Thursday, September 13, 2012

TAARIFA KUTOKA MITANDAO YA KIJAMII ZINAPASHA KUWA DR. DALALY KAFUMU AMEPATA AJALI

Dr. Dalaly Kafumu amepata ajali ya kupinduka na gari akielekea kwenye kijiji kimoja kilichopo kata ya Mwisi ambako alikuwa anaelekea kushiriki mazishi ya Mama mmoja maarufu. Ajali hiyo ilitokea jana ambapo gari ilipoteza uelekeo kutokana na hitilafu ya barabara na hivyo kuvutwa, kugonga gema na kupinduka mara moja na gari kukaa matairi juu.

Gari iko nyang’anyang’a huwezi amini kama kuna mtu ametoka salama, lakini tunavyoongea hapa Dr. Kafumu na kijana wake ambaye alikuwa akiendesha walitoka salama. Dk. Alibanwa na Airbags na walilazimika ili kumtoa kuvunja vyuma kwa shoka na kumkuta amezimia na alizinduka baada ya muda kidogo, pia alikuwa na bruises zilizokuwa zinavuja damu sana kichwani na alilazwa hospitali ya Nkinga na asubuhi hii atapewa ruhusa arudi nyumbani.   

Amekuwa jimboni humo toka Jumatatu akifanya ziara ya kukamilisha miradi ya maendeleo aliyoianzisha, pia kuwaondoa mashaka wananchi kuwa hatowatelekeza kwa kuwa ametolewa Ubunge, na kwamba bado yuko nao pamoja tu.

Taarifa hizi hazijathibitishwa na bado tunaendelea kutafuta mawasiliano na kamanda wa polisi mkoani Tabora ili kupata ukweli wa tukio hilo

Serengeti FIESTA 2012 - Bongo Movie Stars (Wema Sepetu, JB, Ray Kigosi, Auntie Ezekiel & Nyerere)


Magazeti ya Leo Alhamisi 13th September 2012


































ASKARI MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MWANDISHI ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI IRINGA.

              wakati wote alikua amefichwa hivi hivyo hata sura haikuonekana kwenye picha yoyote.
                                            Hili ndio gari lililombeba mtuhumiwa.
Kamanda wa polisi Iringa Michael Kamuhanda amethibitisha kwamba askari polisi ambae anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kukusudia ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi amefikishwa mahakamani Iringa september 12 2012.

Askari mwenyewe ni mwenye namba G2573 na jina lake ni Pasificus Cleophace Simoni mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa FFU Iringa.

Mbele ya Hakimu Mkuu Mwandamizi wa mahakama ya hakimu Mfawidhi ya Wilaya Dyness Lyimo mtuhumumiwa hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haiwezi kusikiliza kesi za mauaji.

Kwenye kesi za jinai sheria kifungu cha 196 iliyofanyiwa marejeo 2002 inakatazwa mtuhumiwa wa mauaji ya kukusudia kupewa dhamana ambapo mtuhumiwa amerudishwa mahabusu kutokana na kesi yake kukosa dhamana kisheria na kesi hiyo imeahirishwa hadi 26 Septemba mwaka huu itakapotajwa tena.

Kamanda Michael Kamuhanda amesema “ni kosa kama makosa mengine huwa yanatokea katika kazi, uchunguzi umekamilika na mtuhumiwa amefikishwa Mahakamani”

(picha zote zimepigwa na Francis Godwin)