Monday, January 14, 2013

RAIS KIKWETE KATIKA UFUNGUZI WA SKULI YA MLIMANI MATEMWE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wazee wa matemwe kuitumia fursa waliyopata ya kujengewa Skuli ya kisasa katika kijiji hicho kwa kuwasimamia vijana wao kupata elimu.

Rais Kikwete ameeleza hayo katika ufunguzi wa skuli mpya ya Mlimani Matmwe ambayo ni miongoni mwa skuli 19 zilizomo kwenye mradi wa Uimarishaji wa Elimu ya lazima Zanzibar (ZABEID) ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema wazazi wanapaswa kuwa karibu zaidi katika maendeleo ya elimu ya watoto wao kwa kuwapatia mahitaji yao ya lazima na hata kujinyima katika baadhi ya mambo na kuwapa ushauri wa mara kwa mara.

“Fursa waliyopata vijana wenu hivi sasa ilikosekana hapa Matemwe kwa miaka mingi kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar, hivyo mchango wenu ni muhimu katika kujenga maisha bora ya baadae ya watoto wenu”, amesema Dk. Kikwete

Habari za Magazetini Leo Jumatatu ya 14th January 2013