Monday, December 10, 2012

Udahili Wanafunzi Wa Kitivo Cha Afya Kuongezwa


Serikali inatarajia kuongeza udahili wa wanafunzi wanaosomea masomo katika sekta ya afya nchini kutoka wanafunzi 7500 hadi 10,000 kwa mwaka ifikapo 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wadau wa chanjo barani Afrika uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi amesema udahili huo utasaidia kukabiliana na changamoto ya uhaba wa watumishi katika sekta hiyo.

Waziri Mwinyi amesema uhaba wa wafanyakazi katika sekta ya afya umesababisha kutowafikia watoto wote nchini ili kuwapatia chanjo za magonjwa mbalimbali.

Kwa upande wake muwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) hapa Tanzania, Lufaro Chatora amesema shirika hilo likisaidiana na Wizara ya Afya wanafanya jitihada ya kuongeza magari ili kuwafikia wototo wote na kuwapatia chanjo.Mkutano huo wa siku tatu unawakutanisha wadau 200 wa huduma ya chanjo kutoka nchi mbalimbali barani afrika ambapo pamoja na mambo mengine watajadili jinsi ya kuboresha na kuimarisha huduma ya chanjo.

Na Veronica Kazimoto – MAELEZO

No comments: