Sunday, August 26, 2012

HII KALI JAMANI WATANZANIA MILLA NA DESTURI TUMEZITUPA WAPI??????: MTOTO AOA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA BABA YAKE KUFARIKI.

                                                Joseph Mapunda (Mtoto)
                                                     Mama Condorada Ngonyani

                                    Mama na Mtoto wake(Mume na Mke)

Mama Condorada Ngonyani mwenye umri wa miaka 70 anaishi kinyumba kama mke na mume na mwanaye wa tatu wa kumzaa mwenyewe akidai kuwa mara baada ya kufariki mume wake, Mzee Mapunda alimchagua mtoto wake amrithi baba yake.

Wananchi wa Mkoa wa Ruvuma wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Maendelo ya Jamii, Jinsia na wtoto kuangalia kati sheria inayomruhusu Mtoto na Mama Mzazi kuweza kuishi kindoa

Umati wa watu wapatao 400 ulifurika kwa Mganga wa Jadi Flora Ndembo Namabengo wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma wakiiomba Serikali ichukue Mkondo wa Sheria dhidi ya condorada ngonyani na joseph Mapunda.

Joseph Mapunda mwenye umuri wa miaka 40 amesema ameweza kuishi kindoa na Mama yake Mzazi Condorada Ngonyani 70 baada ya yeye kukubaliana wenyewe yeye na mama yake mzazi kuishi kindoa kama mume na mke.

Joseph Mapunda ana sema upendo ni upendo amempenda mama na anaishi kindoa wamependana nyie watu mnataka nini kwetu ?

Alipo ulizwa Mama alikiri kuwa kweli wameishi kindoa kwa miaka 10 na anampenda Mume wake ambaye ni Mtoto wake Joseph Mapunda.

Mama Condorada Ngonyani anasema mara baada ya kufariki mume wake Mzee Mapunda alimchagua mtoto wake amrithi baba yake.

Chanzo:blog ya Wananchi

No comments: