Thursday, July 12, 2012

HILI NDIO PIGO JINGINE KWA MCHEZAJI RONALDINHO WA BRAZIL.

Mkali wa soka kutoka Brazil ambae ni mwezi umepita toka aondoke kwenye club ya Flamengo aliyokua anaichezea kutokana na kushindwa kumlipa mishahara yake, amepatwa na tatizo jingine kwenye moja kati ya madili yake.

Kampuni ya vinywaji ya Coca-cola imeukatisha mkataba mnene na mchezaji Ronaldinho baada ya mchezaji huyo kuonekana akiwa na vinywaji vya Pepsi pembeni wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na club yake mpya ya Atletico Mineiro.

Mkataba wake na Coca-cola ambao hauna hata mwaka toka usainiwe, ulitakiwa kwenda mpaka 2014 ambapo malipo yake kwa mwaka ni dola za kimarekani zaidi ya  laki saba.

Pepsi ni wadhamini wa club yake mpya ya Mineiro na kuwepo kwa vinywaji hivyo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari sio chaguo au uamuzi wa Ronaldinho, ni maamuzi ya club kwa sababu ndio yenye mkataba na Pepsi na sio Dinho.

No comments: