Tuesday, April 9, 2013

WAKATI UHURU AKIAPISHWA KENYA LEO, RAILA NA WENZAKE WANADAIWA KUJA HUKU, TAZAMA PIA HII WEBSITE ILIYOFUNGULIWA KWA AJILI YA UHURU

 Wako kwenye mbuga za wanyama Afrika Kusini wanakula bata ni Raila Odinga na wenzake wawili akiwemo Kalonzo Musyoka.

Taarifa kuhusu kina Odinga na wagombea wenza kwenda Afrika Kusini zimetokea @FORA_2013 page ya Organisation inayomsupport Odinga aliekua mgombea Urais kwenye Uchaguzi wa Kenya ambao Uhuru Kenyatta ndio katangazwa mshindi na anaapishwa leo.

Inadaiwa Raila Odinga na wagombea wenza wameamua kukwepa kuwepo kwenye kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta na kuamua kwenda Afrika Kusini kula bata.

Wakati huohuo pia kuna website imefunguliwa ambayo anuani yake ni swali kwa wote wanaofatilia, inaitwa isuhurupresident.com ambapo ukiifungua haijaandikwa wala kuwekwa chochote.

No comments: