Tuesday, March 12, 2013

"BILA DIAMOND SINA MVUTO"...WEMA SEPETU

Wema Sepetu amefunguka kuwa anapenda kuvaa urembo wenye madini ya almasi (diamond) kwani humpendeza kuliko madini mengine.

Akizungumza na mwandishi wetu, Wema alisema amekuwa akivaa madini mbalimbali ila tangu alipoanza kuvaa ya ‘diamond’, watu wake wa karibu wamekuwa wakimsifia kuwa anatoka chicha.

“Ukiniambia nichague madini kati ya silver, gold na diamond mimi nitachagua diamond kwani yananipendeza sana, bila kuyavaa nahisi sijapendeza,’’ alisema Wema.

No comments: