Tuesday, March 26, 2013

CHADEMA WAPOKEA MSAADA WA MILIONI 400

 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea msaada wa fedha shilingi milioni 400 kutoka Chama cha Upinzani nchini Denmark cha Conservative People’s Party (CPP), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo vijana pamoja na Wanawake Viongozi wa chama hicho.

Akizungumza wakati wa kutiliana saini Mkataba wa utekelezaji wa Mradi huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK. WILBROAD SLAA amesema awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wanachama wake kupitia Baraza la Vijana la Chama hicho, (BAVICHA), pamoja na lile la Wanawake (BAWACHA), inatarajiwa kuanza Machi, mwaka huu.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Chama cha Conservative People’s Party (CPP), ROLF AAGAARD, anaelezea lengo la chama hicho kutoa msaada huo.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (CHADEMA), JOHN HECHE amesema msaada huo utawawezesha kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Baraza hilo katika mikoa mbalimbali nchini.

Chama cha Conservative People’s Party (CPP), kilianzishwa mwaka 1915 na kimekuwa madarakani kwa kipindi kirefu hadi kiliposhindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita nchini.

ALIYEMGONGA TRAFIKI ENEO LA BAMAGA AFIKISHWA MAHAKAMANI

                 Waandishi wa habari wakimpiga picha (Simbo) wakati akiingia mahakamani...

 Jackson  Simbo anayedaiwa kumgonga kwa gari marehemu trafiki Elikiza Nko wiki iliyopita maeneo ya Bamaga-Mwenge  jijini Dar ss Salaam amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya Wilaya ya Kinondoni.

Mshitakiwa huyo ameachiwa kwa dhamana hadi kesi hiyo itakapo tajwa tena Aprili 15 mwaka huu

HUU NDO UTAJIRI WA WEMA SEPETU.....

                                                       Wema akiwa na Mama yake
 Well, well, well! Hiki ni kitu ambacho kila mmoja anapenda kukifahamu. Wema Sepetu ni tajiri kiasi gani? Ni ngumu kusema exactly mrembo huyu ana shilingi ngapi benki, lakini mambo anayofanya yanatupa jibu la wazi kuwa, Wema ana mkwanja mrefu. So hebu tuangalie mangapi makubwa yaliyohusisha fedha nyingi aliyoyafanya kuanzia mwezi June, 2012.

WANAFUNZI 10,000 WALIOKATA RUFAA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE-2012 WAMEFELI TENA

    MATOKEO YA RUFAA CSEE 2012 AWAMU YA I
    MATOKEO YA RUFAA QT 2012 AWAMU YA I

Taarifa ifuatayo, inahusiana na rufaa hizo, imenukuliwa kutoka kwenye gazeti la NIPASHE

Wakati tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne mwaka 2012 ikiendelea na kazi, imebainika kuwa wanafunzi waliokata rufaa kutaka mitihani yao isahihishwe upya wamefeli zaidi baada ya kusahihishiwa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambazo zimethibitishwa na baadhi ya maofisa, wanafunzi waliokata rufaa wamefeli zaidi na hata walioongezewa alama matokeo hayakubadilisha madaraja waliyopata awali.

MWANAFUNZI UDSM AJINYONGA HADI KUFA

 Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa pili Kitivo cha Sheria, Joseph Bernadina (25), amejinyonga kwa kutumia kamba na kukutwa ameifunga juu ya mti, katika eneo la Yombo chuoni hapo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Utawala, Profesa Yunus Mgaya, alithibitisha  kutokea kwa tukio hilo na kwamba alipata taarifa hizo jana asubuhi.

Aliongeza kuwa Jumamosi iliyopita alipokea simu kutoka kituo cha polisi cha chuo hicho akielezwa kuwa kuna mwanafunzi alitishia kujiua, lakini aliwahishwa hospitali na kupatiwa ushauri kutoka kitengo maalum cha washauri wa chuoni hapo na kuruhusiwa Jumapili.

WABUNGE ZITTO KABWE NA AZAN WAMALIZA MAFUNZO YAO YA JKT KAMBI YA MGAMBO 835KJ LEO

                       Zitto Kabwe akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha chini
Zito akiwa shambani pamoja na Mbunge mwenzake  Iddi Azan, Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa kambi ya Mgambo 835KJ.

Mbunge wa Kigoma CHADEMA, Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo wakemaliza rasmi mafunzo yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 835KJ kilichopo Mkoani Tanga.

Aidha Zitto Kabwe amesema anafuraha iliyo pitiliza kumaliza mafunzo hayo na ameweka historia ya kubwa katika maisha yake hii leo. Anapasha zaidi katika wakati wa Zoezi la kulenga shabaha alifanikiwa kulenga risasi 3 akiwa amelala, 3 akiwa amepiga magoti na 1 akiwa amesimama.

CHETI ALICHOTUMIA NAIBU WAZIRI WA ELIMU KUOMBEA KAZI YA UALIMU NI CHA RAFIKI YAKE...

 Imebainika kuwa mmoja wa watu ambao Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo (pichani)anadaiwa kutumia jina lake kutafuta kazi ya ualimu katika Shule ya Sekondari ya Southern mkoani Mbeya ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu kishiriki cha elimu Mkwawa (Muce), kilichopo mkoani Iringa.
Mhadhiri huyo ni Dick Aron Mulungu ambaye alisoma na Mulugo katika Shule ya Sekondari ya Songea Wavulana kati ya 1994 na 1996 na alijiunga na shule hiyo baada ya kuhitimu kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kafule, ambayo iko mkoani Mbeya.

Taarifa zinaonyesha kuwa Mulungu alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kupata Shahada ya kwanza katika Elimu (BA Education) 2001 na baadaye alisoma na kupata Shahada ya Uzamili (MA Development studies ) 2007.
Alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi, mahojiano yalikuwa hivi:

MAHAKAMA YAAMURU MATOKEO YA URAIS KENYA YAHESABIWE UPYA KWA VITUO 22 KATI YA 33

Nairobi. Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya nchini Kenya imeagiza kuchunguzwa kwa fomu 34 za matokeo ya uchaguzi wa rais kutoka katika vituo vyote 34,400, vilivyotumika kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Machi 4, mwaka huu.

Kadhalika mahakama hiyo jana iliagiza kuhesabiwa upya kwa kura za urais katika vituo vya kupigia kura 22 kati ya elfu 33 vilivyolalamikiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Muungano wa Cord, Raila Odinga.
Katika malalamiko yake yaliyowasilishwa katika mahakama hiyo kupinga Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa urais katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Machi 4, Odinga alidai kuwa vituo hivyo 22 kura zilizopigwa zinazidi idadi ya wapigakura walioandikishwa.

Jamani Familia ya Sepetu Imebarikiwa Hawa Vimwana Wanne

                                                               WEMA SEPETU

 TUNNU SEPETU... YEYE NI MAMA WA MTOTO MMOJA.. ANAISHI NCHINI MAREKANI

 NURU SEPETU... NI MAMA WA WATOTO WATATU, MARRIED AND BASED IN DAR.


 SUNNA SEPETU: HUYU PIA ANAISHIA MAREKANI KWA KIPINDI KIREFU...








KIBONGO BONGO TUMEZOEA KUMUONA WEMA AKIMAKE HEADLINE BUT WENGI HAMJUI KAMA WEMA AMEZUNGUKWA NA DADA WATATU WALIOSIMAMA KIMAISHA NA WASIOENDA SPOTLIGHT...  LEO NAWAKUTANISHA NA WASICHANA WANNE WANAOKAMILISHA FAMILIA YA SEPETU.