Thursday, January 24, 2013

YANGA YADHIHIRISHA UBABE WAKE KWA BLACK LEOPARDS, YAIFUMUA 2-1 CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

 Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
                                   Umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo


                                                   Foleni Jamani watu kuingia uwanjani
  Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
 Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga, Said Bahanuzi na hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.

                                    Umati wa watu waliokuwa wakisubiri kuingia uwanjani
                                      Umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo
                                        Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
                                                  Kikosi cha timu ya Black Leopards.
                                                           Benchi la ufundi la timu ya Yanga.
 Ilikuwa ni patashika nguo kuchanika, mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry alifanikiwa kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha pili.


                                     Makocha wakipongezana mara baada ya mpira kuisha.
 Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo,ambapo timu ya Yanga imetoka kifua mbele goli 2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, mchezo huo umechezwa leo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Golikipa wa timu ya Black Leopards, Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.

Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.


No comments: