Monday, February 2, 2015

Bondia Francis Cheka amehukumiwa kwenda jela.

Bondia Francis Cheka leo February 2 2015 amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na faini ya Milioni moja laki sita kwa kosa la kumpiga mmoja kati ya wafanyakazi wake kwenye bar yake iliyopo Morogoro.

Muda mfupi uliopita Francis Cheka ameongea  na kusema ndio alikua anajiandaa kuachia simu yake na vitu vingine muhimu ili achukue karandinga kuelekea gerezani ambapo namnukuu akisema ‘imeshakua hivi tayari ila hamna noma, niko na wanangu wengine wamepigwa miaka 10 nitakua nao fresh tu ila hamna noma ni miaka mitatu tu mimi’

Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Said Msuya ambapo baada ya hayo upande wa Francis Cheka unasemekana kujiandaa kukata rufaa.

millardayo.com

No comments: