Wednesday, October 17, 2012

Hali ilivyo mjini Zanzibar,

  Picha na Maktaba Barabara ya Darajani Visiwani Zanzibar. Askari wa kutuliza ghasia wameshaanza kurusha mabomu ya machozi kutawanya kundi la uamsho ambao wapo Barabara ya Darajani wanachoma matairi na kurusha mawe kwa askari. Fujo hizo zimetokana na kukamatwa kwa kiongozi wa Uamsho Sheikh Farid.


Huyu ndiye Kiongozi wa Kundi linaloitwa UAMSHO la Zanzibar Sheikh Farid aliyekamatwa huko Visiwani Zanzibar. Kundi hilo shughuli zake ni za mihadhara ya Kidini hasa ya Kiislam.

Yaliyojiri siku ya Jumamosi 13th October katika uwanja wa sheikh abd amani karume katika maombi ya kuombea taifa la tanzania na kukombolewa



                      Hizi picha ni za jumamosi asubuhi wakati watu wakisubiri maombi kuanza
                                                                     Umati wa watu





Wakati wakristo wakiombea Tanzania yetu hivi sasa udini umetawala kila kona makanisa yanachomwa watu wanaumizwa tunapoteza mali zetu. hivi sasa hali si nzuri Zanzibar na Dar es Saalam maandamano na fujo zinaendelea.

Upako wa Ngurumu atua Arusha mjini na Helkopta

                                                                         Msafara
                                                              Huu ndio msafara wake

                                helkopta iliyomleta upako wa ngurumu

RAIS SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI ALIOWATEUA KARIBUNI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akimuapisha Bi Shawana Bukheti Hassan kuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiekuwa na Wizara Maalum katika hafla iliofanyika Ikulu Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohd Shein akiwa katika Picha ya Pamoja na Mawaziri na Manaibu Makatibu wakuu aliowaapisha leo Ikulu Mjini Zanzibar.


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu Makatibu Wakuu aliowateua hivi karibuni

 Walioapishwa ni Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiyekuwa na Waizara maalum Shawana Bukheti Hassan,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mohamed Said na Naibu Waziri wa Kilimo na Mali Asili Mtumwa Kheir Mbaraka

Wengine walioapishwa na Dkt.Shein ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Taahir Mohamed Khamis,Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Mustafa Aboud Jumbe.

 Pia aliwaapisha Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais Fedha,Uchumi na Mipango ya Maendeleo Juma Ameir na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anayeshighulikia Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar CDR Julius Nalimy Maziku.

 Miongoni mwa viongozi ambao walitarajiwa kuapishwa leo na hawakuwepo ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,Makazi,Maji na Nishati Ali Khalil Mirza na Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Dkt Juma Malik Akili

 Shuguli hiyo ambayo ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar ilihudhuriwa na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad,Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd,Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho, Mawaziri mbalimbali,Washauri wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Khamis Haji,Maofisa wa ngazi mbalimbali za Serikali, pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vikosi vya SMZ.


Na Maelezo Zanzibar

Sheikh Farid wa Uamsho 'atekwa nyara' visiwani Zanzibar



Habari zilizogaaa kila kona sasa hivi unguja kuwa Sheikh Farid wa Uamsho ametekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa hajulikani yuko wapi.

Mengi tuthabarishana. Ila kwa sasa hali ni tee maana watu washaqnza kujikusanya kila pahala.

Uhalisia wa kinachoendelea kama ifuatavyo:

    - Kwa mujibu wa Katibu wake, Abdallah Said Ally, amesema alikuwa na dereva wake maeneo ya Michenzani akitokea nyumbani kwake Mbuyuni, ndipo akakutana na gari moja ambalo dereva halifahamu na akashuka mwenyewe kwenye gari lake na kuingia katika hilo gari na kuanzia hapo hadi sasa hajulikani alipo.
    - Katibu huyo wa Uamsho na wenzake wamekuwa katika juhudi za kutuliza jazba za wafuasi wao na sasa wanawasiliana na polisi kujua alipo kiongozi wao.
    - Sheikh Farid 'amepotea' muda ule ule ambao inadaiwa mwenzake (Sheikh Ponda) alikamatwa (saa 5 usiku wa kuamkia leo). Juu ya sakata la Sheikh Ponda fuatilia - Sheikh Ponda akamatwa Dar!
    - Hata hivyo, wananchi wa hapa Zanzibar wanasema polisi, UAMSHO na serikali wangesubiri wanafunzi wamalize mitihani ya Form 4 kabla ya wao kuanza malumbano yao!

Chanzo Jamiiforum.

Wenje Apokea Wanachama Wapya Wa CHADEMA London

                                                           Kamanda ndibalema akipokea kadi
 CHADEMA UK ilipata wanachama wapya na picha ni ni mwanachama mpya kipokea kadi yake. Mwanachama mpya wa CHADEMA UK akipeana mkono na Mh. Ezekiel Wenje
                                                               mkutano unaendelea
                                                              Picha ya chini ni meza kuu
Makamanda wakiwa katika picha ya pamoja

Ulimboka Kutaja Wabaya Wake ...!

KIONGOZI wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka, amepanga kumwaga taarifa nyeti kuhusu kutekwa na kuteswa kwake na kisha kutupwa katika Msitu wa Mabwepande, Bunju, jijini Dar es Salaam.

 Mmoja wa ndugu na rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka, ameliambia Mwananchi kuwa, kiongozi huyo wa jumuiya, amepanga kuanika hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari. Alisema Dk Ulimboka, atatumia mkutano huo kueleza siri ya kutekwa kwake.

 “Siku yoyote kuanzia sasa umma, utafahamu ukweli halisi wa kilichompata kijana wetu. Niliongea naye juzi na amenithibitishia kuwa atakutana na waandishi wa habari na kueleza kila kitu katika masahiba yaliompata,” alisema ndugu huyo wa Ulimboka ambaye hata hivyo, hakutaka jina lake litajwe gazetini.

Alisisitiza “Ni kweli kwamba Steven (Dk. Steven Ulimboka) amepanga kukutana na waandishi wa habari. Anataka kutumia mkutano huo, kuanika wote walioshiriki kumtesa, kumteka na kisha kumtupa katika msitu wa Mabwepande,” Alipoulizwa kuhusu kipya ambacho daktari huyo ataueleleza ulimwengu ambacho hakijafahamika, mwanafamilia huyo alisema:

“Tuvute subira. Steven amepanga kutaja wote waliohusika katika kutaka kuangamiza maisha yake. Ameniambia kuwa anataka kuwaambia Watanzania ukweli wa kilichompata,” Dk Ulimboka alitekwa usiku wa Juni 26 mwaka huu, katika maeneo ya Leaders Club jijini Dar es Salaam na baadaye kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikononi na miguuni kabla ya kunyofolewa kucha na meno; katika Msitu wa Mabwepande.

Aliokotwa na wasamaria wema asubuhi yake na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alilazwa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini Juni 30 kwa matibabu zaidi. Tangu aliporejea nchini Agosti 12 mwaka huu, kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka ndani na nje ya nchi, kumtaka azungumze kwa madai kuwa kauli yake itasaidia kujulikana kwa ukweli kuhusu kilichompata. Kufanyika kwa mkutano huo kunatajwa na wachambuzi wa mambo kuwa kunaweza kuondoa kiwingu hicho, ikiwa ni pamoja na kujibu baadhi ya maswali yaliyobuka juu ya tukio hilo.

mahojiano yake ya kwanza na gazeti hili, wiki iliyopita, Dk. Ulimboka alisema hali yake inaendelea kuimarika siku hadi siku na kwamba anamshukuru Mungu na wote waliomuombea, ingawa bado anahitaji matibabu zaidi.

“Madaktari wangu bado wanaendelea na uchunguzi kuhusu figo zangu ili waone kama zinaweza kufanya kazi au zinahitaji kuondolewa na kuwekwa nyingine. Lakini kwa jumla, hali yangu inaleta matumaini kidogo.

Chanzo:www.mwananchi.co.tz

Breaking News Fujo Zanzibar kutokana na kiongozi wa uamsh

Habari zilizotufikia hivi sasa vurugu kubwa zinaendelea maeneo ya darajani mjini Zanzibar habari zinaeleza kuwa kiongozi wa uamsho ametekwa hivyo wafuasi wake ndio wanafanya fujo. tunaendelea kuwaletea habari kamili hapa hapa Tanzania Asilialive


Magazeti ya leo Jumatano 17th October 2012