Wednesday, March 27, 2013

KITABU CHA KIFO NI HAKI YANGU CHAZINDULIWA RASMI


 Mtunzi mashuhuri wa vitabu kutoka kampuni ya Mkuki na Nyota, Mzee Walter Bgoya, akikata utepe pamoja na mtunzi wa kitabu cha ‘Kifo ni Haki Yangu’, Eric James Shigongo (kulia) wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam.
 Mtunzi Eric Shigongo akimpatia kitabu mtunzi mwenziye, mzee Walter Bgoya.

Mzee Walter Bgoya akiongea na wanahabari wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Eric Shigongo cha ‘Kifo ni Haki Yangu’.

Mtunzi wa kitabu cha ‘Kifo ni Haki Yangu’, Eric James Shigongo, akiongea na wadau (hawapo pichani) waliofika katika uzinduzi wa kitabu chake katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House lililopo mtaa wa Samora jijini Dar.

Eric Shigongo akimsainia kitabu mwanaye, Samwel Shigongo.

Shigongo akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa duka la TPH.

Eric Shigongo (kushoto), akibadilishana mawazo na msomaji wa hadithi zake, Ahmed El Maamry, wakati akimsainia kitabu.

MTUNZI mahiri wa vitabu nchini, Eric James Shigongo, leo amezindua rasmi kitabu chake cha ‘KIFO NI HAKI YANGU’ katika duka la vitabu la Tanzania Publishing House (TPH) lililopo mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, wasomaji 50 wa mwanzo walipata fursa ya kupata zawadi ya kitabu hicho bure kilichosainiwa na mtunzi. Kujipatia nakala ya kitabu hicho na vinginevyo, wasiliana au fika katika vituo tajwa hapo chini:No comments: