Friday, August 3, 2012

Picha Mbalimbali za Matukio ya Jana Wilaya Monduli

 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akipatiwa maelezo ya Mifugo hiyo kabla Rais Kikwete hajafika na kuigawa kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake uliozikumba wilaya hizo mwaka 2008/2009.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwa katika Mazungumzo na Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Mh. Christopher Ole Sendeka.
     
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na kina mama wa Kimasai katika kijiji cha Makuyuni











Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa alipowasili katika kijiji cha Makuyuni,Wilayani Monduli kwa ajili ya kuzindua mpango wa kugawa ng'ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha mifugo 800,000 kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.

No comments: