Monday, December 17, 2012

Filikunjombe Anena Mbele Ya Mangula

Viongozi   wa CCM mkoa  Njombe  wakishirikiana na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Phili Mangula ( wa pili kulia ) kuwaongoza  wanachama wapya wa CCM zaidi ya 600 waliojiunga na CCM jana wakati wa mapokezi ya makamu huyo  wa kwanza  kulia ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini na spika  wa bunge Anne Makinda  wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga ambae ni mbunge wa jimbo la Njombe kasikazin na anayefuatia ni katibu wa CCM mkoa wa Njombe Hosea Mpangike

                                                Deo Filikunjombe miongoni mwa wananchi

                               Msafara wa pikipiki kwenye mapokezi ya Mangula Njombe

MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe awakuna wapiga kura wa jimbo la Njombe Kaskazini Linaloongozwa na mbunge wake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga Kwa kuwalipua watendaji wabovu serikalini ,mbele ya makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi ( CCM) Tanzania bara  Philip Mangula.

Filikunjombe ambea alipewa nafasi ya kusalimia katika mkutano huo mkubwa wa mapokezi ya Mangula mkoani Njombe alisema kuwa masikitiko ya wananchi juu ya serikali ya CCM yanatokana na baadhi ya viongozi wabovu ndani ya Chama na serikalini ambao wamekuwa wakifanya kazi chini ya kiwango na kupelekea wananchi kukichafua Chama tawala.

" Ndugu zangu wananchi wa Makambako na mkoa wa Njombe Chama chetu CCM ni Chama kizuri sana na safu hii ya sasa chini ya Rais Kikwete ,Kinana na Mangula ni safu ya uhakika na itakiwezesha Chama  chetu kuendelea kuaminiwa zaidi na watanzania ...ila tatizo ni viongozi wachache wa serikali wasiowajibika katika nafasi zao"kauli iliyowakuna wananchi na kushindwa kujizuia kushangilia huku wakiimba wewe ni Jembe .

Hata hivyo Filikunjombe alisema kuwa ili Chama kuendelea kupendwa na akina Mangula na Kinana wanapaswa kusaidiwa na watanzania wote kwa kuombewa zaidi ili kuendelea kuifanya kazi hiyo bila woga ndani ya chama.

Kwa Upande wake  Mangula mbali ya kusifu mapokezi makubwa ya kihistoria Katika mji wa Makambako na Njombe mkoani Njombe aliweza kutoa  ya Moyoni kuhusu Kati yake na Rais Jakaya Kikwete kwa Madai kuwa yeye alikuwa hajui chochote juu ya uteuzi wake na kuwa alisitaajabu kupokea simu ya Kikwete kuhusu kusudio la uteuzi wake.

" Kweli Mimi nilikwenda Dodoma katika mkutano mkuu wa CCM Kama mualikwa ila Nikiwa Hotelini nilipokea simu ya mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Kikwete akiomba kuniteua kuwa makamu mwenyekiti na baada ya kwenda Ukumbini wajumbe wote walinipa kura zote za ndio...kweli namshukuru sana mwenyekiti wangu na wanachama wote na sasa ni kazi zaidi na sitawaangusha"


Hata hivyo aliwataka wana CCM kufanya vikao bila kuchota na kuwa wasizingizie kukosa ajenda kwani hata kukosa ajenda ndani ya CCM ni ajenda Kukosa agenda pia ni agenda ndani ya CCM pia yaweza kuwa ajenda.

Aidha amehimiza  nidhamu na taratibu ndani ya CCM kuendelea kuzingatiwa ili kukiwezesha Chama kuwa na amani na kuwa iwapo taratibu ndani ya  Chama hazitazingatiwa upo uwezekano wa Amani ndani ya nchi kutoweka.

Alisema kuwa haitapendeza kuona Tanzania inafika mahali inaendeshwa  bila Chama iwapo tutaruhusu wasiopenda Amani kuendelea kuvuruga Amani yetu iliyopo...

Picha na Said Ng'amilo wa Mjengwablog, habari na Francis Godwin

No comments: