hali yangu bado haijawa nzuri zaidi, asanteni,” alisema.
Msikilize hapa

Magazeti ya leo Alhamisi ya 6th June 2013





PICHA MSANII M 2 THE P AKIBEMBELEZWA KIAINA NA HUYU MREMBO..BADO HAJUI KWAMBA MANGWEA KAFARIKI

Msanii M2 the P aliyekutwa mahuhuti pamoja na Ngwair ambaye alifariki, anaendelea vizuri kiafya na ameshatoka hospitali. Mpaka sasa M To The P hajui kama Mangwea amefariki na anadhani mwenzake ametangulia kwenda Dar es Salaam.

M2 the P alipotembelewa na huyu sister anayeitwa Magie aliyeenda kumjulia hali baada ya msanii huyo kutoka hospitali M2 the P alipotembelewa na huyu sister anayeitwa Magie aliyeenda kumjulia hali baada ya msanii huyo kutoka hospitali m2-the-p
"Hapo Magie anamtania ikabidii amyeyushe eti ukirudi bongo mwambie Mangwea nina case nae yakuondoka bila kuniaga. Dah so so sad"- Jestina George “Hapo Magie anamtania ikabidii amyeyushe eti ukirudi bongo mwambie Mangwea nina case nae yakuondoka bila kuniaga. Dah so so sad”- Jestina George Magie amekuwa karibu sana na M2 The P na alikua karibu na marehemu Albert “Ngwair” Mangwea kwa muda waliokuwa Africa Kusini. kama inavyoonekana pichani,

 Magie alienda kumcheki M2 The P, kumpa moyo na kumchangamsha. Alipo fika alimkuta M2 The P amejawa na mawazo huku kikombe chake cha chai kiko mezani ikabidii aanze kumtania tania angalau aondokane na mawazo. Bado anamuuliza rafiki yake kipenzi Mangwea maana hajui yaliyo mfika. Tuendelee kumuombea M2 The P maana ana mtihani mkubwa mbele yake akija kujua ukweli, na ni Mungu pekee ndo ataweza kumsaidia.

VYAMA VYA UPINZANI VYANUIA KUUNGANA 2015

Vyama vya siasa vyenye idadi ndogo ya wanachama nchini vimekubali hatua ya kuungana na kuwa Muungano wa vyama (Alliance) kwa lengo la kupata nguvu ya uwakilishi wa kuingia katika Bunge Jipya la Shirikisho baada ya rasimu mpya kupitishwa kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Hatua hiyo imekuja baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kutangaza rasimu iliyotoa mwelekeo wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania.

Akizungumza jana na gazeti la Mwananchi, Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Samweli Ruhuza amesema hali hiyo inaweza kuleta changamoto kubwa hivyo muda sahihi wa vyama vichanga kuzungumzia hili ni sasa.

Katibu mkuu wa chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muhabi anaunga mkono hatua ya kuunganisha vyama hivyo kwa lengo la kuwakilisha mawazo yao kwa maslahi ya taifa.

MUME WA KHADIJA KOPA AFARIKI DUNIA

                          Khadija Omar Kopa akiwa na mumewe Jaffari Ally enzi za uhai wake.

Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya wilaya Bagamoyo.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.

PICHA TOKA MOROGORO AMBAKO MWILI WA ALBERT NGWEA UMEPOKELEWA TAYARI KWA MAZISHI




Msafara wa kupokea mwili wa msanii  marehemu Albert Mangwea ukiwa unaingia morogoro hapa ni eneo la nane nane,Umati mkubwa umejitokeza katika mapokezi mpendwa wao