Tuesday, March 26, 2013

CHADEMA WAPOKEA MSAADA WA MILIONI 400

 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea msaada wa fedha shilingi milioni 400 kutoka Chama cha Upinzani nchini Denmark cha Conservative People’s Party (CPP), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo vijana pamoja na Wanawake Viongozi wa chama hicho.

Akizungumza wakati wa kutiliana saini Mkataba wa utekelezaji wa Mradi huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK. WILBROAD SLAA amesema awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wanachama wake kupitia Baraza la Vijana la Chama hicho, (BAVICHA), pamoja na lile la Wanawake (BAWACHA), inatarajiwa kuanza Machi, mwaka huu.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Chama cha Conservative People’s Party (CPP), ROLF AAGAARD, anaelezea lengo la chama hicho kutoa msaada huo.

Nae Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (CHADEMA), JOHN HECHE amesema msaada huo utawawezesha kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Baraza hilo katika mikoa mbalimbali nchini.

Chama cha Conservative People’s Party (CPP), kilianzishwa mwaka 1915 na kimekuwa madarakani kwa kipindi kirefu hadi kiliposhindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita nchini.

No comments: