Thursday, September 13, 2012

TAARIFA KUTOKA MITANDAO YA KIJAMII ZINAPASHA KUWA DR. DALALY KAFUMU AMEPATA AJALI

Dr. Dalaly Kafumu amepata ajali ya kupinduka na gari akielekea kwenye kijiji kimoja kilichopo kata ya Mwisi ambako alikuwa anaelekea kushiriki mazishi ya Mama mmoja maarufu. Ajali hiyo ilitokea jana ambapo gari ilipoteza uelekeo kutokana na hitilafu ya barabara na hivyo kuvutwa, kugonga gema na kupinduka mara moja na gari kukaa matairi juu.

Gari iko nyang’anyang’a huwezi amini kama kuna mtu ametoka salama, lakini tunavyoongea hapa Dr. Kafumu na kijana wake ambaye alikuwa akiendesha walitoka salama. Dk. Alibanwa na Airbags na walilazimika ili kumtoa kuvunja vyuma kwa shoka na kumkuta amezimia na alizinduka baada ya muda kidogo, pia alikuwa na bruises zilizokuwa zinavuja damu sana kichwani na alilazwa hospitali ya Nkinga na asubuhi hii atapewa ruhusa arudi nyumbani.   

Amekuwa jimboni humo toka Jumatatu akifanya ziara ya kukamilisha miradi ya maendeleo aliyoianzisha, pia kuwaondoa mashaka wananchi kuwa hatowatelekeza kwa kuwa ametolewa Ubunge, na kwamba bado yuko nao pamoja tu.

Taarifa hizi hazijathibitishwa na bado tunaendelea kutafuta mawasiliano na kamanda wa polisi mkoani Tabora ili kupata ukweli wa tukio hilo

No comments: