Wednesday, May 8, 2013

Magazeti ya leo Jumatano ya 8th May 2013



BAADHI YA PICHA ZA JANA RAIS KIKWETE NA MAMA SALIMA WALITEMBELEA MAJERUHI wa BOMU HOSPITALI YA MOUNT MERU ARUSHA


                                                                          Pole Baby Utapona

MAHAKAMA YAFUTA KESI YA UGAIDI ILIYOKUWA INAMKABILI LWAKATARE

Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

Taarifa zaidi zinasema ni shangwe kuu kutoka kwa wafuasi wa Chadema walioko mahakamani na Familia ya Lwakatare.Baadhi ya wafuasi wa Chadema waliohojiwa wamesema huu ni ushindi mkubwa dhidi ya udhalimu.

Katika kesi hii Lwakatare anawakilishwa na Jopo la mawakili nguli watano ambao ni Mabere Marando,Tundu Lissu,Professor Abdallah Safari, Peter Kibatala na Naronyo Kicheere.

HATIMA YA ZOMBE NA LWAKATARE NI LEO

Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare. 

MAHAKAMA ya Rufaa nchini leo inatarajia kutoa uamuzi rufaa iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Dk. Eliezer Feleshi, dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi, Abdallah Zombe, wa kuifuta au kutoifuta rufaa iliyokatwa na DPP baada ya jicho la mahakama kuona hati ya kukatia rufaa ina dosari.

Sambamba na hilo, pia Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajia kutoa uamuzi wa kuifuta au kutoifuta kesi ya tuhuma za ugaidi za kutaka kumteka mhariri wa gazeti la Mwananchi, Denis Msaki, inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph

RAIS KIKWETE AKIWA ARUSHA KUHANI MISIBA YA WALIOFARIKI KATIKA MLIPUKO WA BOMU KANISANI


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete wakishiriki dua ya pamoja, wakati walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7, 2013.



 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mke wake Mama Salma Kikwete walipomtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo la Arusha la Kanisa Katoliki jijini Arusha Muadhama Josephat Lebulu katika makazi yake rasmi kutoa pole kwa shambulio la kigaidi katika Kanisa la Mtakatifu Joseph, Parokia ya Olasiti ambako alikutana pia na Maaskofu wa Makanisa mbalimbali waliokuwa hapo Mei 7,          

MSISITIZO WA KADINALI PENGO ALIOUTOA TENA JANA

 Kadinali Pengo

“Jana (juzi), niliongelea kwamba suala zima la tukio la Arusha halihusiani na imani yoyote ya kidini. Tamko hilo nilitamka kutokana na taarifa nilizofikishiwa na watu ambao sikuweza kuwa na shaka kwamba wanaoniambia ni kweli na sidhani kama ningekuwa na sababu ya kusema wamefika kwa kunidanganya kwa hiyo tamko litakuwa limesimama juu ya msimamo huo,” alisema Kadinali Pengo na kuongeza:

“Lengo la msingi kabisa, langu na la kanisa ni kwamba tukio lolote lile liwe kwa nia mbaya au nzuri kwa upande wetu isiwe ni sababu ya kuanza mapambano na kuwa chimbuko la ukosefu wa amani katika nchi yetu,” alisema Pengo.

Alisema kuwa kila anayehusika ajue amani ya kweli ya taifa lolote haiwezi ikapatikana isipokuwa ikijengwa juu ya ukweli na ukweli kabisa bila kufuta au kujaribu kupotosha ukweli kwa namna yoyote ile.

“Tusipojua kusema ukweli ulivyo hatuwezi kufaulu kuleta amani katika taifa letu. Kwa hiyo pamoja na kuendelea kuwaomba waumini wa Katoliki pamoja na watu wenye mapenzi mema kuendelea kumwomba Mwenyezi Mungu arehemu taifa letu na mapambano ya aina yoyote ile. Tuendeleze nia yetu njema ya kusema ukweli, haidhuru ukweli huu unamgusa nani,” alisema Pengo.

BALOZI WA VATICAN ALIYENUSURIKA KATIKA SHAMBULIZI LA BOMU ARUHUSIWA KUONDOKA ARUSHA

Mwakilishi wa Papa akiwa na Askofu Lebulu akitoka kwenye VIP ya Arusha Airport kuelekea kwenye ndege ya Precision .
 Ilikuwa ni dakika za majonzi na masikitiko kwa kundi lote lililokuwa limemsindikiza uwanja wa ndege Balozi wa Papa ambaye ameondoka leo mjini Arusha kuelekea Dar, baada ya kunusurika katika shambulio la bomu lililorushwa wakati akiwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kanisa la Mt. Joseph Mfanyakazi huko Olasiti Arusha.

Hapa akisaidiwa na wafanyakazi wa Precision kukamilisha dokomenti zake za Usafiri, huku ulinzi ukiwa umeimarishwa
 Kwaheri Mtumishi wa Mungu, tunaomba uje tena tutakapoamua kuzindua upya Parokia Yetu ya Yosefu Mfanyakazi- Olasiti Arusha.

