Wednesday, March 20, 2013

BREAKING NEWS YA SASA HIVI KUHUSU LWAKATARE WA CHADEMA


RAIS KIKWETE AHANI MSIBA WA TRAFIKI ALIYEGONGWA MAENEO YA BAMAGA

Taarifa tulizozipata zinaeleza kuwa  yule dereva aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2493 CPL-Elikiza  Lokisa Nko na kutokomea, amekamatwa juzi usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya Bamaga mapema jana mchana.

Kwa Mujibu wa Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Usalama barabarani nchini, Kamanda Mohamed  Mpinga alisema jana kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo aina ya Landlover Discovery rangi nyeusi limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.

Kupatikana kwa gari hilo kumekuja baada ya Polisi kufuatilia na kujua mmiliki wa gari hilo kuwa ni kanisa la TAG chini ya Mchungaji Wambura, ambaye kwa ushirikiano alioutoa dereva aliyetambuliwa kama Jackson Stephen, alijulikana na hatimaye kupatikana

Kamanda Mpiga alitoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete jana jioni nyumbani kwa Marehemu hukoUnunio kiasi cha kilomita 25 hivi Kaskazini mwa jiji la Dar.

Rais Kikwete pamoja na uongozi wa juu wa jeshi la polisi walifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha  Mume na watoto watatu. Mume wa marehemu pia ni askari polisi.

NANCY SUMARI AZINDUA KITABU CHA WATOTO NYOTA YAKO

 Miss World Africa 2005, Nancy Sumari leo amezindua kitabu chake cha watoto kiitwacho Nyota Yako. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu wakiwemo mamiss Tanzania wa zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe na Faraja Nyalandu.
 Nancy Sumari akizungumza kwenye uzinduzi huoNancy Sumari akizungumza kwenye uzinduzi huo

Wengine ni pamoja DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya watoto na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Profesa Esther Mwaikambo, Jokate Mwegelo, Shaa, Ally Remtullah. Fina Mango na wanafunzi mbalimbali.
Akizungumzia jambo lililomsukuma kuandi ka kitabu hicho, Nancy alisema:
Vilinisukuma vitu vingi, kwanza nafasi ya mwanamke kwenye jamii yetu, umuhimu wake, sababu ya kumuenzi na kumsherehekea na kutambua michango yetu, mwanamke mdogo, msichana mdogo, mama zetu, bibi zetu. Kuna kila sababu ya sisi kuangaliana na kutambuana na pia kufananisha.

DEREVA ALIYEMGONGA TRAFIKI JANA AMEKAMATWA

Taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa  yule Dereva aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2492 CPL-Elikiza na kutokomea, amekamatwa jana usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya Bamaga mapema jana mchana.

kwa Mujibu wa kamanda wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani nchini,Kamanda Mohamed  Mpinga amesema leo kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.

Kamanda Mpiga ametoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete nyumbani kwa Marehemu,hukoUnunio,kaskazaini mwa jiji la Dar. Rais Kikwete alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha  Mume na watoto watatu.