Wednesday, May 29, 2013

Yaliyojiri leo Jumatano Magazetini 29th May 2013





"SITAKI KUSIKIA NYIMBO ZA NGWEA ZIKIPIGWA CLOUDS FM..WAO NDO WALIOMFANYA AANZE KUVUTA BANGI ILI KUONDOA MAWAZO"...P FUNK

 Muda mfupi uliopita djchoka amepokea simu kutoka kwa Producer mkongwe hapa bongo anayejulikana kwa jina la P Fuck Majani na kumuuomba aipokee msg hii hapa chini na kuwaomba watanzania walijue hili na baadae atatoa barua rasmi.



KIFO CHA NGWEA: LADY JAYDEE NAYE ASITISHA SHOW YAKE

 Mwanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya nchini, mwanadada Judith Wambura Maarufu kama Lady Jaydee ametangaza kuahirisha shughuli ya maadhimisho ya miaka 13 tangu aanze muziki iliyokuwa imapangwa kufanyika Ijumaa hii ya Mei 31, 2013 katika mgahawa wake wa Nyumbani Lounge kupisha msiba wa kifo cha msanii Albert Robert Mangweha aliyeripotiwa kufariki nchini Afrika Kusini jana.

Judith amesema hayo muda mfupi uliopita (saa 3:52 asubuhi) wakati akihojiwa katika kipindi cha Super Mix ya East Africa Radio na mtangazaji Zembwela.
 
Jaydee ameeeleza uamuzi wake wa kutitisha show hiyo kuwa unalenga kutoa nafasi kwa wafiwa wote na wadau wa tansnia ya muziki na wapenzi wa Mangwea kumaliza taratibu za kumsitiri kipenzi chao na kueleza kwamba tarehe nyingine ya shughuli hiyo itatangazwa baadae.

Tangu amekaribishwa studio, Judith Wambura alionekana kuwa na majonzi sana kiasi cha kushindwa kuongea mara kwa mara na kukatisha mazungumzo yake kutokana na kukabwa na kilio.

TAARIFA YA KIFAMILIA KUHUSU MAZISHI YA NGWEA NA JINSI MWILI HUO UTAKAVYOLETWA TANZANIA

Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbinga Songea kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Songea kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach.
 
Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.

Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu.

Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa.

Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa