Thursday, May 16, 2013

DR. SLAA AMKIMBIA NAPE NNAUYE KATIKA OFISI ZA ITV

Katika tukio lisilo la kawaida ambapo kituo cha Matangazo cha ITV kiliandaa mjadala wa kujadili hali ya kisiasa nchini na masuala mbalimbali ya kitaifa ambapo kwa busara za watendaji wa ITV waliwaalika wasemaji wakuu wa mjadala huo kuwa Viongozi waandamizi wa Vyama vya Siasa wakianza na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana na Katibu Mkuu wa CDM Ndugu Slaa.

Kutokana na hudhuri wa Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana ambapo amesafiri kuelekea Dodoma kwenda kuhudhuria kikao cha kamati kuu jana na kubanwa na majukumu mengine muhimu ya kichama na kitaifa, alimuagiza Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, ndugu Nape Nnauye kumuwakilisha katika mjadala huo wa viongozi wa vyama vya siasa katika kujadili hali ya kisiasa na mustakabali wan chi yetu.

Baada ya kufika katika Ofisi za ITV zilizopo mikocheni asubuhi ya Leo, Nape pamoja na Slaa walikutana na Nape kueleza kuwa atamuwakilisha Katibu Mkuu wake katika mazungumzo hayo ambapo baada ya kusikia kauli hiyo, Dr Slaa alianza kuhamaki na kudai kuwa hawezi kuongea na Nape kwa sababu anamtaja vibaya kwenye mikutano yake.


Hata busara zilipotumika za kumsihi apungumze munkari na kumtaka kuangalia umuhimu wa mazungumzo hayo na kipindi hicho kwa watanzania, bado Slaa aligoma na kuondoka katika ofisi za ITV.

Baada ya tahamaki hiyo, mijadala ya pembeni ya mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa kimsingi Slaa anamuogopa Nape katika mijadala ya kisiasa, nahii ni kutokana na uwezo wa Nape katika kujenga hoja na kuzilinda na kuzitetea hoja hizo...

Tukio hilo linadhihirisha kukosa uvumilivu wa kisiasa (lack of political tolerance) ambako viongozi wa CDM hasa Slaa wanao..... Hii ni kwa sababu Nape alimtaka aeleze ni kusemwa vibaya kupi ambako yeye Slaa anakumaanisha na akashindwa kubainisha.....
Hali hiyo pia imeonesha taswira ya political immaturity kuwa viongozi wa aina hii hawajakomaa ...

Pia, tukio hilo linaweka wazi kuwa CDM hawako tayari kuyazungumzia ana kwa ana matatizo yaliyotokana na Siasa mbovu za matusi....
Tabia hii ya kukwepa kuyashughulikia makosa ya kisiasa kutalileta Taifa letu madhara makubwa sana. ...kukataa kulikubali tatizo tulilonao la siasa mbofu zenye kuhamasisha chuki, utengano, udini, ukabila na hata kuendesha matukio ya kudhuru watu na mauaji ni makosa.

No comments: