Saturday, September 15, 2012

Inaijua asili yako tanzania asilialive inakuletea utamaduni mwa mwaafrika halisi

 Mimi ni Msandawe ingawa nimezaliwa mjini ila nafahamu nilikotoka wazazi na Babu zangu hasili ya kwetu ni nyumba hizi za tembe ndizo walizokulia wazee wangu pamoja  na shida walizo pata bana wanajivunia kuwa mwaafrika tena msandawe kabila lisiloweza kuandikika hiyo ni moja kati ya vitu vya kujivunia ingawa kwa upande mwingine ni hasara sana



Hawa  ni akina mama ambao ni majirani wa wasandawe yaani wagogo mkoani dodoma unajua hilo





Je watanzania tuna vazi la kitanazania ili tuweze kujivunia mimi na wewe. Kama una picha yako ya mavazi ya kabila yako tutumie tanzania asilialive ipo kwa ajili yako tuma kwa email, Asilialive@yahoo.com

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 LARINDIMA UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA USIKU HUU


 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dkt. Rehema Nchimbi akitangaza namba ya mshindi wa bahati nasibu ya gari aina ya Toyota Virtz  aliyejishindia gari hilo katika droo ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mkoani Dodoma kwenye tamasha la lililofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma usiku huu, aliyeshika kompyuta ni Meneja masoko wa kampuni ya Push Mobile Rugambo Rodney, kulia ni Mkuu wa wilaya ya Dodoma Lephy Gembe na wa pili kutoka kulia ni mwakilishi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Bw. Humud.

Katika tamasha hilo wasanii mbalimbali wanatumbuiza katika tamasha hilo kubwa  baada ya matamasha mengine kama hayo katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Mwanza, Shinyanga, Mara, Tabora, Singida na sasa mkoani Dodoma.
Waigizaji wa filamu wakielezea uwezo wao katika kusakata muziki kutopka kulia ni Jacob Steven JB, Wema Sepetu, na Aunt Ezekikel.
Aunt Ezekiel akimwaga mauno yake lanini mbewle ya mashabiki
Raymond Kigosi Ray akifanya vitu vyake katika kusakata mayenu.
Wema Sepetu akinyonga viuono mbele ya mashabiki wa tamasha la Serengeti Fiesta uuwanja wa  mjini Jamhuri Dodoma

                                   Rachel na mmoja wa wanenguaji wake jukwaani.
 Rachel akifanya vitu vyake jukwaani
 Msanii Young Killer akionyesha uwezo wake mbele ya mashabiki kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma
 Msanii w a muziki wa kizazi kipya Bongofleva Ommy Dimpoz akifanya vitu vyake kwenye Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma
 Msanii Richa Mavoko akionyesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta linalofanyika musiku huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
                                            Richa Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake

 Mtangazaji wa kituo cha rediao cha Clouds FM Gea Habib akiwa pamoja na wadau wengine wa fiesta kwenye uwanja wa jamhuri usiku huu katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
                                                          Mashabiki wakiwashangilia
 Shetah msanii wa muziki wa kizazi kipya bongofleva akifanya vitu vyake jukwaani katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma,
 Msanii Diana akiwa amebebwa juu juu na wacheza shoo wake katika tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini Dodoma  katika uwanja wa Jamhuri.
             Msanii Diana kutoka THT akiimba katika tamasha hilo usiku huu kwenye uwanja wa Jamhuri.

ZIARA YA WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA NGUDU MKOANI MWANZA

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akifungua mradi ya Ufugaji nyuki katika kijiji cha  Nkalalo   wilayani kwimba akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza Septemba 14, 2012. Nyuma yake ni mkewe Tunu na kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarest Ndikilo na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Suleiman Mzee. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wasanii wa Kikundi cha Ng’wanadelema cha Ngudu wilayni Kwimba wakicheza ngoma ya Wayeye wakai Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasalimia wnanchi katika kijiji cha Nkalalo wilayani Kwimba akiwa katika ziara ya Mkoa wa Mwanza Septemba 14, 2012.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunuwakiwa wamevikwa mavazi ya kiongozi wa jadi wa Sungusungu katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Ngudu Septemba 14, 2012.
Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Kwimba  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mpira wa miguu  wa Ngudu akiwa katika ziara ya mkoa wa Mwanza Septemba 14,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Ajali Mbili Zaua Watu Wanane Siingida.

 Wananchi wa mji wa Singida wakiwa wamekusanyika nje ya viwanja vya chumba cha kuhifadhia maiti ktk hospitali ya mkoa wa Singida
Wauguzi wa hospitali ya mkoa wa Singida wakijiandaa kumsaidia mmoja wa majeruhi wa ajali ya lori iliyotokea wakati wakienda mna

WATU wanane wamefariki dunia katika ajali mbili tofauti zilizotokea mjini Singida kwa kuhusisha magari mawili, ikiwemo Landrover ya polisi na kusababisha jumla ya majeruhi 25. Ajali hizo zimetokea jana (14/9/2012) moja saa 5:30 asubuhi na nyingine saa 6:30 mchana.

Landrover ya polisi iliyohusika na ajali hiyo ni namba PT 1149 kutoka mkoni Morogoro ikiwa na abiria 11 waliokuwa wanasindikiza mwili wa askari polisi Regu Kamamo, kwenda Musoma kwa ajili ya maziko.

Kamanda wa polisi mkoa mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa alisema kuwa gari hilo lilipata ajali katika kambi ya Wachina iliyopo eneo la Manguajunki nje kidogo ya mji wa Singida.Aliwataja walifariki katika ajali iliyohusisha gari la polisi ni, staff sajenti Rose Mary Nyaruzoki (53), Nyamwenda Juma, Rehema Juma.

Sinzuma alisema uchunguzi zaidi bado unaendelea ili kubaini chanzo cha ajali hiyo huku akifafanua kuwa majeruhi wanane wa ajali hiyo wamelazwa hospitali ya mkoa Singida na hali zao zinaendelea vizuri.

Katika tukio la pili, alisema lori Fusso T.126 AEU likiwa na wafanyabishara wa mnadani likitokea Singida mjini kwenda mnada wa Mtavira kata ya Minyunge wilaya ya Singida, lilipinduka na kusababisha vifo vya watu watano na majeruhi 17
Alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 6.30 mchana katika kijiji cha Mtavira, Singida vijijini.Aliwataja waliofariki dunia papo hapo ni Sarafina Ally, Pili Saida, Charles Thomas na wengine wawili waliofahamika kwa jina moja moja la Bakari na Bilali.

Alisema chanzo cha ajili ya fuso,bado hakijafahamika na uchunguzi zaidi bado unaendelea. Hata hivyo Sinzumwa alisema taarifa kamili kuhusiana na ajali hizo, atazitoa kesho (leo 15/9/2012) .Mganga mfawidhi hospitali ya mkoa Singida, Dk. Joseph Malunde alisema majeruhi hao 17, wamelazwa hospitali ya mkoa wa Singida na hali zao zinaendelea vizuri.

"Maiti zote tisa pamoja na ile ya askari aliyekuwa anasafirishwa na gari la polisi na zile za Fusso, zimehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa,"alisema Dk. Malunde.

Kwa mjubu wa mmoja wa majeruhi wa fuso,Maulidi Mohammed,fuso hilo lilipinduka baada ya breki zake kufeli likiwa kwenye mteremko mkali hali iliyosababisha dereva ambaye hata hivyo hajafahamika ashindwe kulimudu.

Na: Elisante John-Singida

Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari-TahadharI Dhidi Ya Mvua Za Oktoba 2012–Disemba, 2012

 
Kufuatia Utabiri wa Hali ya Hewa uliofanywa kwa pamoja na Mamlaka za Hali ya Hewa kwa nchi za Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki, Mamlaka ya Hali ya Hewa - Tanzania imetoa taarifa kuhusu uwezekano wa nchi kupata mvua nyingi iliyo juu ya wastani. Hali hii ya kuwa na mvua nyingi inatabiriwa kuikumba nchi kwa kipindi cha Oktoba, 2012 hadi Disemba, 2012 na huenda ikaendelea zaidi.

Kanda ya Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza, Geita, Simiyu na Shinyanga). Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya tatu ya mwezi Septemba, 2012 katika mkoa wa Kagera na kaskazini mwa Kigoma na kuendelea kusambaa katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Mara, Geita na Simiyu katika wiki ya nne ya mwezi Septemba, 2012. Kwa ujumla mvua hizo zinatarajiwa kuwa juu ya wastani katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Viktoria.

Ukanda wa Pwani ya Kaskazini (Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Morogoro-kaskazini pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba): Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza ya mwezi wa Oktoba, 2012. Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.

Nyanda za juu Kaskazini Mashariki (Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara). Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza katika wiki ya pili ya mwezi Oktoba, 2012 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani.

Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi na Rukwa).
Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya tatu ya mwezi Oktoba, 2012 katika mkoa wa Kigoma na wiki ya pili ya mwezi Novemba katika mikoa ya Tabora, Rukwa na Katavi. Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika mikoa ya Rukwa na Kigoma. Aidha maeneo mengi ya mikoa ya Katavi na Tabora mvua zinatarajiwa kuwa juu ya wastani.

Kanda ya kati (Mikoa ya Singida na Dodoma). Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya mwezi Novemba na zinatarajiwa kuwa za juu
ya wastani.

Nyanda za juu Kusini Magharibi (Mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe na kusini mwa Morogoro): Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya mwezi Novemba 2012 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika mkoa wa Njombe na kusini mwa mikoa ya Mbeya na Morogoro. Maeneo ya kaskazini mwa mikoa ya Mbeya na Iringa, mvua zinatarajiwa kuwa juu ya wastani.

Maeneo ya Kusini na Pwani ya Kusini (mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara): Mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya nne ya mwezi Novemba, 2012 na zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi.



Kwa kuzingatia hali hii Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa tayari imetoa taarifa/elimu kwa umma kupitia kipindi cha “Tuambie” cha TBC 1 na kuelekeza taasisi na wadau mbalimbali kuchukua hatua za tahadhari. Mfumo wetu wa kukabiliana na maafa una Kamati za Maafa kwenye ngazi ya mkoa, wilaya hadi kijiji ambazo zina majukumu ya kusimamia masuala ya maafa katika maeneo yao. Kamati zilizoanishwa hapo juu pamoja na wadau wote mnakumbushwa kujiandaa kukabiliana na maafa endapo yatatokea. Katika jitihada za kujiandaa mnakumbushwa kuzingatia yafuatayo:-

1. Kutekeleza mipango mbadala katika maeneo mliyobaini kuwa yana uwezekano mkubwa wa kukumbwa na mafuriko; kama vile kuhamisha wananchi maeneo ya mabonde kwenda sehemu salama na kurejesha mawasiliano endapo yataharibika.
2. Kupatikana dawa muhimu za magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu na madawa ya kusafisha maji ya kunywa (Water Guard Tablets).

3. Kupatikana kwa dawa muhimu za mifugo kwani magonjwa miguu na midomo (FMD) na homa ya bonde la ufa (RVF) yana uwezekano mkubwa wa kutokea.
4. Upatikanaji wa chakula cha kutosha. Aidha wananchi wahimizwe kuweka akiba ya chakula cha kutosha.

5. Kutenga fedha za kukabiliana na maafa endapo yatatokea.
6. Elimu kwa Umma itolewe kwa kuhusisha vyombo vyote vya mawasiliano na uongozi wa Vijiji na Mitaa.

7. Kuchukua hatua za ziada kwa maeneo ambayo yana uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na mmomonyoko wa ardhi.

8. Kuainisha mitaro inayoweza kuingiza maji katika migodi ya wachimbaji wadogowadogo, na kuchukua tahadhari zinazostahili.

9. Kuhakikisha kuwa mifereji na mitaro ya maji machafu kwa maeneo ya Jiji/miji iko safi na wazi wakati wote kupitisha maji.

10. Kuchimba au kukamilisha uchimbaji wa mabwawa ya kuvuna maji ya mvua.
11. Maofisa Ugani - Kilimo kutoa ushauri kwa wakati kuhusu mazao ya kupanda na pia wafugaji kutumia nafasi kuvuna malisho ya kutosha yatakayotumika kipindi cha kiangazi .

12. Kila ngazi kujiweka tayari kukabiliana na mafuriko ni muhimu kuunda timu za wataalam wa kukabiliana na athari zitakazotokea, majina yao yaainishwe na waelekezwe cha kufanya pindi hali ikiwa hivyo.

Ni matumaini yangu kuwa tukishirikiana katika kukabiliana na mvua nyingi pamoja na majanga yanayoambatana na mvua hizi, tunayo nafasi kubwa ya kujihakikishia usalama wa nchi yetu kutokana na majanga ya asili.

Nashukuru kwa ushirikiano wenu.
IMETOLEWA NA KATIBU MKUU, OFISI YA WAZIRI MKUU

Magazeti ya leo Jumamosi 15th September 2012