Wednesday, February 3, 2016

Wema Sepetu Aelezea Kwa Kina Beef yake na Zari, ‘Sio Nasib Wala sio Mwanamke Wake, Wote Waniache’


Wema Sepetu amefunguka kwa mapana kuhusiana na ugomvi wake na Zari the Bosslady ulioshuhudia warembo hao wakibadilishana michambo kwenye Instagram.


Miss Tanzania huyo wa zamani alikuwa akihojiwa kwenye Ijumaa hii kwenye kipindi cha Ala za Roho cha Clouds FM. Alikuwa ameongozana na mpenzi wake, Idris Sultan.

Mimi nilivyoamua kuwa out of Diamond’s life niliamua hivyo and I am out of Diamond’s life. I don’t know why watu wanajaribisha sana kunibring back to his life wakati I have already like moved on,” alisema Wema.

“I accepted my break up with Diamond from the beginning and I never wanted anything to do with him, nilivyoamua kwamba this is is going to be it nikaamua. Mimi na Diamond tumeachana 2014 and I was the one who actually decided that it’s going to be over. Lakini wakati Diamond ameshamove on ameshakutana na girlfriend wake, mama wa mtoto wake mimi sikuwahi kujihusisha katika mambo yao. Lakini I think the girl (Zari) anakuwa kama ana kitu na mimi. I have been quite for a very long time, first year nimekaa kimya, second year nimekaa kimya, it’s like kama vile anataka kunichokonoa,” alifafanua.Wema alisema kuwa kuna wakati Zari alikuwa anatembelea ukurasa wake wa Instagram na kulike baadhi ya post zake lakini aliamua kumblock ili kuepusha shari.

“Nilivyomblock nikaona sasa anaendelea,ataongea atamtag Esma sasa nikitagiwa mimi nakuta kwenye ‘photos of you.’ Anasema ndipo alipogundua kuwa Zari amemwandikia maneno makali yaliyomuumiza kiasi cha kuamua kuuvunja ukimya wake.

“So I said what I have to say, kwasababu najua at that point nimwambie tu kitu ambacho kitamkera, sijui kuhusu mtoto wao that’s their life na sitaki kujihusisha. So nikafanya hivyo ili naye kumkera kwasababu lengo si ni kukerana.”

Wema anasema baada ya kumjibu hivyo Zari, mpenzi wake Idris alimgombeza sana kwakuwa hakufurahia. Hata hivyo amesema watu wake wa karibu walimjaza kuwa amekuwa akimvumilia Zari kwa miaka mingi sasa na kwamba ifike wakati naye ajibu mashambulizi.

“So I was like ‘okay let me do it’ so I did lakini sio kwamba nimetaka kufanya ni kitu ambacho this is not me.” Muigizaji huyo alisema ndio maana aliamua kuandika post kwake kuwa amefunzwa kutogombana na ‘watu wazima.’

Kwa upande wake Idris alisema hakupenda kitendo hicho na hapendi kuona kikitokea tena.

"Mimi sipendi, mimi na Diamond hatuna tatizo, he has been a brother to me for a long time. Naamini kwamba yeye na Wema haya mambo ni ya nyuma na yalishatokea na hakuna tatizo. Sio kwamba wewe ukishaondokkiliza sauti yake hapo chini.
a ndio umefunga basi marafiki zako wote, Diamond anajuana na watu wangapi? Kama watu wote anaojuana nao ikitokea mmoja amependana na ex wake basi nilishatoka na kaka yangu basi ndio imetoka,” alisema Idris.

Wema alimalizia kwa kuwataka Diamond na Zari waachane na maisha yake. Mrembo huyo na mpenzi wake Idris wanatarajia kupata mtoto katikati ya mwaka huu.

No comments: