Wednesday, March 20, 2013

DEREVA ALIYEMGONGA TRAFIKI JANA AMEKAMATWA

Taarifa iliyotufikia inaeleza kuwa  yule Dereva aliyemgonga askari polisi wa usalama barabarani WP 2492 CPL-Elikiza na kutokomea, amekamatwa jana usiku masaa kadhaa baada ya kupoteza uhai wa askari huyo maeneo ya Bamaga mapema jana mchana.

kwa Mujibu wa kamanda wa Polisi kikosi cha Usalama barabarani nchini,Kamanda Mohamed  Mpinga amesema leo kuwa gari lilohusika kwenye ajali hiyo limepatikana likiwa limefichwa maeneo ya Tabata dampo jijini Dar.

Kamanda Mpiga ametoa taarifa hiyo mbele ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete nyumbani kwa Marehemu,hukoUnunio,kaskazaini mwa jiji la Dar. Rais Kikwete alifika kuhani msiba huo nyumbani kwa marehemu ambaye ameacha  Mume na watoto watatu.

No comments: