Tuesday, March 26, 2013

HUU NDO UTAJIRI WA WEMA SEPETU.....

                                                       Wema akiwa na Mama yake
 Well, well, well! Hiki ni kitu ambacho kila mmoja anapenda kukifahamu. Wema Sepetu ni tajiri kiasi gani? Ni ngumu kusema exactly mrembo huyu ana shilingi ngapi benki, lakini mambo anayofanya yanatupa jibu la wazi kuwa, Wema ana mkwanja mrefu. So hebu tuangalie mangapi makubwa yaliyohusisha fedha nyingi aliyoyafanya kuanzia mwezi June, 2012.


 1. Thamani ya nyumba yake

Wema Sepetu aliwaacha hoi watu wengi baada ya kuonesha nyumba yake mpya exclusively kwenye kipindi cha Take One cha Clouds TV. Alisema thamani ya nyumba yake hiyo ilifikia shilingi milioni 400 na hiyo ni tofauti na karibu shilingi milioni 30 za kuipamba ndani. Hiyo ilikuwa ni tarahe za mwanzo za mwezi June, 2012.
 Dj Choka alikuwa miongoni mwa watu waliotembelea nyumba hiyo
 Wema na Zamaradi Mketema wa Clouds TV


 5. Gharama anayotumia kuwatunza mbwa wake, Vanny na Gucci
Mtandao wa Global Publisher jana uliandika, “KWA wale wenye hali ngumu kimaisha wataishia kusema; ni kufuru iliyoje kwani staa wa filamu za Kibongo, Wema Isaac Sepetu hivi karibuni amewafanyia mbwa wake wawili ‘shopping’ iliyogharimu dola 4,000 za Kimarekani (zaidi ya Sh. milioni 6.5 za madafu).

Wema aliteketeza kiasi hicho cha fedha kwa kuwanunulia mbwa hao pafyumu, viatu na nguo, alivyoagiza kutoka nchini China, lengo likiwa ni kuhakikisha wanaishi katika mazingira mazuri.

Akizungumzia ‘shopping’ hiyo nyumbani kwake Kijitonyama, jijini Dar, Wema alisema: “Kiukweli nawapenda sana hawa mbwa, ukinipasua roho yangu utawakuta ndiyo maana nataka wavae na kunukia vizuri, kinyume chake siwezi kuwa na amani. 


 2. Uzinduzi wa filamu yake Superstar
Katika historia ya Bongo Movies, hakuna filamu iliyowahi kuwa na uzinduzi wa nguvu kama wa filamu ya Wema ambayo hata hivyo haijawahi kutoka, Supastar. Katika uzinduzi huyo, Wema alimdondosha muigizaji namba moja wa kike nchini Nigeria, Omotola Jalade ambaye alimpeleka kwenye event iliyofanyika Giraffe Hotel Ocean View ambako watu mbalimbali walikutana kubadilishana mawazo na Omotola. Hiyo ilikuwa ni baada ya kushindwa kufika kwa wakati.

  4. Thamani ya ofisi na kampuni yake, Endless Fame Films
February 21, Wema alifanya uzinduzi maalum wa ofisi za kampuni yake ya Endless Fame Films zilizopo Mwananyamala jijini Dar es Salaam ambazo thamani yake ni takriban shilingi milioni 70.


 3. Gari anayomiliki
Kwa sasa Wema anamiliki gari aina ya AUDI Q7 ambayo thamani yake inafikia shilingi milioni 80. Awali ya hapo alikuwa na Toyota Mark X ambayo thamani yake ni takriban shilingi milioni 60.
Wema akiwa na mkoko wake


                                                         Wema akimuaga na Omotola
Hayo ni machache tu tunayofahamu na kwa hesabu hizo bila shaka utakubaliana nasi kuwa Wema Sepetu ana mkwanja mrefu!!!

No comments: