Monday, February 2, 2015

Habari njema kuhusiana na majaribio chanjo ya Ebola…


Stori kuhusu ishu ya Ebola huenda ni moja ya story zilizochukua headlines kubwa kwa mwaka wote 2014, tangu iliporipotiwa kuibuka kwa maambukizi ya ugonjwa huo Afrika Magharibi mwanzo wa mwaka 2014.

Hii inaweza kuwa habari njema kwa Waafrika na dunia nzima kwa ujumla, taarifa iliyopo ni kwamba jaribio la kwanza la chanjo ya ugonjwa wa Ebola kutarajiwa kuanza kutumika Liberia wakati wowote kuanzia sasa.

Wataalamu wanatarajia zaidi ya watu 30,000 watajitokeza katika zoezi la majaribio hayo wakiwemo wahudumu wa afya.

Katika kipindi cha mwaka mmoja zaidi ya watu elfu tisini wamefariki kutokana na ugonjwa huo ambao uliandama zaidi Mataifa ya Guinea, Sierra Leone na Liberia.

No comments: