Saturday, October 13, 2012

Askari Polisi Wapewa Zawadi

 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Stanslaus Mulongo akimkabidhi cheti cha utendaji bora wa kazi askari wa Jeshi la Polisi mkoani humo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (ACP) Jane Warioba wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika uwanja wa michezo uliopo katika kambi ya polisi ya mjini Arusha tarehe 08/10/2012. (Picha zote na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).
 Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti kwa askari 37 wa mkoa huo waliofanya vizuri zaidi katika utendaji wao wa kazi za kila siku. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 08/10/2012 katika uwanja wa michezo uliopo katika moja ya kambi ya jeshi hilo iliyopo mjini Arusha.
 Baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi mkoani Arusha wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutunukiwa vyeti na fedha taslimu TSh 100,000 kila mmoja kutokana na utendaji mzuri wa kazi zao za kila siku.
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ili aweze kutunuku vyeti na fedha taslimu TSh 100,000 kwa kila askari ambaye alikuwa amefanya vizuri zaidi katika utendaji wake wa kazi za kila siku.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Polisi wa Mkoa huo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa michezo uliopo katika moja ya kambi zilizopo mkoani humo. Kulia kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (ACP) Liberatus Sabas akimtambulisha viongozi hao.

No comments: