Monday, September 10, 2012

RATIBA YA MECHI ZA CHAN 2014 NDIO HII, TAIFA STARS INAHUSIKA PIA.

                                                   Soccer city Johannesburg South Africa.

Timu ya taifa Taifa stars imepangiwa kucheza na Uganda (The Cranes) kwenye raundi ya kwanza ya michuano ya kuwania ticket ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (ChAN) zitakazofanyika Afrika Kusini 2014.

Ratiba iliyopangwa sept 7 2012 kwenye makao makuu ya shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF) mjini Cairo inaonyesha Tanzania imeingia moja kwa moja raundi ya kwanza ambapo itacheza na Uganda.

Mechi ya kwanza itachezwa uwanja wa taifa Dar es salaam kati ya june 21,22 na 23 2013 wakati marudiano itakua uwanja wa Mandela Namboole jijini Kampala kati ya july 5,6 na 7 2013.

Nchi 38 zinashiriki kwenye hizo mechi za mchujo ambapo nyingine zitaanzia raundi ya awali itakayochezwa kati ya november 30 na december 1 na 2 mwaka huu wakati mechi za marudiano zitakua kati ya December 14, 15 na 16.

Ratiba imepangwa kwa makundi ya kanda ambapo jumla ya timu 16 ndizo zitakazocheza fainali hizo nchini Afrika kusini, kanda ya kaskazini itapeleka timu mbili katika fainali, kanda ya magharibi A pia timu mbili, Magharibi B timu tatu, Kanda ya kati timu tatu, Kanda ya kati mashariki timu tatu, kanda ya kusini timu tatu akiwemo mwenyeji Afrika Kusini.

Kwa upande wa kanda ya Tanzania (Kati mashariki) timu zinazoanzia raundi ya awali ni Burundi, Eritrea, Ethiopia na Kenya ambapo kama hufahamu fainali za kwanza za CHAN zilifanyika Ivory Coast 2009 ambapo Tanzania ilishiriki lakini mshindi alikua Congo DRC na fainali za pili zilifanyika 2011 nchini Sudan ambapo Tunisia ndio ilichukua ubingwa.

Fainali za kwanza zilishirikisha timu nane kabla ya kuongezwa hadi 16 za sasa.

No comments: