Monday, September 24, 2012

KAMATI KUU YA CCM YAKUTANA DODOMA, WAWANIA UONGOZI 'PRESHA' JUU

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama.
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM, mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Sheni na Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama
  Katika Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akisoma utangulizi, mwanzoni wa kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya  Kikwete na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius  Msekwa
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akiwaslimia wajumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa NEC, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba, Mjumbe wa NEC Oganaizeshenu, Asha Abdallah Juma na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, (Zanzibar Vuai Ali Vuai) kabla ya kuanza kukao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo
  Wajumbe wa Kamati Kuu, Maua Daftari na Simba wakijadili jambo taratibu, kabla ya Kikao cha kamati hiyo kuanza leo mjini Dodoma
 Baadhi ya viongozi wa CCM wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi kwa awamu nyingine katika uchaguzi mkuu wa CCM utakaofanyika Novemba mwaka huu, wakiwa nje ya ukumbi wakati kikao cha Kamati Kuu kikiendelea mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Azim Premji, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Rukwa, Hypolitus-Rukwa, Wajumbe wa NEC Asha Baraka na Hkadija Kopa
Anthony Dialo (kulia) akijadili jambo na wenzake nje ya ukumbi

No comments: