Thursday, July 5, 2012

Bungeni ni full uhuni na ubabe


15 WATEULIWA KUCHEZESHA KOMBE LA KAGAME

Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeteua waamuzi 15 kuchezesha michuano ya Kombe la Kagame itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Julai 14-28 mwaka huu.

Waamuzi hao wanatakiwa kuwasili Dar es Salaam, Julai 11 mwaka huu kwa ajili ya vipimo vya afya na mtihani wa utimamu wa viungo utakaofanyika Julai 12 na 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya wakufunzi wa CECAFA.

Kwa upande wa waamuzi wa kati (centre referees) walioteuliwa ni Anthony Ogwayo (Kenya), Dennis Batte (Uganda), Israel Mujuni (Tanzania Bara), Issa Kagabo (Rwanda), Thierry Nkurunziza (Burundi), Farah Aden Ali (Djibouti) na Waziri Sheha (Zanzibar).

Waamuzi wasaidizi (assistant referees) ni Elias Kuloba (Kenya), Peter Sabatia (Kenya), Musa Balikoowa (Uganda), Hamis Changwalu (Tanzania Bara), Jesse Erasmo (Tanzania Bara), Simba Honore (Rwanda), Abdulahi Mahamoud (Djibouti) na Josephat Bulali (Zanzibar).

TWIGA BANCORP WATOA HUDUMA KAMILI ZA KIBENKI KATIKA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA SABASABA

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Twiga Bancorp ambao wapo kwa ajili ya kutoa huduma katika banda la Benki hiyo katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu Saba Saba wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya Banda lao linalotoa huduma kamili za Kibenki.

Afisa Masoko wa Twiga Bancorp Limited, Adelbert Archerd Tibikunda akiwa amekamatia tuzo ya Century International Gold Quality ERA waliyo ipata Genever kwa huduma bora .
Katika Banda la Twiga Bancorp wateja wanapata fursa ya kuweka fedha zao papo hapo baada ya kufanya mauzo ndani ya Saba Saba. Yanini utembee na fedha nyingi wakati Benki ya twiga ipo nawe pale ulipo.Fedha katika ATM ni kwa saa 24, siku 7 za  wiki, mwezi mzima na siku 360. Huduma hii katika banda la Twiga hafungwi mwaka mzima.Utoa huduma bora ndio nguzo na ngao ya Twiga Bancorp, pichani ni mteja akiwa na furaha wakati akizungumza na Afisa Mwandamizi  Mwendeshaji wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Lydia Matembel, alipotembelea banda lao katika viwanja vya Maonesho Saba Saba.
Ofisa wa Benki ya Twiga Bancorp Limited, Ernest Kikwasi, akitoa maelezo kwa wananchi  waliotembelea banda hilo jana juu ya akaunti maalum ya watoto. Twiga Bancorp ni miongoni mwa benki zinazoshiriki katika Maonesho ya 36 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu JK Nyerere barabara ya Kilwa huku wakitoa huduma kamili za kibenki.
 Mmteja wa Twiga Bancorp akitoka kupata huduma katika banda la Benki hiyo kwa furaha baada ya kufanikiwa kutimiza alichotaka kwa wakati.
Deidre Lorenz kukisaidia kituo cha watoto yatima cha Upendo cha Moshi

Balozi wa Heshima wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon katika jiji la mapesa la New York City (NYC) nchini Marekani ambaye pia ni mcheza sinema na mlimbwende maarufu kutoka jiji hilo linaloaminiwa kuwa kitovu cha pesa duniani, Mmarekani Deidre Lorenz ameahidi kukisadia kituo cha watoto yatima cha Upendo kilichopo katika Manispaa ya Moshi.

Lorenz alikitembelea kituo hicho siku mbili (tarehe 22 Juni) kabla ya kukimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon zilizotimua vumbi tarehe 24 juni mwaka huu kuanzia Moshi Club hadi Rau mudukani.

Mbio za Mt. Kilimanjaro Marathoni zilianzishwa na Marie Frances anayetoka katika jiji la matajiri la Bethesda nje kidogo ya jiji la Washingyon DC nchini Marekani mwaka 1991 baada ya kuombwa na balozi wa zamani nchini Misri.

Marie Frances aliyekuwa muandaaji wa vipindi vya television ya ABC alianzisha mbio za Pyramid Marathon zilizofana sana nchini Misri na kumfanya balozi wa Tanzania nchini Misri wakati ule kumuomba aje Tanzania kuanzisha mbio za marathon.

Mt. Kilimanjaro Marathon ilianzishwa mwaka 1991 katika Manispaa ya Moshi zikiwa ni mbio kukimbia kwa furaha (fun run) inayowaleta wazungu kupanda mlima Kilimanjaro, kukimbia na kwenda kutembelea mbuga zetu za wanyama. Mbio hizi zipo katika kiundi la Seven Continental Marathons ambazo hukimbiwa katika mabara saba ya dunia.

Deidre Lorenz ambaye amewahi kuigiza katika filamu nyingi alipatikana katika bahati nasibu (Raffle) iliyochezeshwa na Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 wakati wa mbio za New York Marathon jijini New York Marekani mwaka 2011. Katika bahati nasibu hiyo Deidre Lorenz aliibuka mshindi na kujipatia tiketi ya bure pamoja na gharama za hoteli za kuja kukimbia mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon mwaka huu.

Wadhamini wa mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon ni kampuni ya ndege ya Ethiopia Airlines (ET) ambayo huwa inantoa tiketi za bei rahisi kwa wale wanaokuja kukimbia mbio hizo. ET pia hugharamia ushiriki wa Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 katika mbio za New York Marathon, Boston Marathon na Los Angelos Marathon ili kijitangaza.

Katika mpango huo Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 huweka banda la kutangaza vivutio vya Tanzania kama vile mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, Zanzibar na mali zetu za asili.

Mkakati huu umesaidia sana kuitangaza Tanzania na hivyo kuwapa fursa watalii wengi kutoka Marekani na nchi nyingi duniani kuijua vyema Tanzania. Wengi wa wakimbiaji hawa hutembelea vivutio vya Tanzania baada ya kutembelea banda la Mt. Kilimanjaro Marathon 1991 katika mbio hizo.

Ufadhili wa Deidre Lorenz akishirikiana na taasisi ya Screen Actors Guild utakisaidia sana kituo cha watoto yatima cha Upendo ambacho kinakabiliwa na changamoto nyingi za fedha na vifaa vya kuwatunza watoto wanaolelewa kituoni hapo. Kituo hiki kilianzishwa miaka ya 60 na masista wa shirika la Precious Blood wa Kanisa Katoliki jimbo la Moshi.

Kwa miaka mingi kituo hiki kimekuwa kinapokea watoto wachanga wanaotelekezwa na mama zao baada ya kuzaliwa katika hospitali mbalimbali za mkoa wa Kilimanjaro. Kituo cha Upendo kinawapokea pia watoito ambao mama zao wamefariki wakati wa kujifungua.

Aidha Lorenz ameahidi kuwashawishi walimbwende na wacheza filamu wengine wa Marekani kuja kushiriki katika mbio za Mt. Kilimanjaro Marathon na kutembelea vivutio vya kitalii vya nchi hii kila mwaka.

Utata Watanda Nchi Anakotibiwa Ulimboka ( Mwananchi)

 TAARIFA MPYA ZAELEZA YUKO UJERUMANI SI AFRIKA KUSINI, RAFIKI YAKE  ATOA   USHUHUDA MPYA WA JINSI ALIVYOTEKWA

Waandishi wetu
WAKATI ikielezwa kwamba Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk Steven Ulimboka anatibiwa Afrika Kusini, kuna taarifa kwamba amelazwa katika hospitali moja ya huko Ujerumani.Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa Dk Ulimboka alipelekwa Afrika Kusini lakini alikaa kwa muda mfupi tu kabla ya kupelekwa Ujerumani anakoendelea na matibabu yake sasa.

Awali, jopo la madaktari waliokuwa wanamtibu Dk Ulimboka hapa nchini lilieleza kuwa baada ya hali yake kuendelea kuwa mbaya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, waliamua kumpeleka Afrika Kusini kwa matibabu zaidi.

“Ni kweli alikwenda kwanza Afrika Kusini, lakini hapo alipita tu. Ndege ilitua na akaunganisha ndege nyingine kwenda Ujerumani,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
Hata hivyo wakati chanzo hicho kikieleza hivyo, mmoja wa wanafamilia yake, alisema: “Sisi katika level (ngazi) ya familia tunajua yuko Afrika Kusini lakini hii haiwazuii madaktari kumhamishia kwenye hospitali nyingine wanayoona inafaa.”

Mwanafamilia huyo ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alisema suala la Dk Ulimboka kuhamishiwa Ujerumani si la ajabu kwani anachotafuta ni matibabu ya uhakika.

Alipoulizwa kuhusu habari hizo, Kiongozi wa Jopo la Madaktari waliokuwa wakimtibu, Profesa Joseph Kahamba alisema: Mimi ndiyo kwanza nasikia, lakini kwa nature (aina) ya tukio lake, si vyema ikaanikwa amepelekwa wapi. Pia si vizuri ikaelezwa yuko wapi ingawa tayari watu wanajua yuko Afrika Kusini.”

“Kama kiongozi wa jopo la madaktari wanaomtibu Dk Ulimboka ninajua kwamba yuko Afrika Kusini ingawa hata hiyo taarifa tusingependa watu waijue kwa jinsi tukio lilivyokuwa.”

Mmoja wa madaktari ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini alipoulizwa juu ya suala hilo alipinga na kusema; “Habari za aina hiyo mtakuwa mnazipata nyingi, najua  mtaandika, ndiyo maana mnaandika madaktari Muhimbili wanafanya kazi wakati si kweli”.

Alisisitiza kuwa Dk Ulimboka yupo Afrika Kusini  anakopatiwa matibabu na kusisitiza kuwa habari alizokuwa nazo tangu juzi jioni ni kwamba anaendelea vizuri.

Katibu wa Chama cha Taifa cha Madaktari (MAT), Dk Rodrick Kabangila alipoulizwa juu ya hali ya Dk Ulimboka alisema kwa mujibu wa taarifa za juzi jioni alikuwa anaendelea vizuri.

Alipoulizwa juu ya taarifa za kupelekwa Ujerumani aliguna kisha akasema: “Naomba ieleweke kuwa yupo Afrika ya Kusini kwa matibabu.

Rafiki asimulia mkasa

Rafiki wa karibu wa Dk Ulimboka aliyekuwa naye wakati mkasa wa kutekwa ukitokea, Dk. Deogratius Michael ameelezea tukio zima lilivyotokea na kusema ulikuwa wa kitaalamu na ulifanywa na watu wenye ujuzi na mambo hayo.

Dk Deogratius alisema jana kwamba siku ya tukio walikuwa wametokea kwenye msiba wa ndugu wa mwalimu wao Profesa Yongolo na baada ya msiba walikwenda Viwanja vya Leaders saa moja usiku kuangalia taarifa ya habari na mambo mengine.

Huko walikutana na madaktari wengine na ilipofika saa 4:00 usiku, Dk Ulimboka aliwaambia kwamba kuna jamaa alikuwa akimtafuta hivyo angependa kwenda kukutana naye.
“Tukamwuliza anamtafutia nini? Akatueleza kuwa kwa siku tatu huyo jamaa anamtafuta. Wenzangu wakasema asiende mwenyewe na mimi ndiyo nikamsindikiza. Mara ya kwanza huyo jamaa alisema anaitwa Abeid na alisema yuko Sterio, tukaenda huko hatukumkuta tukaenda Hugo hatukumkuta lakini baadaye tukakutana naye maeneo ya Barabara ya Tunis karibu na Ofisi za Ultimate Security.”

Dk Deogratius alisema wakati wakiendelea na mazungumzo, Abeid alikuwa akitaka kujua nini kinachotakiwa ili kutatua mgogoro uliopo wa madaktari.

“Wakati tunamalizia mazungumzo nilikwenda msalani, niliporudi Abeid alikuwa akizungumza na simu kila wakati, tuliendelea na mazungumzo hadi tukamaliza na kuanza kuagana,” alisema.

Alisema wakati wakiagana bado walikuwa wamekaa katika viti pamoja na Abeid... “Ghafla kuna watu walifika na kusema kuwa wanamtaka Dk Ulimboka. Walimchukua na kwenda naye katika gari. Walikuwa watano, walikuwa ‘giant’ (miili mikubwa) na ‘very skilled’ ( wenye uzoefu) wakamchukua Dk Ulimboka wakaenda naye kwenye gari,” alisema Dk Deogratius.

Alisema wakati huo Abeid alikuwa anakimbia hivyo akamkimbilia ili ampe namba yake ya simu ambayo ingemsaidia kwa mawasiliano.

“Alinipa namba yake nikampigia muda huohuo lakini nilipokuja kumpigia tena sikumpata na mpaka leo hapatikani,” alisema.

Alisema baada ya tukio hilo alimpigia mke wa Dk Ulimboka na kumweleza na pia alipiga simu polisi kuwaeleza.

“Nilikwenda polisi kutoa maelezo na nikawapa namba zangu za simu zote ili wanipigie kama watapata chochote, lakini mtu wa kwanza kunipigia asubuhi (kesho yake)  alikuwa Juma Mgaza (aliyemwokota Dk Ulimboka) ambaye alinieleza kuwa kuna rafiki yangu amempa hiyo namba na kwamba yuko hoi amepigwa.”

Alisema baada ya kupata simu hiyo aliwasiliana na watetezi wa haki za binadamu ambao walimtaka waende pamoja na kwamba walipokuwa njiani kuelekea Kituo cha Polisi Bunju alipigiwa simu na polisi wa kituo hicho.

Kutokana na hali hiyo aliomba iundwe tume huru ikijumuisha wanasheria, madaktari na watu wengine ili ukweli ujulikane.

Upelelezi wa Polisi
Kamanda wa Polisi...www.mwananchi.tz

Utoto Mtakatifu Wa Yesu Wafanya Hija Mbeya

Maandamano ya watoto wa utakatifu wakiingia kanisa la hija kwa maandamano
                           Askofu mtega akipokwea na watoto katika kanisa la hija jijini Mbeya
Askofu mkuu wa jombo la Songea Mhashamu Norbert Mtega akiongoza maandamano hayo kuingia kanisa la Hija Mbeya

Picha kutoka Mbeya yetublog

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI 5th JULYHUYU NDIO BOSS WA FACEBOOK ALIEFUNGA NDOA NA HUYU MWANAUME MWENZAKE, NA HIKI NDIO WALICHOFANYA FACEBOOK.

Baada ya mmoja wa waanzilishi wa mtandao wa kijamii wa facebook Chris Hughes kufunga ndoa ya jinsia moja na mpenzi wake wa muda mrefu bwana Sean Eldridge jumamosi iliyopita huko New York City, USA last Saturday, the social networking website chose to symbolically introdMtandso huo umeamua kuongeza kitufe kitakacho ashiria ndoa za jinsia moja kwenye relationship status za mtandao huo.

Kwa kawaida ilikua mtu akioa kwenye page yake ya facebook anaruhusiwa kubadilisha status ambapo kitufe cha facebook huwa kinaonyesha mwanaume na mwanamke lakini kwa sasa inaweza kuwa mwanaume kwa mwanaume au mwanaume kwa mwanamke.
           Hiki ndio kitufe walichokiongeza kwenye facebook cha ndoa ya wanaume waliooana

.Mabadiliko haya sio mapya kwenye mtandao wa facebook katika harakati za kwenda na wakati kwani 2011 facebook iliongeza kitufe cha kuonyesha kwamba ndoa imefungwa mahakamani hatua ambayo ilionekana kuunga mkono ndoa za kimahakama za watu wa jinsia moja.

Pamoja na hilo facebook imekua inatoa support kwa asasi zisizo za kiserekali ambazo zimekua zikiweka kipaumbele kwenye kutetea haki za mashoga na wasagaji.
                                                  Chris Hughes na mkewe bwana Sean Eldridge.

GOOD NEWS KWA TOTTENHAM, CHELSEA HII INAWAHUSU PIA.

Andre Villas Boas aliyekua kocha wa Chelsea kabla ya kutimuliwa muda mfupi baadae baada ya timu kuvurunda ndio ametangazwa kuwa kocha mpya wa club ya Tottenham sasa hivi.

Villa Boas (34) aliwasili London jumatatu wiki hiikufanya mazungumzo na Tottenham ambapo baada ya kukubaliana, mzigo ukatangazwa.

Kocha huyu mdogo kiumri ameanza kufundisha club kama kocha akiwa na umri wa miaka 21 tu na sasa amechukua mkataba wa miaka mitatu kwenye club yake ya tano kuifundisha.

SABABU ZA YANGA KUTOLEWA KWENYE MASHINDANO YA URAFIKI.

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) kimewafukuza Yanga katika mashindano ya Urafiki kwa kitendo cha kupeleka kikosi cha vijana (Yanga B) badala ya kikosi cha wakubwa kwenye michuano hiyo kama walivyokubaliana.
ZFA na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ujumla wamekerwa na kitendo kilichofanywa na uongozi wa Yanga na wamekichukulia kama ni dharau, kupeleka timu B badala ya timu A. (Stori imeandikwa na Bin Zubery)

ILICHOSEMA MOI KUHUSU MADAKTARI WAKE BINGWA.

Taasisi ya mifupa Muhimbili MOI imesema Madaktari bingwa 18 wa taasisi hiyo wanaendelea na kazi yao kama kawaida na hawajihusishi na mgomo kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari huku ikiendelea kutoa huduma za wagonjwa wa dharura na wale wa kawaida.

Akitolea ufafanuzi kuhusu tamko lililotolewa na jumuiya ya Madaktari kwamba Madaktari bingwa wote wamejiunga kwenye mgomo huo, mwenyekiti wa bodi ya Udhamini ya MOI Balozi Mstaafu Charles Mutalemwa amesema tangu kuanza kwa mgomo huo june 23 mwaka huu Taasisi hiyo imeendelea kuhudumia wagonjwa licha ya kugoma kwa madaktari walio kwenye mafunzo katika hospitali ya taifa Muhimbili.

Kwenye sentensi nyingine, Mutalemwa ametaka vyombo vya habari kutochanganya Taasisi ya mifupa MOI na hospitali ya taifa Muhimbili kwa sababu kila moja ni taasisi inayojitegemea na kila moja ina bodi ya maamuzi yake ingawa wanashirikiana kikazi.Thanx http://millardayo.com/

HUYU NDIO KOCHA MPYA YANGA AMBAE TAYARI AMESHATUA BONGO BADALA YA MAXIMO..

Kocha mpya wa Yanga, Mbelgiji Thom Saintfiet amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam na kulakiwa na mamia ya wapenzi wa klabu hiyo.