KINANA AJISAFICHA DHIDI YA TUHUMA ZA UJANGILI......AWATAJA WALIOHUSIKA NA SHEHENA YA PEMBE ZA NDOVU

 Katibu Mkuu wa CCM ndg Abdulrahman Kinana amesema kinga ya Bunge isiwe sababu ya baadhi ya wabunge kutumia fursa hiyo kuchafua watu wasio na nafasi ya kujitetea ndani ya mhimili huo wa Dola.

Amehadharisha hayo alipozungumza na waandishi wa habari  mjini Dodoma juzi kukanusha tuhuma zilizoelekezwa kwake binafsi na chama chake na Kambi ya Upinzani Bungeni.

Tuhuma hizo zilihusu shehena ya pembe za ndovu iliyokamatwa Vietnam mwaka 2009 ambazo aliziita za kupika na za uongo. "Tuhuma hizo hazina ukweli wowote, zina nia mbaya dhidi yangu na zimelenga kuniharibia taswira yangu na ya chama changu," alisema Kinana.

Alisema hahusiki vyovyote na tuhuma hizo na kutuhumu Kambi ya Upinzani Bungeni kwa kushindwa kujadili hoja za maana za maendeleo na badala yake kujihusisha na siasa za kuchafua heshima za watu.

MUSWADA WA KUZUIA MAANDAMANO NCHINI WAANDALIWA

 Katika hali ya kushtusha Waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Nchimbi aliliambia bunge jana  jioni  kwamba serikali  imeridhia kuleta mswada bungeni ili itungwe sheria ya kuzuia maandamano kote nchini.

Waziri Nchimbi alisema kuwa  hiyo ndiyo njia pekee ya kuondoa uvunjifu wa amani nchini unaofanywa na watu wasiolitakia mema Taifa....Alisema mswada huo utaletwa wakati wowote kuanzia sasa akimaanisha tayari umeshakamilika.Nchimbi alikuwa akishangiliwa sana na wabunge wa CCM wakati alipokuwa akitamka maneno hayo Huenda  azimio hili litakuwa ni pigo kubwa kwa demokrasia katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.Ikumbukwe ni hapo juzi  tu Chadema kilidai kunasa mpango wa siri wa serikali  wa kuzuia maandamano na mikutano ya hadhara ili kudhibiti wapinzani kuiimarisha CCM.

Credit: JF 

WABUNGE WAANZA KUJIHAMI NA MILIPUKO YA MABOMU....WAMEOMBA ULINZI UIMARISHWE BUNGENI

MBUNGE  wa Jimbo la Simve kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Richard Ndasa amemuomba Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda kuhakikisha usalama wa Bunge unaimarishwa.

Ndasa aliyasema hayo wakati akichangia hoja katika Bajeti ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kusema kuwa tukio la juzi Mjini Arusha kwa Bomu kurushwa katika sherehe za uzinduzi wa jingo la Kanisa Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasit mjini Arusha na kupelekea vifo vya watu wawili na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa vibaya.

“Mheshimiwa Spika, naomba usalama Bungeni uimarishwe na katika jingo la Bunge maana hofu ya kushambuliwa Bunge hili inaweza kutokea enbdapo ulinzi utakuwa hafifu,” alisema Ndasa.

Ndasa alitolea mfano eneo la nyuma la Bunge hilo kuwa halina ulinzi wa kutosha hivyo ni rahisi mtu kusogea jirani na kufanya uhalifu nakuleta madhara makubwa kwa taifa.

Wabunge leo wanaendelea kuchangia Hotuba ya Wizara ya Mambo ya Ndani huku kila anaesimama akilaani tukio hilo la Arusha.

JESHI LA TANZANIA LIMESHATUA CONGO.....WAASI WA M23 WAANZA KUHAHA KWA KUJIKOSHA KWA WANANCHI

Kwa mujibu wa mwandishi aliye na waasi  wa  m23, Diana Katabarwa kwenye Blog yake  anamnukuu kiongozi wa kisiasa wa M23  Mr. Bisimwa akiwambia wakazi wa North Kivu kuwa majeshi ya Tanzania na South Africa nimajeshi dhalimu yaliyo jaa rushwa na hayawezi kuibadili Congo....

Bisimwa anadai  kwamba  majeshi  ya  Tanzania  yamekuja kuiba mali na kumsaidia KABILA awatawale   hali  itakayosababisha   jeshi lake la FDLR na waasi wa MAI MAI wapewa nafasi ya kuwa pora mali zao na kuwabaka wake zao na watoto....

Mbali  na  hayo,  bwana Busimwa anadai kinyume na taarifa zilivyo , kikosi cha jeshi la Tanzania kikiwa na askari 450 kimesha ingia mashariki ya CONGO kwenye mji wa UVIRA SOUTH KIVU huku Kamanda wao (TPDF) akiwa mjini Goma.