Monday, April 1, 2013

MIILI YA WATU ILIYOPATIKANA KWENYE GHOROFA LILILOANGUKA DAR IMEFIKIA 21 MPAKA SASA

 Miili ya watu iliyoopolewa kutoka kwenye vifusi vya jengo lenye ghorofa 16 lililoanguka jana katikati ya jiji la Dar es Salaam, imefikia 21.

Shughuli za uokoaji zilizoanza jana bado zinaendelea kwa siku ya pili huku kukiwa na taarifa za kuwepo miili zaidi kwenye vifusi hivyo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete alitembelea katika eneo la jengo hilo lililoporomoka lililopo Mtaaa wa Indira Gandhi/Morogoro.

No comments: