Wednesday, October 22, 2014

Chanjo ya Ebola Kutolewa Afrika Magharibi

Shirika la afya duniani, WHO limearifu kuwa liko mbioni kufanya majaribio ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ambao umeripotiwa kuua takribani watu 4,500 huku nchi za Afrika Magharibi zikiripotiwa kuathirika zaidi tangu kulipuka kwa ugonjwa huo.

Taarifa iliyoripotiwa na CNN imesema kuwa shirika hilo limepanga kuanza utekelezaji wa jaribio hilo mapema Januari mwaka 2015 katika nchi za Afrika Magharibi, huku wakisisitiza kuwa chanjo zote hazina madhara kwa afya ya binadamu, japo chanjo hiyo haitowahusu wagonjwa ambao tayari wana maambukizi Ebola.

Mratibu wa zoezi hilo Dk. Marie Paule Kieny amesema, chanjo hiyo itatolewa kwa mtu yoyote atakayekuwa tayari kujitolea kushiriki.

Amezitaja nchi za Mali, Uingereza na Marekani kuwa ni baadhi ya nchi ambazo jaribio la chanjo hiyo litafanyika.

Shirika la afya limesema limeagiza wataalamu kufanya ziara Afrika Magharibi katika nchi ambazo wananchi wake wameathirika zaidi na ugonjwa huo, ambapo pia ziara hiyo itahusisha pia zoezi la ukaguzi wa vituo ambavyo vitatumika kutolea huduma hiyo ya chanjo.

Iwapo chanjo hii itafanikiwa itafufua matumaini kwa watu wa Afrika ya Magharibi ambao wameshuhudia athari kubwa zilizosababishwa na Ebola ambapo watu zaidi ya 4,500 wameripotiwa kufariki na wengine zaidi ya 9,000 wana maambukizi ya ugonjwa huo.

Bilionea wa Madini Arusha auwawa leo So sad jamani

Jamani samahani kwa picha hii ila ndio hali halisi polisi jamani mtandao wa majambazi bado unaendelea kutishia usalama wa wananchi jijini arusha.Poleni wafiwa na wana Arusha secta ya madini. P.I.P Fadhili

Mti uliofufuka huko Tabora haya ni maajabu jamani ?




 
Jamani haya ni maajabu hii imetokea mkoani Tabora mti ulioanguka miaka mitatu iliyopita umesimama huku wanyeji wakisema ulikuwa ukipiga kelele sasa najiuliza ni muujiza wa mungu au nguvu za giza mbona hii ni ajabu jamani mlioko huko tupeni habari kamili.

Tuesday, October 21, 2014

Unaikumbuka Hii....( HATIMAE LUDOVICK AFUNGUKA AELEZEA UHUSIANO WAKE NA LWAKATARE NA MWIGULA)

*Aelezea uhusiano wake na Mwigulu, Lwakatare

*Asema yeye bado ni mwanachama hai wa Chadema, amkwepa Kibanda
SIKU chache baada ya Mahakama kumuachia kwa dhamana mshitakiwa mwenza wa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, Joseph Ludovick, amefunguka na kuelezea tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake, ikiwamo uhusiano wake na Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba.

Ludovick, ambaye anadaiwa kurubuniwa na Nchemba na hivyo kumrekodi Lwakatare wakipanga mipango ya kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaky, alijitokeza juzi katika mtandao wa kijamii wa Mabadiliko na kuomba kuulizwa jambo lolote, kwa kile kilichoonekana kutaka kujibu tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake.

Maswali na majibu yake ilikuwa ni kama ifuatavyo;

Asante Mungu u Mwema


 Nakupenda  baby wangu mungu akupe maisha marefu na afya njema Happy birthday my Precious 1yrs old Asante mungu

Thursday, October 9, 2014

Hongera my pacha

Mungu awalinde awajalie upendo na uvumilivu hakika mmependeza sana

Hahahah

Pendeza sisi chezea posiiii duu naanza mazoezi kwa kweli ufupi umezidi sasa hahahahahahahaaa

Hi wapenzi wa Tanzania asilialive.blogspot .com

Habari za siku nyingi wapenzi wa tanzania asilialive kutokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wetu tunaomba radhi kutokuwepo hewani kwa muda mrefu.kwa sasa tunajaribu kurekebisha na punde tutakuwa hewani kuendeleza libeneke hili.

Asanteni sana by  faulisa