Thursday, January 3, 2013

Cheki kitu Kipya kutoka FBG ft Banx - Money Hunt

 Keep yo hustle on and stay Fly all day by downloading the audio to "Money Hunt" here
http://www.hulkshare.com/dl/lbf0weugrg1s/Fbg%20ft%20banx-money%20hunt%20(noiz)?d=1

TUKIO LA MOTO MADUKANI SINGIDA KATIKA PICHA


 Mkuu wa Mkoa Singida Dakta Paserko Kone ametangaza kuwa ataunda tume ya kufanya uchunguzi wa chanzo cha moto uliounguza nyumba ya shirika la nyumba la taifa na kusababisha hasara kubwa kwa wapangaji waliokuwa na maduka na makazi katika nyumba hiyo

Mkuu huyo wa mkoa amefikia azima hiyo baada ya kukosa habari sahihi za chanzo cha moto huo pamooja na kutaarifiwa kuwa kikosi cha zima moto mkoani Singida kimeshindwa kufika kwa wakati kuuzima moto huo kwa visingizio mbalimbali ikiwemo kukosa maji na uchakavu wa matari ya gari la kuzima moto

 Mmoja wa wapangaji waliokuwa wanaishi na kufanya biashara ndani ya Nyumba hiyo ni pamoja na Bi Aida Mlei ambaye alifanikiwa kumwokoa mwanae mwenye umri wa miaka mitano amesema kuwa yeye hajui nini hasa chanzo cha moto huo kwani mwanae huyo ndiye alikuwa anaangalia runigna sebuleni ambako kulikuwa na makochi, jiko la umeme na gesi, kabati la vyombo, magunia ya mchele ambavyo vimeteketea vyote
Kwa mujibu wa jirani wa nyumba hiyo Bwana Saduni Halfani amesema kuwa zima moto zilizotumika zimetoka majumbani kwao kwani gari la zima moto lilishindwa kutoa huduma hiyo kwa kuwa na matatizo yaliyosemekana kuwa ni ya kiufundi
hili ni tukio la pili kwa nyumba ya biashara kuungua moto mjini singida katika eneo la soko kuu, na lawama zote kupelekwa kwa kikosi cha zima moto

Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha kuzima moto Bwana Kelvin Mapunda amekiri kuwa gari la zima moto lilikuwa na matatizo ya matairi hatimaye kushindwa kutoa msaada wakati wa ajali hiyo
huyu ni mmoja wa wananchi ambaye alijitosa ndani ya nyumba hiyo kujaribu kuokoa uhai wa binadamu, hata hivyo alipata majeraha na kupata huduma ya kwanza.

Taarifa za awali zinaonesha kuwa, hakuna kifo kilichotokea na thamaniya mali zilizoharibiwa haijafahamika.

Standard Radio Itaendelea kufuatilia na kuendelea kukuletea taarifa zaidi

Habari hii imeandaliwa na EUFRASIA MATHIAS, SAADA SALUM MASOUD na SAMUEL LUCAS, Picha na Standard Radio FM

MAANDAMANO DHIDI YA BOMBA LA GESI: KILIO CHA UWAJIBIKAJI

                                               Maandamano dhidi ya Bomba la Gesi

'Dar inachangia asilimia 80 ya mapato. Kitovu cha Uchumi. Dar inachangia 90% ya ufisadi. Uti wa mgongo wa ufisadi nchini'

Malumbano kati ya wananchi wa Mtwara na Serikali kuhusu matumizi bora ya utajiri wa nchi yameendelea kwa takribani wiki moja sasa. Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Waziri wa Nishati na Madini kuwaita Watanzania wa Mtwara Wahaini, wapuuzi na watu hatari, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naye aliingia kwenye mjadala huo kwa kuonya watu wanaowaunga mkono watu wa Mtwara na kuwaita watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa na wanaotaka kugawa nchi. Siku moja baada ya hotuba ya Rais, Waziri wa Nishati na Madini alifanya mkutano na waandishi wa habari kueleza suala lile lile ambalo bosi wake alilielezea usiku wa kuamkia mwaka mpya 2013. Hii ni dalili ya Serikali kuweweseka.

Katika kauli ya Serikali, ambayo haikuwa na jipya zaidi ya wimbo ule ule wa ‘kugawa nchi’ ‘umaarufu wa kisiasa’ nk, Serikali ilitaka kuonyesha umma kuwa watu wa Mtwara hawana shukurani. Kwamba miaka yote toka Uhuru watu wa Mtwara wamekuwa wakilishwa na Pamba, Kahawa, Chai, Tumbaku, Sukari, Kidatu nk. Kwamba watu wa Mtwara na Lindi hawakuchangia hata kidogo kwenye hazina ya Taifa. Hivyo wao kupigia kelele gesi yao ni uchoyo na roho mbaya na kukosa shukurani. Kauli ya Serikali ni kauli ya chombo kinachoendelea kukosa ‘legitimacy’ ya kuongoza taifa. Ni kauli ya kukata tamaa. Ni kauli hatari sana dhidi ya Watanzania waliojitolea damu kulinda uhuru wa nchi yetu.

SITAONGELEA SUALA LA URAIS 2015 - ZITTO KABWE

                                Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Zuberi Kabwe.

Ngoja niweke wazi kabisa. Ninaulizwa sana kuhusu suala la Urais 2015 baada ya kauli za wanachama waandamizi wa CHADEMA kunukuliwa kuzungumzia suala hilo. Jibu langu kwa wote wenye kutaka kusikia kauli yangu ni kwamba 'katika moja ya maazimio yangu ya mwaka mpya 2013 ni kutoongelea kabisa suala la Urais 2015. Hivyo sitaongelea suala hili. Sitasema kitu kuhusu suala hili mpaka baada ya Katiba mpya kupatikana na chama changu kuweka utaratibu na mchakato wake'. Maneno haya yameandikwa na Zitto katika ukurasa wake wa Facebook mu...

MANENO YA MWISHO ALIYOYASEMA MAREHEMU SAJUKI KUHUSU WASTARA.

                                                                   Millard na Dinno.

Mwigizaji Dinno alikua rafiki mkubwa sana wa Marehemu Sajuki na ndio alikua analala hospitali na Sajuki pale Muhimbili.

Ameongea Exclusive na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutoa maneno ya mwisho ambayo aliyasikia kutoka kwa Sajuki akimzungumzia mke wake ambae ni Wastara.

Kwa haraka haraka mwigizaji Wastara amesifiwa sana na watu mbalimbali kwa moyo wake wa ushujaa wa ukweli wa upendo kwa Sajuki japo walipitia matatizo makubwa na mengi kwenye maisha yao.

Masanja Mkandamizaji na Arnold Kayanda ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopaza sauti zao kupitia mitandao ya kijamii kumsifia Wastara kwa moyo wa upendo.

Tukirudi kwa Dinno, namkariri akisema “tulipokuwa Arusha sisi watatu tu Sajuki alionyesha ishara ya kukata tamaa, siku moja tulikua hotelini usiku kama saa tisa hivi Wastara alikuja kuniamsha kwenye chumba changu nikaenda kwa Sajuki, alikua anaumwa sana akamwambia Wastara naomba mpigie mama niongee nae, Sajuki akamwambia mama yake mzazi kwamba Wastara nampenda sana, kanizalia mtoto mzuri anaitwa Farhini, naomba msimsumbue naomba msimpe shida yoyote amenisaidia sana, naomba mumwachie Farhini amlee amtunze mtamuona, yalikua maneno mazito sana mpaka machozi yakawa yananitoka”

Kwenye mstari mwingine Dinno amesema jambo jingine ambalo Sajuki aliliongea mwishoni ni kuhusu upendo miongoni mwa wasanii wa movie Tanzania, namkariri akisema “alikua ananiambia hebu jitahidi kuwa unakaa na wasanii, unajua sisi hatupendani Dinno ila mimi iko siku nitakuja kuropoka nikae na watu niwazungumzie tuweke upendo pamoja, tukishapendana tutafanya kitu Dinno”

Posted: by MillardAyo

BEI YA NISHATI YA MAFUTA YASHUKA NI PETROL, DISEL NA MAFUTA YA TAA


MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), imetangaza bei kikomo cha bidhaa za mafuta kinachoonyesha kuwa petroli, dizeli na mafuta ya taa zimeshuka kuanzia leo.

Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu imesema bei hizo zimepungua ikilinganishwa na toleo lililopita la Desemba 5, mwaka jana.

“Katika toleo hili, bei za rejareja kwa petroli, dizeli na mafuta ya taa, zimepungua kwa viwango vifuatavyo: petroli Sh126 kwa lita sawa na asilimia 5.96; dizeli Sh32 kwa lita sawa na asilimia 1.60 na mafuta ya taa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.50,” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa punguzo hilo, bei ya rejareja ya petroli katika jiji la Dar es Salaam itauzwa kwa Sh1,993, dizeli Sh1,967 na mafuta ya taa Sh1,973.

Arusha petroli ni Sh2,077, dizeli Sh2,051 na mafuta ya taa Sh2,057.
Katika jiji la Mbeya petroli itauzwa kwa Sh2,099, dizeli Sh2,074 na mafuta ya taa Sh2,079 na jijini Mwanza, petroli itauzwa kwa Sh2,142, dizeli Sh2,117 na mafuta ya taa Sh2,122.

Taarifa imefafanua kuwa mbali na kupungua bei hiyo katika uuzaji wa rejareja, bei pia imepungua kwa katika uuzaji wa jumla ikilinganishwa na matoleo mawili yaliyopita.

“Bei za jumla kwa kulinganisha matoleo haya mawili zimepungua kama ifuatavyo: petroli kwa Sh126.10 kwa lita sawa na asilimia 6.17; dizeli kwa Sh32.48 kwa lita sawa na asilimia 1.69 na mafuta ya taa kwa Sh50.74 kwa lita sawa na asilimia 2.6,” alisema.

Mkurugenzi huyo amesema katika taarifa hiyo kuwa mabadiliko hayo ya bei, yametokana na kupungua kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na kuimarika kidogo kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2008, bei za bidhaa za mafuta ya petroli, zitaendelea kupangwa na soko. “Ewura itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.

Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya uamuzi stahiki kuhusu ununuzi wa bidhaa za mafuta,” alisema Masebu.

Hata hivyo, Masebu alisema pamoja na mpango huo wa Ewura kuweka bei ya kikomo, kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa hizo kwa bei ya ushindani, ilimradi ziwe chini ya bei hiyo kikomo.

Alivitaka vituo vya mafuta kuchapisha bei hizo mpya katika mabango yanayoonekana bayana na kuonyesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika.

“Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta kutoka kwenye vituo vinavyouza mafuta kwa bei ndogo zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika,” alisema.

Masebu aliwashauri wanunuzi kuchukua stakabadhi ya malipo inayoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita ili itumike baadaye kama kidhibiti endapo kutajitokeza malalamiko ya ama kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko ya kikomo au yenye kiwango cha ubora kisichofaa.

Magazeti ya leo Alhamisi January 3rd 2013

Tazara yaandaa safari kwenda Selous siku ya wapendanao

UONGOZI wa Shirika ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara) umesema unaandaa safari ya kitalii katika Hifadhi ya Selous maalum kwa Siku ya Wapendanao ‘Valentino’ itayofanyika Februari 14 kila mwaka.

Sababu hasa za kufanya hivyo ni kutokana na mafanikio iliyopata katika safari iliyofanyika Desemba 29 mwaka jana katika kukamilisha sherehe za Sikukuu za mwisho wa mwaka.
Katika safari iliyopita iliyojumuisha wafanyakazi wa kampuni moja ya habari ilipokewa vizuri na watu wengi ambao waliwashukuru viongozi wa Tazara kwa kuwapa nafasi hiyo licha ya kuwa walichelewa kutoa taarifa ya kuwepo kwa safari hiyo.

Akizungumzia mrejesho wa safari iliyopita, Meneja Masoko wa Tazara Hemed Msangi alisema ziara hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa kwa sababu watu wengi waliitikia vizuri tofauti na matarajio yao.
Sababu hiyo inawafanya kuandaa safari nyingine tena ili kuwaridhisha wateja wao.

“Tumepanga kuwapeleka tena wateja wetu katika Hifadhi ya Selous tarehe 16 Februari mwaka huu ili kutoa nafasi ya kufurahi pamoja katika Siku ya Wapendanao ambayo hufanyika Februari 14 kila mwaka, hivyo wananchi wajiandae tena,” alisema Msangi.

Msangi aliongeza kuwa kwa sasa wanawasiliana na wadau wengine ili kukamilisha maandalizi ya safari hiyo ili iwe na mafanikio makubwa zaidi ya ile iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

“Tumepata changamoto nyingi katika safari iliyopita, vilevile tumepata maoni mengi ya namna ya kuboresha huduma yetu hivyo tunaahidi kuwa tutayafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa na kuhakikisha kuwa tunakidhi haja za wateja wetu,” alisema Msangi.