Thursday, August 9, 2012

Sekretarieti Ya Ajira Yatoa Ratiba Ya Usaili Kwa Mwezi Agosti, 2012

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, Bw. Xavier Daudi akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari hawapo pichani na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Ajira, Bw. Bakari Mahiza.

Sekretarieti ya Ajira imetangaza ratiba ya usaili kwa mwezi Agosti, 2012 kwa waombaji nafasi za kazi katika Taasisi za Umma kwa wale waliokidhi vigezo. Tangazo hilo limetolewa leo na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira, Bw. Xavier Daudi alipokuwa akiongea na Waandishi wa habari ofisi kwake.

Daudi amesema usaili huo utafanyika katika Mikoa sita ambayo ni Dodoma, Morogoro, Manyara, Arusha, Dar es Salaam na mkoa wa Pwani.

Amesema usaili umeanza tarehe 6 hadi 7 Agosti, mwaka huu kwa mkoa wa Manyara, wilaya ya Babati kwa nafasi za Mtandaji wa Kata, kijiji na Madereva, ilihali kwa mkoa wa Dodoma umeanza tarehe 7-9 Agosti, 2012 katika Chuo cha Serikali za Mitaa, Hombolo kwa nafasi Wahadhiri wasaidizi, Afisa Utumishi, Afisa Tawala, Watunza kumbukumbu, Madereva na  Wasaidizi wa Ofisi.

Aidha, usaili utafanyika pia katika Chuo cha Mipango Dodoma (IRDP) kuanzia tarehe 10-14 mwezi huu kwa kada za Afisa Ugavi, Afisa Utumishi, Mkutubi na Afisa Mitaala. Wakati katika Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Biashara (COASCO) utaanza tarehe 15-16 Agosti kwa kada za Wakaguzi wa hesabu wa ndani, Wakaguzi Wasaidizi wa hesabu wa ndani na nafasi ya  Katibu Mahususi.

BALOZI MAHALU ASHINDA KESI

Balozi Profesa Mahalu akiwa pamoja na Mdogo wake Mirasi Rama wakitoka nje ya Mahakama ya Kisutu Mchana huu mara baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikimkabili akidaiwa kununua nyumba ya Ubalozi wa Tanzania nchini Italia, Akisoma hukumu iliyosomwa  kuanzia Saa sita leo na  Hakimu Mfawidhi mkazi wa mahakama ya Kisutu Mh. Ilivin Mugeta imemtoa Balozi Profesa Mahalu katika hatia na kumwachia  huru

(Picha Kutoka: Fullshangweblog)

Rais Kikwete akutana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe Morgan Tsvangirai

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha  Waziri Waziri Mkuu wa Zimbabwe Bwana Morgan Tsvangirai ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Baadaye Bwana Tsvangirai aliondoka kurejea nchini kwake
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri Waziri Mkuu wa Zimbabwe Bwana Morgan Tsvangirai ikulu jijini Dar es Salaam leo mchana.Baadaye Bwana Tsvangirai aliondoka kurejea nchini kwake
(picha na Freddy Maro)

KAMANDA LEMA AKIAGANA NA MWENYEKITI WA CHADEMA LONDON

Kamanda Godbless Lema  (kushoto) akiagana na Mwenyekiti wa tawi la CHADEMA London, kamanda Chris Lukosi  wakati akielekea Frankfurt ambako ataendelea na kazi yake ya kufungua matawi  ya CHADEMA.

JK: Alivyomfunga Mdomo Membe Sakata La Rada

KAULI iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete kwamba hakuna ushahidi wa kuwashtaki watuhumiwa rushwa ya rada, inaonekana kumfunga mdomo Waziri wake wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye aliwahi kuahidi kwamba angewataja watuhumiwa hao.

Rais Kikwete alipokutana na wakuu wa vyombo vya habari wiki iliyopita, alisema Serikali inashindwa kuwashtaki waliotuhumiwa katika suala hilo kutokana ukweli kwamba hata Uingereza walikana Kampuni ya BAE Systems kutoa rushwa na badala yake wakasema ilikosea katika kuandika hesabu zake.

Wakati Rais Kikwete akisema hakuna ushahidi wa kuwashtaki watuhumiwa wa rushwa ya rada, tayari Membe alikuwa amesema watuhumiwa wapo, anawajua na aliahidi kwamba angewataja bungeni.

Hata hivyo, Membe aliyewasilisha Hotuba ya Makadirio ya Matumizi ya wizara yake bungeni juzi, alishindwa kutekeleza ahadi yake licha ya kutakiwa kufanya hivyo na baadhi ya wabunge, wakiongozwa na Waziri Kivuli wa wizara hiyo, Ezekia Wenje ambaye pia ni Mbunge wa Nyamagana (Chadema).

Juzi, kabla Membe hajasoma hotuba yake, Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe alitoa taarifa rasmi ya Serikali bungeni kuhusu suala hilo na alisema kuwa, hakuna mtuhumiwa wa rada anayeweza kupelekwa mahakamani na kutamka kwamba mjadala kuhusu suala hilo umefungwa rasmi.

“Hata Uingereza iliyochunguza suala hilo imeeleza bayana kwamba hakuna rushwa na katika hatua hiyo, Serikali haiwezi kumfikisha mtu yeyote mahakamani,” alisema Chikawe.

Kauli hiyo ya Serikali inaonekana kuwakera baadhi ya wabunge ambao jana waliliambia gazeti hili kwamba wanashangazwa na jinsi Serikali ilivyomaliza na kufunga mjadala wa ufisadi wa rada, hali kukiwa na kila dalili kwamba wapo Watanzania waliohusika katika ufisadi huo.

Kauli za wabunge
Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisema: “Ushahidi wa kwanza ni fedha zilizorejeshwa kwa sababu Watanzania walilipa zaidi. Kama kuna fedha zililipwa zaidi, iweje asipatikane mtu wa kuchukuliwa hatua. Tulivyoelezwa ni kuwa vyombo vya uchunguzi vilikuwa vinachunguza suala hili, sasa tunashangaa kuelezwa kuwa hakuna uchunguzi unaoendelea.”
Alihoji kama fedha zaidi ya Sh70 bilioni zililipwa zaidi, kwa nini waliohusika na uzembe huo wasichukuliwe hatua?

Alisema kama fedha za nchi zimelipwa zaidi,
inawezekana kulikuwa na ufisadi au uzembe na hayo yote yanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangala alisema kuwa, amefurahishwa na msimamo wa mawaziri katika suala hilo ingawa haamini kama ungekosekana ushahidi wa kumnasa aliyehusika.“Siamini kama ilishindikana kupata ushahidi, ninachokiona ni kwamba hakukuwa na juhu di za kuhakikisha unapatikana ushahidi na wahusika waliamua jambo hili liende kama lilivyo.

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alisema atamwandikia rasmi Spika kwa mujibu wa Kanuni ya 46 ili waziri atakiwe kujibu kwa ukweli na kuacha kutetea ukiukwaji wa sheria.

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz

Benki Ya KCB Tanzania Yatoa Msaada Hospitali Ya Wazazi Zanzibar

 Katibu wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Bw.Omar Abdallah akipokea misaada ya vyandarua, mashuka pamoja na mashine ya kupumlia wagonjwa mahututi (Oxygen Conamtrator) vyenye thamani ya Milioni Tano kwa ajili ya Hospitali ya Wazazi ya Mwembeladu kutoka kwa Meneja wa Banki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Bw.Rajabu Ramia. Kulia ni Meneja wa Biashara wa Benki hiyo tawi la Zanzibar Bw.Abdallah Mshangama.
 Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Stone Town Zanzibar Bw.Rajabu Ramia, akimkabidhi Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Mwembeladu Zanzibar Bi.Zawadi Suleiman, Vyandarua na mashuka 50 vilivyotolewa na Benki ya KCB kama msaada kwa hospitali hiyo ya wazazi.
Afisa Uhusiano wa Benki ya KCB Tanzania Bi. Martha Edward akimpatia zawadi ya Tende Bi.Amina Ahamed alielazwa kwenye Hospitali ya Wazazi ya Mwembeladu Zanzibar mara baada ya wafanyakazi wa Benki ya KCB kufanya ziara katika hospitali hiyo mara baada ya kumaliza kutoa msaada wa vifaa mbalimbali kwenye hospitali hiyo.

Hospitali ya Wazazi ya Mwemberadu mjini Zanzibar, leo imepata msaada wa mashine ya kupumulia Wagonjwa mahututi, mashuka na vyandarua vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 kutoka Benki ya KBC Tanzania.

Akipokea msaada huo, kwa niaba ya Waziri wa Afya, Katibu wa Hospitali Kuu ya Zanzibar ya Mnazi Mmoja Bw. Omari Abdallah, amesema kuwa msaada huo utaiwezesha Hospitali hiyo kuweza kuwahudumia wagonjwa mbalimbali wakiwemo mama wajawazito na watoto wachanga wanaozaliwa kwenye Hospitali hiyo.

Hata hivyo Bw. Omar ametoa wito kwa makampuni mengine zikiwemo taasisi za fedha hapa nchini, kuendelea kutoa misaada ya hali na mali katika Hospitali na Zahanati ili ziweze kuboresha huduma kwa wagonjwa.

Awali akikabidhi Msaada huo, Meneja wa Benk ya KCB Tawi la Ston Town mjini Zanzibar Bw. Rajab Ramia, amesema benki yake imetoa misaada kama kwa Hospitali ya Mwananyamala na kusaidia madawati katika shule mbalimbali za Msingi za zanzibar na Dar es Salaam.

Wakati wa hafla hiyo, wafanyakazi wa Benki ya KCB wakiongozwa na Meneja Uhusiano wa Benki hiyo, Bw. Said Amour na Mneja wa Biashara Bw. Abdul Mshangama, walitoa zawadi mbalimbali kwa akina mama wajawazito na waliojifungua kwenye hospitali hiyo.

Na Mohammed Mhina, Zanzibar

CHADEMA WAVURUNDA KWA AIBU LONDON.



Chama Cha Demokrasia na Maendeleo jana kilipata AIBU kubwa hapa jijini London baada ya Watanzania kuzira kuhudhiria mkutano wao uliofanya katika Bar imilikiwayo na Wakenya ya The Thatched House.

Sababu nyingi zilizotajwa ni pamoja na urafiki mkubwa na kukubali kila sera ya Chama Tawala cha Uingereza cha Conservative ambacho kinachukiwa na Waingereza wenyewe kwa sera za kulazimisha zilizoleta hali mbaya ya maisha na umaskini nchini hapa. Aidha ni Chama kilichoilazimisha serikali kuwabagua na kuwafukuza Watanzania wengi waliokuwa wakiishi Uingereza na kuwarudisha Tanzania kwa Aibu kubwa huku wakiacha mali zao nyuma.

Maandalizi ya mkutano wa Chadema pia yaliwachefua Watanzania wengi na kukataa kushiriki kwa kuwa yalichangiwa na kufanywa na baadhi ya watu wenye kudhaniwa kwa muda mrefu kuhusudu tabia za USHOGA na USAGAJI wakati ambapo Watanzania wengi hawajapona kidonda kilichotibiwa kwa mabavu na serikali ya CCM wakati iliposhinikizwa kukumbatia utamaduni wa USHOGA na serikali ya Conservative au isahau misaada ya maendeleo ya kitaifa. Chadema katu haikupinga shinikizo hili la rafiki zao Conservative.

Aidha waandaaji wakuu wa mkutano huo iliwajumuisha wakurugenzi wakuu wa SERENGETI FREIGHT, kampuni inayojishughulisha na usafirishaji wa mizigo kwenda Tanzania na kwingineko. Kampuni ya Serengeti imekuwa ikilaumiwa na kushutumiwa sana siku hizi kwa kutokusema ukweli kwa Watanzania kuhusu muda, gharama za ghafla na uhakika wa usafirishaji wa mizigo ya Watanzania ambao wengi wameishia kulipa gharama kubwa za ziada, ucheleweshwaji au kuamua kuacha mizigo dhidi ya muda uliokubalika. Kuhusika kwa Wakurugenzi hawa kuliongeza uchungu kwenye kidonda kibichi.

Baadhi ya Watanzania waliokuwa wakijiburudisha ndani ya Bar hiyo na kuangalia mashindano ya Olyimpic walimrushia Bw. Lema maswali ya kebehi na kumzomea pia na kusema.... “Gwanda linanuka RUSHWA meku”....huku wengine wakitoa kadi zao za CCM na kunyanyua juu.

Katika mahudhurio hayo machache,idadi kubwa walikua ni wanaCCM waliohudhuria kwa makusudi na wengine kuchangia kwenye mkutano huo. Baada ya mkutano vicheko vya kebehi vilisikika na kuambatana na kauli kama “...jamaa wanabwabwaja tu hawawezi hata kujenga hoja...wanafikiri hapa ni walipotoka..ovyoo.”

Ikitarajia kufuata nyayo za CCM UK itabidi Chadema waombe miujiza ya aina yake kupata w/chama na si washabiki tu katika maeneo tofauti ya UK ili itoke kwenye sura ya Kijikundi. CCM UK ilifanikiwa kufungua mashina katika miji/majiji kumi hapa UK.

Magazeti ya leo Alhamis 9th August 2012