Wednesday, March 20, 2013

NANCY SUMARI AZINDUA KITABU CHA WATOTO NYOTA YAKO

 Miss World Africa 2005, Nancy Sumari leo amezindua kitabu chake cha watoto kiitwacho Nyota Yako. Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu wakiwemo mamiss Tanzania wa zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe na Faraja Nyalandu.
 Nancy Sumari akizungumza kwenye uzinduzi huoNancy Sumari akizungumza kwenye uzinduzi huo

Wengine ni pamoja DAKTARI Bingwa wa magonjwa ya watoto na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Profesa Esther Mwaikambo, Jokate Mwegelo, Shaa, Ally Remtullah. Fina Mango na wanafunzi mbalimbali.
Akizungumzia jambo lililomsukuma kuandi ka kitabu hicho, Nancy alisema:
Vilinisukuma vitu vingi, kwanza nafasi ya mwanamke kwenye jamii yetu, umuhimu wake, sababu ya kumuenzi na kumsherehekea na kutambua michango yetu, mwanamke mdogo, msichana mdogo, mama zetu, bibi zetu. Kuna kila sababu ya sisi kuangaliana na kutambuana na pia kufananisha.


                                                              Ally RemtullahAlly Remtullah


 Profesa Mwaikambo akikielezea kitabu hichoProfesa Mwaikambo akikielezea kitabu hicho.
Profesa Mwaikambo akimuonesha picha ya kwenye kitabu hicho mtoto wa Nancy, ZuriProfesa Mwaikambo akimuonesha picha ya kwenye kitabu hicho mtoto wa Nancy, Zuri
 Nancy aliongeza kuwa mwanae pia alimchochea kuandika kitabu hicho.

Kwa upande wake Profesa Mwaikambo(74), ambaye mwaka huu ubalozi wa Marekani ulimtunuku tuzo ya haki ya Dk Martin Luther King amempongeza Nancy kwa kuandika kitabu hicho na kusema kuwa watoto wengi hasa wenye kuanzia umri wa miaka mitatu wataweza kukifurahiia kwa kuangalia picha tu.Akizungumzia kasumba ya watanzania wengi kutopenda kusoma vitabu na jinsi alivyokabiliana nayo Nancy anasema, “nilimshirikisha mchoraji mzuri sana kwasababu nilitaka kumvutia mtu kwa wepesi kwanza kiwe kifupi, yaani kidogo. Ni kitabu ambacho unaweza kukipitia ndani ya dakika tano. Kuna picha nyingi lakini meseji yake ni nzito sana.”
                         Farja Nyalandu akizungumzaFarja Nyalandu akizungumza


 “Baada ya mimi kuwa na Zuri nikaona kuna umuhimu wa yeye kuangalia wanawake wa kitanzania kama role models. Anaweza akawaangalia wanaojulikana akawajua pia lakini kuna kila sababu ya kuangalia wanawake wengi na michango mingi inayofanyika kwenye jamii yake akawatambua wanawake na kuwaenzi.”
 Kuhusu upatikanaji wa kitabu hicho, anasema, “kwanza nitakisambaza kwenye shule za msingi bure, halafu nitakisambaza kwenye bookshop ambako kitauzwa, kwahiyo watoto wa shule ya msingi watakuwa na access nacho bure lakini wengine wengi watakinunua kwenye bookshop. Hizo hela ambazo zitapatikana zitaprint kitabu na kukisambaza mbali zaidi.”

“Nimepata mchango mkubwa sana kutoka Bongo5 Media Group ambao wamenisaidia kufanikisha kitabu hiki, nawashukuru sana,” alisema Nancy.

Sababu baada ya kutembea kwenye shule nyingi na kuzungumza na wasichana wengi nimegundua kwamba story zetu zinafanana. Changamoto ni nyingi tunazozipitia na tunafanana kwa vitu vingi kwahiyo nikaona ni vyema nikawafananisha wasichana wengi wakamwangalia mwanamke kama Dokta Migiro wakasikiliza story yake, wakajiona kwenye hiyo hadithi, wakaona uwezo wao wa kufikia alipofikia Dokta Migiro.
 Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari King'ongo ya Kimara jijini Dar es Salaam Wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari King’ongo ya Kimara jijini Dar es Salaam

 Shaa na Nancy wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunziShaa na Nancy wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi
                   Picha ya pamoja na Nancy, K-Lyinn, Ally Remtullah na rafikiPicha ya pamoja


                                                    Nancy na FarajaNancy na Faraja
 Mamiss Tanzania wa zamani wakiwa wameshikilia kitabu hichoMamiss Tanzania wa zamani wakiwa wameshikilia kitabu hicho

                      MC wa uzinduzi huo Rebeca GyumiMC wa uzinduzi huo Rebeca Gyumi

                                          
K-Lyinn akisaini kitabu cha waliohudhuria uzinduzi huoK-Lyinn akisaini kitabu cha waliohudhuria uzinduzi huo          

No comments: