Monday, May 20, 2013

WANAWAKE JIJINI MBEYA WAMVAA MCHUMBA WA DR. SLAA BAADA YA KUMKASHIFU MKE WA RAIS KIKWETE

UMOJA wa wanawake  wa chama cha Mapinduzi Mkoani Mbeya(UWT) umemshukia Bi.Josephine Mushumbusi ambaye ni mchumba Katibu Mkuu wa chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA kufuatia kauli za udhalilishaji dhidiya Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.

Hatua hiyo inatokana  na kauli za kiudhalilishaji zilizotolewa mwishoni mwa wiki na mchumba huyo wa Katibu Mkuu wa Chadema kuwa mama Kikwete ameshindwa kumshauri   Rais ambaye ni mume wake  kuiongoza nchi vizuri .

Kauli hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa Mbeya Bi.Priscilla Mbwaga wakati  akitoa Tamko   kwa waandishi wa habari juu ya Matusi ya wazi yaliyotolewa na Bi.Mushumbusi   kwa Mke wa Rais katika mikutano ya hadhara iliyofanyika Wilayani Mbozi Kata ya Vwawa Mkoani hapa.

Bi.Mbwaga alisema kuwa katika mikutano yake ya Hadhara Bi.Mushumbusi alidai kuwa  mama Salma Kikwete  ameshindwa kumshauri  mume wake kuingoza nchi na kuacha Twiga wakiwa wanakunjwa na kuondoka na kwamba yeye akiwa Ikulu hataacha kumshauri mume wake Dkt.Slaa katika masuala ya kuingoza Nchi

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kama umoja huo wanalaani  vikali lugha chafu na za kichochezi zinazopandikizwa  chuki miongoni mwa jamii ya watanzania .

Alisema kuwa kama umoja wa wanawake  wanalaani matusi hayo na kwamba umoja huo  ulifuatilia  mikutano  hiyo na kugundua kuwa ilikuwa imetawaliwa  na  matusi badala ya kutoa sera  kwa wananchi kuwa wanataka kufanya nini.

“Sisi kama umoja wa wanawake  Mkoa tunaeleza umma  ambao una imani na  kuwa katika utamaduni   na maadili  yao hawapendi  na wala hawajazoea kusikia matusi  katika  jamii yao hivyo wakiangalie vizuri na kwa  makini Chadema  kuwa  cha hicho kina  watu  wa maadili gani , mahali  pote  siku zote  na miaka  yote  ni matusi,kuongea uongo, uzushi  na kashfa wasimamapo majukwaani “alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha Bi.Mbwaga alisema kuwa wanawake wa mkoa wa Mbeya  wanadhani kuwa kauli ambazo zimetolewa na  Mushumbusi ni  ni za kuwadhalilisha wanawake wote wa Tanzania  kwani Mama Salma ni Kiongozi wa juu pamoja
na Mushumbusi .

“Tunamshangaa sana  Mushumnbusi anaposimama majukwaani na kutoa kashfa nzito za namna hii ni  kama nani kwa wanawake  wa Tanzania 'alihoji Mwenyekiti huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi Mkoani hapa (CCM),Bw.Amani Kajuna  alisema  kauli aliyotoa Dkt.slaa kuwa Rais Kikwete  ana Udini ni ulaghai  mkubwa  ambao anaufanya kwa wananchi  na kuendelea kuiweka nchi katika mazingira magumu .

“Kama vijana  tunatambua kuwa  Rais Kikwete ni kiongozi wa watanzania, na kwamba hana sifa ya Udini hii ajenda inaanzishwa kisiasa ili kujipatia umaarufu wa bure wa kudhani kuwa ndiyo njia ya kuwapeleka ikulu  mwaka 2015 jambo ambalo halitawezekana ,maana  watanzania hawataweza kukubali" alisema Mwenyekiti huyo.

Hata hivyo Bw.Kajuna aliendelea kusema kuwa Dkt. Slaa amekuwa akimtuhumu  Rais Kikwete kuwa  ni FREEMASON , “hebu tumuulize huyu mtu amekutana lini na Rais kwenye iman hiyo” na kwamba katika uongozi wake watanzania  wameona miradi mikubwa  ya maendeleo ya nchi yetu kwa ukuaji wa wa pato la Taifa.

No comments: