Monday, March 4, 2013

PAPA AWAAGA RASMI WAUMINI WA KANISA CATHOLIC

 -UTUMISHI wake umekoma rasmi 28th ,02 ,2013, aaga kwa mawingu mazito, jua lawaka ghafla

ILE historia ambayo haijawahi kuwepo kwa miaka 600 iliyopita ya papa kujiuzulu inafikia tamati Alhamisi 28th February 2013 ambapo Papa Benedict XVI ameachia rasmi uongozi wa Kanisa Katoliki Duniani.

Jumapili iliyopita katika Uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Petro, jijini Vatican, maelfu ya waumini wa madhehebu hayo walijitokeza kumuaga wakati alipowabariki katika ibada yake ya mwisho wa utumishi ambapo alisema ilikuwa Februari 28, 2013.

Papa mwenye umri wa miaka 85 ambaye ni mzaliwa wa nchini Ujerumani aliwaambia waumini hao waliokadiriwa kufikia laki moja (100,000) kuwa, Mwenyezi Mungu amemuita kwa njia nyingine na kwamba kujiuzulu kwake ni matakwa yake binafsi wala hakuna shinikizo.

Papa aliyasema hayo kwa sauti yenye nguvu na mamlaka lakini iliyokuwa ikiashiria kutetemeka ambapo umati huo ulijikuta ukijawa na simanzi.

Awali mawingu mazito yalitanda na mvua kubwa kutarajiwa kunyesha jijini humo na watu kuhofia kujitokeza, lakini kengele ilipolia kuashiria muda wa papa kuzungumza na watu umewadia, mawingu yalitoweka na kuacha jua likimulika kwenye anga ya bluu jambo ambalo papa huyo alimshukuru Mungu kwa kusema:

“Tunamshukuru Mungu kwa kutupatia jua,” kauli iliyoibua furaha kwa watu.

Jijini Dar es Salaam habari za uhakika zinasema kuwa, Kadinali Pengo aliondoka wiki iliyopita kwenda Vatican kuhudhuria zoezi la mchakato wa kumchagua papa mpya.

No comments: