Monday, October 22, 2012

Jukumu langu na lako Kuilinda Amani yetu.


JK Akutana Na Ujumbe Wa Kenya Ikulu

 Rais JAkaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya.
Wengine ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012
 Rais JAkaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na  Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. Kulia kwake  Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA. Kushoto kwa Rais ni 
Wengine ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012
Rais JAkaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA, Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya, Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu (kulia), Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda (kushoto) na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli alipokutana na ujumbe huo Ikulu jijini Dar es salaam Jumapili Oktoba 21, 2012

PICHA NA IKULU

JK Akutana Na Ujumbe Kutoka Kenya


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaka wananchi wa Kenya wapewe nafasi ya kuamua ni viongozi gani wanawataka katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Machi mwakani. Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kenya wanayo haki ya msingi kabisa kuamua hatma ya taifa lao katika Uchaguzi Mkuu huo.

Mheshimiwa Rais aliyasema hayo jana Oktoba 21, 2012 alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya nchini Kenya uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam.

Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha TNA na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya.

Wote wawili ni wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao. Wengine katika msafara huo walikuwa ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu, Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli. Rais Kikwete aliwapongeza kwa kuamua kufanya kazi kwa pamoja licha ya kuwa watakuwa washindani katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu huo.

Mheshimiwa Rais ameitakia heri nchi ya Kenya katika uchaguzi huo ujao, na kusisitiza kwamba nchi hiyo ya jirani ina umuhimu katika mustakabali wa kiuchumi kwa nchi za Afrika Mashariki. Rais Kikwete wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alikuwa miongoni mwa viongozi walioshughulika sana kutafuta ufumbuzi wa ghasia na vurugu zilizozuka kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Rais Kikwete alikaa siku tatu nchini Kenya akitafuta usuluhishi wa vurugu hiyo ya kisiasa nchini humo, ambayo katika mazungumzo yake leo ameyataja kama ajali iliyolipata Taifa la Kenya, na ambayo majirani wake hawaitarajii kutokea katika uchaguzi ujao.


Imetolewa na:

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS DAR ES SALAAM,

21 Oktoba, 2012

Tanzania Asilialive yawaomba Radhi kwa kutokuwepo kwa muda.


Tanzania Asilialive yawataka radhi wapenzi wetu wote kwa kutokuwepo na kuwahabarisha habari ila kwa sasa tumerudi kwa kasi mpya. Nawakaribisha tuendelee kuelimishana na kujenga Taifa letu.

Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa awataka Waislam, Wakristo Kuungana

WAZIRI Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, amewataka waumini wa madhehebu yote nchini kuonyesha mshikamano katika ujenzi wa shule nchini bila kujali shule inayojengwa ni ya Wakristo au Waislam.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alitoa kauli hiyo jana wilayani Mwanga katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Kiislamu ya Lambo iliyopo kata ya Shighatini. 

Lowassa alitumia fursa hiyo kusema kuwa Wilaya ya Mwanga ni ngome ya Chama cha Mapinduzi (CCM), na kwamba kwa kusema hivyo hakipigii debe chama chake bali huo ndio ukweli.

Katika tamasha la harambee hiyo iliyohudhuriwa pia na Mbunge wa Mwanga, Profesa Jumanne Maghembe, Masheikh na Wachungaji wa madhehebu mbalimbali, Lowassa alichangia Sh10 milioni.

“Mwanga ni nguzo yetu ya CCM na wala hili sio jambo la siri…Namfahamu Profesa Maghembe, katika kura hapa hamkukosea hili ni jembe…ni kiongozi hodari na mchapa kazi,” alisema Lowassa.

Lowassa ambaye anatajwa kuw amiongoni mwa watakaoingia katika kinyang’anyiro cha kugombea Urais mwaka 2015, alimpongeza Profesa Maghembe pamoja na mtangulizi wake, Waziri Mkuu mstaafu, Cleopa Msuya kuwa wana mipango mizuri ya maendeleo.

Akizungumzia kujitoa kwake kuchangia shughuli za kijamii, Lowassa alisema japokuwa ana mialiko mingi lakini suala la kuitwa Mwanga kuchangia ujenzi wa sekondari limemfurahisha sana.

“Watu huwa wanaogopa kuchangia lakini ni lazima wanadamu wafahamu kuwa vyote vilivyomo duniani ni vya mwenyezi Mungu…tushikamane wakristo na waislamu tujenge shule,” alisema.

Lowassa alisema suala la ujenzi wa shule za msingi na sekondari ni jambo linalopaswa kupewa kipaumbele na Watanzania akisema wanaodai elimu ni ghali basi wajaribu ujinga.

“Kuna maneno yanasemwa kuwa Waislamu huwa hawajengi shule bali wanajenga misikiti mikubwa lakini nyinyi hapa hapa Mwanga mmefuta dhana hiyo na ni mfano wa kuigwa,” alisema. 

Awali, Profesa Maghembe alisema amezunguka kwa marafiki zake ambao walichangia Sh25 milioni kabla ya jana, na kabla ya kuanza harambee alikuwa amepata michango mingine ya Sh19.5 milioni.


Katika harambee hiyo, Profesa Maghembe alichangia Sh3 milioni wakati mfanyabiashara Seleman Mfinanga akichangia Sh1 milioni na hadi mchana bado harambee hiyo ilikuwa ikiendelea.

Akisoma risala kwa Lowassa, mjumbe wa Halmashauri ya Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata), linalomiki shule hiyo, Sadik Ramadhan, alisema shule hiyo itagharimu Sh2 bilioni hadi kukamilika. Alifafanua kuwa harambee ya jana ililenga kukusanya Sh255 milioni kwa ajili ya kujenga jengo la utawala, maabara na mabweni mawili lakini kwa siku ya jana zilihitajika Sh150 milioni. 

Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Magazeti ya leo Jumatatu 22nd October 2012

Happy Birthday Baby Kamila





                                                             Baby Girl wetu akisubiri kukata keki

                                                                    Wahooooo Kamila
                                                                    Nice one



                                                            Kamilia akimlisha criss keki
                                                                          Dad thanks
                                                    Mum kula keki 2yrs si mchezo jamani
                                                     duuuu keki tamu hiyooo thanks kamila
                                             Mama wa asilialive apitwe noooo haiwezekani
                                            Kamila akimbusu mdogo wake wahooo nice

                                                  Amina mdogo wangu kula keki heeee
                                                          Ashuya kula keki dada yangu
                                                                 kula keki