Tuesday, May 28, 2013

JACK WOLPER ALIA NA MATAPELI YANAYOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII KWA JINA LAKE KUOMBA HELA WATU

Katika kile kinachoonekana ni mwendelezo wa matapeli wa mjini kutumia majina ya waigizaji maarufu nchini kutapeli watu kwa njia ya mtandao, dhahama hii sasa imemkuta mwanadada Jacqueline wolper baada ya watu wanaoaminika kuwa ni matapeli kutumia jina lake kujipatia fedha na vitu vingine kiudanganyifu.

Akizungumza kwa simu na tovuti ya bongomovies, mwanadada Jacqueline wolper  alisema matapeli hawa sasa wameamua kutumia mtandao wa instagram na mtandao mwingine wa kijamii uitwao badoo kwa jina la “wolper gambe25” katika kutapeli watu kwa kuwaomba hela au michango mbalimbali kupitia account hizo feki

“Leo nilikuwa naenda saluni, baada ya kufika tuu, yule dada wa saluni akaanza kunilalamikia kuwa mbona sijaenda kuchukua viatu nilivyomuagiza pamoja na hela?

Nikawa sijui cha kumwambia maana sikumuagiza viatu na wala sijampigia simu kumwambia anitumie hela, ndipo aliponionesha huo ujumbe kwenye simu yake na ndio nikagundua hizo account feki za hao watu wanaoutumia jina langu kutapeli watu” Alisema Jack.

“Mimi sipo facebook na wala sitarajii kujiunga, nawaomba sana mashabiki wangu wajue hilo. Natumia mtandao wa instagram kwa jina la wolpergambe au jacklinewolperjacklinewolper.” Alisisitza Wolper

Pia alisema kuwa amegundua leo kuna mtu mwingine anayetumia jina lake kuomba watu wamchangie kuhusu kampeni inayoitwa “Zinduka” na amewataka sana mashabiki wake wasije wakafanya hivyo kwani mtu huyo ni mwizi na analengo la kumchafulia jina lake.

No comments: