Thursday, February 4, 2016

Wema Sepetu amekua Mtanzania wa pili kufikisha followers milioni moja Instagram


Ikiwa ni siku chache baada ya mwimbaji Diamond Platnumz kuwa msanii wa kwanza wa bongo fleva kuwa na wafuasi milioni 1 kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, mwigizaji Wema Sepetu ameiandika rekodi kwa kuwa staa wa pili Tanzania kufikisha followers milioni moja.

Huku Tanzania ikitajwa kuwa ya kwanza kwa utumiaji wa mtandao wa Instagram Africa, mastaa wengine wenye followers wengi ni pamoja na Vanessa Mdee mwenye zaidi ya laki nane na elfu 40, Jokate mwenye zaidi ya laki nane na elfu sitini na Ommy Dimpoz mwenye zaidi ya laki saba.

No comments: